Headings za Magazeti Zampakazia Kikwete

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,485
19,319
Nimesoma hii hapa:


Rais Kikwete atoa waraka wa mwisho kwa majamabazi

* Atangaza operesheni mpya, aonya serikali isije ikalaumiwa

Na Midraj Ibrahim, Muleba


Rais Jakaya Kikwete ametangaza rasmi kuanza upya operesheni ya kusaka majambazi nchini mwezi ujao.


Aliwataka majambazi kujisalimisha na wananchi wanaowaficha kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kabla ya operesheni kuanza.


Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Muleba jana, rais Kikwete alisema operesheni mpya haitajali mtu na hakutakuwa na huruma.


"Napenda kuwaarifu mwezi ujao tutaanza operesheni kubwa nchini ya kusaka majambazi," alisema Rais Kikwete na kuongeza akiseama : "mtalaumu sana, lakini mtajilaumu wenyewe kwa kuwa ujambazi unafanya binamu, mtoto wa mjomba, lakini mnawaficha, watoeni kabla operesheni hiyo haijaanza."


Rais Kikwete alisema tangu serikali yake iingie madarakani, hakuna jambo gumu lililowashinda na kwamba sasa watachukua hatua zinazotahili lakini serikali isije ikaluamiwa.


Alisema hivi sasa vumbi la majambazi limetulia, wakibuni mbinu mpya na kwamba, kabla hawajaibuka watateketezwa na salama yao ni kujisalimisha.


Akzungumzaia kuchelewa kukamila ujenzi wa wa barabara ya Kagoma-Lusahunga alisema watambana mkandarasi ili akamilishe kulingana na mkataba.


Alisema suala la ulinzi na usalama halina mjadala ni jukumu la serikali na aliwaahidi wananchi kuwa majambazi hawataachwa watambe.


Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, alimsifu Rais Kikwete kwa ujasiri wake wa kupambana na mafisadi wakubwa.


"Umeonyesha mfano, umeanza na mafisadi wakubwa wewe endelea, sisi tutawashughulikia hawa wa chini ili tukutane katikati, wewe endelea kaza uzi!" alisema Masilingi.


Masilingi alisema hawatakubali fedha za umma kufujwa na wachache na kuongeza kuwa watapambana nao, wakishindwa wataomba msaada ngazi za juu.


Akiwa wilaya ya Chato juzi, Rais Kikwete aliwashukuru wananchi kwa kumchagua John Magufuli ambaye alisema ni msaidizi wake muhimu kutokana na utendaji wake mzuri.

Heading hiyo inaonyesha kuwa Rais K. I. Kwete anawasiliana na majambazi kwa awamu; na hivi sasa ndipo amefikia awamu ya mwisho kama vile huko nyuma alikuwa akitudanganya. Hata hivyo Rais K. I. Kwete anatakiwa aachane na lugha ambazo zinaweza kuwa na tafsiri nyingi. Aliposhika usukani, alisema kuwa yule ambaye haiwezi spidi yake (Kikwete) ajitoe ili kuzuia kulaumiana. Hatujanoa mafisadi wakicuhukuliwa hatua yoyote zaidi ya huyu Ballali aliyetolewa mbuzi wa shughuli. Buzwagi, Richmond, Kiwila na kadhalika naona kama ni oda ya siku.

Ushauri wa bure kwa JK:

(a) Kila unalofanya linaingia ktika historia ya kudumu ya nchi hii; usifanye upuuzi

(b) Uliachaguliwa kwa vile watu walikuwa namtumaini makubwa sana na wewe baada ya kuwa chini ya tawala za kukatisha tamaa. Ukiboronga watakuchukia zaidi ya waliokutangulia na jina lako litakuwa chafu sana katika historia ya nchi hii kwa ubaya.

(c) Majina ya marafiki zako wote unaowakingia kifua hayamo katika historia ya nchi hii. Ukibeba uchafu wao, basi jina lako litabaki nao milele.
 
Mimi napendekeza hii heading basi,

JK KIBOKO NA ANATISHA!!!!!!!!!!


