Health care bill tapita- tumejifunza nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Health care bill tapita- tumejifunza nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hekima Ufunuo, Mar 22, 2010.

 1. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mswada wa afya uliokuwa unajadiliwa nchini Marekani Kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja sasa umepitishwa na Baraza tayari kusainiwa na Raisi Obama.

  Kwa wafuatiliaji wa siasa mjadala wake unatakiwa kutupa sisi somo kubwa sana katika medani ya Demokrasia, naamini M. M Mwanakijiji atatuandalia mada juu ya hili.

  MIMI NIMEJIFUNZA NINI?
  1. Mpambano ulikuwa kati ya Republican na Democrat, Hakuna Repblican hata mmoja aliyeunga mkono mswada huu.- Wapiganaji/ Wapamabanji waliendela na mpambano mpaka mwisho.

  2 Wale Democrat ambao hawakuwa wameridhika, hawakujificha walionyesha wazi msimamo wao mpaka zilipofanyika juhudi za kuwashawishi nao kuridhika ndipo walipoungana na wenzao- HAKUNA MSIMAMO WA CHAMA, HAKUNA KIKAO CHA KAMATI YA CHAMA NA WALA HAKUNA CHAMA KILITAKA KUNINYANGANYA KADI. yote yalikuwa maslahi ya taifa na wananchi wake.

  3. Wingi wa wajumbe wa Democrat ndani ya Baraza na pia idadi ya wajumbe wa Repblican ilikuwa ni changamoto nzuri sana kwa mswada wenyewe. siyo baraza lote kuwa la chama kimoja kama hapa kwetu. Hoja zimechambuliwa na ufafanuzi kufanyika kwa makini mpaka kila mmoja ameridhika.

  4. Maandamano niliyoyaona kwenye miji mbalimbali hakuna polisi hata mmoja aliyewapiga mabomu, Ustarabu ni wa kiwango cha juu kwa wote polisi na hata waandamanji.- kwetu inawezekana?

  Mwisho
  Nimejifunza mengi sana, hata hizi kanuni za uchaguzi zinatotungwa sasa Dk slaa asingelalamika kama mjadala wa sheria ungekuwa wa wazi kama huu wa Afya- Marekani.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  "MIMI NIMEJIFUNZA NINI?
  1. Mpambano ulikuwa kati ya Republican na Democrat, Hakuna Repblican hata mmoja aliyeunga mkono mswada huu.- Wapiganaji/ Wapamabanji waliendela na mpambano mpaka mwisho."

  Republicans wote kuunga mkono inaonyesha dalili ya partisan na kupinga mswada kwa sababu tu ume tolewa na Democrats. Kuwa mpingaji haimaanishi moja kwa moja kwamba wewe ni mpiganaji au mpambanaji.

  "2 Wale Democrat ambao hawakuwa wameridhika, hawakujificha walionyesha wazi msimamo wao mpaka zilipofanyika juhudi za kuwashawishi nao kuridhika ndipo walipoungana na wenzao- HAKUNA MSIMAMO WA CHAMA, HAKUNA KIKAO CHA KAMATI YA CHAMA NA WALA HAKUNA CHAMA KILITAKA KUNINYANGANYA KADI. yote yalikuwa maslahi ya taifa na wananchi wake."

  Hii ina tokana zaidi na mfumo wa nchi husika. Kwa mfano sisi mfumo wetu unaendana zaidi na wa Uingereza. Uingereza mbunge yuko expected kupiga kura upande wa chama chake na asipo fanya hivyo basi uanachama wake au political future yake ipo matatani. Chama tawala inakua na kikao na bungeni unapiga kura kutokana na chama mlivyo kubaliana. Pamoja na yote hayo huwezi kuniambia Uk hamna demokrasia right?

  "3. Wingi wa wajumbe wa Democrat ndani ya Baraza na pia idadi ya wajumbe wa Repblican ilikuwa ni changamoto nzuri sana kwa mswada wenyewe. siyo baraza lote kuwa la chama kimoja kama hapa kwetu. Hoja zimechambuliwa na ufafanuzi kufanyika kwa makini mpaka kila mmoja ameridhika."

  This is an advantage but it is also a disadvantage. Kuna baadhi ya jumbe walikua wana pinga siyo kwa sababu ya maslahi ya taifa bali kwa sababu ya kukosha wale ambao wana lipia gharama zao za kampeni. It's no secret kwamba Marekani kuna different lobby groups na wote hao wana tumia wabunge kwa ajili ya manufaa yao. Kuna lobbist mbali mbali wa insurance companies waliokuwa wanafanya kazi usiku na mchana mswada huu usipite. Hii ni kwa sababu maswada huu utafanya hizi insurance companies ziwe regulated zaidi na zilipe kodi nyingi zaidi.

  "4. Maandamano niliyoyaona kwenye miji mbalimbali hakuna polisi hata mmoja aliyewapiga mabomu, Ustarabu ni wa kiwango cha juu kwa wote polisi na hata waandamanji.- kwetu inawezekana?"

  My friend sijui ulikua una angalia channel zipi. Most of the discussions kuhusu mswada huu zilikua zikifanyika kwenye what are called @town hall meetings@. Kwenye hii mikutano kulikuwa na instance nyingi za kutukanana. Na hata kwenye baadhi ya maandamano kuna some instances ya mambo kwenda out of hand.
   
 3. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwnafalsafa
  Nakushukuru kwa mchango makini lakini je huoni kuwa ni somo la kujifunza hapa kwetu, hata kama tunafuata mfumo wa Uingereza je mfumo huo una manufaa kwetu?

  Kupinga kwa kutukanana kwa sababu tu hekima ya mtu imepotea siyo jambo la ajabu na hili lilikuwa linatokea kwa wananchi wenyewe siyo serikali against wananchi. hii ndiyo hoja. Huku kwetu ingekuwa ni Virungu na maji washawasha tu.

  Hata hapa kwetu tunayo hayo makundi ya kuloby lakini hayako wazi. Tunachojifunza ni kwamba wenye fedha wanaweza pia kuiyumbisha serikali kwa kupiga kampeni za chini chini. kule ni wazi hapa siyo wazi. Hivi sasa kuna strategy za wafanyabiashara kufadhili wagombea fulani fulani kwa ajili ya masilahi yao baada ya uchaguzi. (Kuwa na Idadi kubwa ya wabunge wa kukulinda bungeni. Hii wewe unaionaje?

  Respect Mkuu
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ni vigumu sana kujua somo hili lita apply vipi haswa katika nchi yetu. Jua what works for America does not necessarily work for us as Tanzanians. Na pia jua kwamba kila mfumo una faida yake na hasara zake. Kwa hiyo kusema Tanzania tuchukue tu mfumo fulani bila kuangalia hasara zake is not wise.

  Marekani is a two party state. Meaning kuna teo parties ambazo zina uwezo wa kuongoza nchi. Tanzania japo tuna jiita ni "multiparty" ukweli ni kwamba it's just one party which can hold power. Just that fact makes it hard for us to be like America. Reason why there was such debate in America is because they was a party which could stand against the ruling party. We don't have that. Wabunge wenyewe wa upinzani hawafiki hata nusu ya bunge so hawana negotiating power yoyote.

  So with just one strong party how can we achieve what you think should be a lesson for us? Or wouldn't it be better for us to find a solution which works with our current situation?
   
Loading...