"Tangu serikali yake iingie madarakani, hakuna jambo gumu lililowashinda!!!!"

"Asema watachukua hatua kali na serikali isije ikaluamiwa"

Unaonaje hiyo heading mkuu kichuguu???????
 
Mimi napendekeza hii heading basi,

JK KIBOKO NA ANATISHA!!!!!!!!!!


"Tangu serikali yake iingie madarakani, hakuna jambo gumu lililowashinda!!!!"

"Asema watachukua hatua kali na serikali isije ikaluamiwa"

Unaonaje hiyo heading mkuu kichuguu???????

Labda anatisha kwa bla ..bla ..bla nothing NEW! tumechoshwa na uswahili...
 
Mkuu Mashoo maana yangu kwa hiyo heading ni namana ambavyo waandishi wa magazeti flani flani hapa bongo huwa wanaandika. Hivyo I just wanted to convey the other side of the book kwa hoja ya kichuguu!!!!!! Maana the condemned headings mimi naona zina unafuu kuliko utumbo unaoongelewa na JK siku hadi siku!!!!
 
Mimi napendekeza hii heading basi,

JK KIBOKO NA ANATISHA!!!!!!!!!!


"Tangu serikali yake iingie madarakani, hakuna jambo gumu lililowashinda!!!!"

"Asema watachukua hatua kali na serikali isije ikaluamiwa"

Unaonaje hiyo heading mkuu kichuguu???????

Mpigaji wa kweli huwa hatangazi. Nashangaa sana hata enzi zile za Mrema alikuwa akitutangazia kwamba ataanzia operesheni yake kwenye meli mbovu pale bandarini kesho saa fulani, akienda anakuta hakuna mtu. Kwa mtazamo wangu nadhani ni kukosa mbinu yakinifu za kupambana na mambo haya maana kutangaza hivyo ni kumpa mbinu mpya mbadala unayemkusudia. Mathalani msako wa lotion zenye kemikali zenye athari kwa binadamu utashangaa serikali hutangaza kesho tutakuwa na msako wa kuwanasa wanaouza bidhaa hii mbaya tutaanzia Kariakoo nk. Shiiiiiiiit!!!!!!!
 
Unganisha hii mada tafadhali kuna mada kama hii .Beside JK si lolote kwa utendaji ila kwa sifa na misifa ni moja wapo .
 
Mimi napendekeza hii heading basi,

JK KIBOKO NA ANATISHA!!!!!!!!!!


"Tangu serikali yake iingie madarakani, hakuna jambo gumu lililowashinda!!!!"

"Asema watachukua hatua kali na serikali isije ikaluamiwa"

Unaonaje hiyo heading mkuu kichuguu???????

jamaa anatishia mtu mzima nyau...doh salaaaala kweli huyu jamaa bingwa wa blaaha blaaaah!!

may b kwa sababu anawaju awanaodo those thing dats why anawatishia kwani hata Iyumba sijui yule pleya wa Bot si alimpiga biti kwanza???then akafukuzwa kazi?
 
Hivi hapa JK alimanisha kwamba jambazi aliyefanya uhalifu wake kabla ya kauli yake atakuwa salama?
Ukiwa na nia ya kukamata wahalifu hutakiwi kuwaambia kwamba naja kuwakamata. Blah ... blah zimezidi, anza kufanya kazi JK.
 
Sidhani kama Magazeti yana mpkazia, ni kwamba mkuu wa kaya siku zote amekuwa kiranja wa sentensi tata! kuna mahali tulijadili sana juu ya kauli zake nyingi zisizo eleweka, nadhani anapaswa kuwa makini zaidi na kauli zake!
 
Siy kwamba JK ameshindwa kuwachukulia hatua mafisadi, ni kwamba yeye kwa muono wake naona hao mafisadi wenzake ndiyo wachapa kazi. Mimi na wewe ndiyo tunaona ni jmafisadi lakini JK anaona serikali yake iko safi.
 
Back
Top Bottom