Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 14,514
- 17,139
Nimesoma hii hapa:
Heading hiyo inaonyesha kuwa Rais K. I. Kwete anawasiliana na majambazi kwa awamu; na hivi sasa ndipo amefikia awamu ya mwisho kama vile huko nyuma alikuwa akitudanganya. Hata hivyo Rais K. I. Kwete anatakiwa aachane na lugha ambazo zinaweza kuwa na tafsiri nyingi. Aliposhika usukani, alisema kuwa yule ambaye haiwezi spidi yake (Kikwete) ajitoe ili kuzuia kulaumiana. Hatujanoa mafisadi wakicuhukuliwa hatua yoyote zaidi ya huyu Ballali aliyetolewa mbuzi wa shughuli. Buzwagi, Richmond, Kiwila na kadhalika naona kama ni oda ya siku.
Ushauri wa bure kwa JK:
(a) Kila unalofanya linaingia ktika historia ya kudumu ya nchi hii; usifanye upuuzi
(b) Uliachaguliwa kwa vile watu walikuwa namtumaini makubwa sana na wewe baada ya kuwa chini ya tawala za kukatisha tamaa. Ukiboronga watakuchukia zaidi ya waliokutangulia na jina lako litakuwa chafu sana katika historia ya nchi hii kwa ubaya.
(c) Majina ya marafiki zako wote unaowakingia kifua hayamo katika historia ya nchi hii. Ukibeba uchafu wao, basi jina lako litabaki nao milele.
Rais Kikwete atoa waraka wa mwisho kwa majamabazi
* Atangaza operesheni mpya, aonya serikali isije ikalaumiwa
Na Midraj Ibrahim, Muleba
Rais Jakaya Kikwete ametangaza rasmi kuanza upya operesheni ya kusaka majambazi nchini mwezi ujao.
Aliwataka majambazi kujisalimisha na wananchi wanaowaficha kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kabla ya operesheni kuanza.
Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Muleba jana, rais Kikwete alisema operesheni mpya haitajali mtu na hakutakuwa na huruma.
"Napenda kuwaarifu mwezi ujao tutaanza operesheni kubwa nchini ya kusaka majambazi," alisema Rais Kikwete na kuongeza akiseama : "mtalaumu sana, lakini mtajilaumu wenyewe kwa kuwa ujambazi unafanya binamu, mtoto wa mjomba, lakini mnawaficha, watoeni kabla operesheni hiyo haijaanza."
Rais Kikwete alisema tangu serikali yake iingie madarakani, hakuna jambo gumu lililowashinda na kwamba sasa watachukua hatua zinazotahili lakini serikali isije ikaluamiwa.
Alisema hivi sasa vumbi la majambazi limetulia, wakibuni mbinu mpya na kwamba, kabla hawajaibuka watateketezwa na salama yao ni kujisalimisha.
Akzungumzaia kuchelewa kukamila ujenzi wa wa barabara ya Kagoma-Lusahunga alisema watambana mkandarasi ili akamilishe kulingana na mkataba.
Alisema suala la ulinzi na usalama halina mjadala ni jukumu la serikali na aliwaahidi wananchi kuwa majambazi hawataachwa watambe.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, alimsifu Rais Kikwete kwa ujasiri wake wa kupambana na mafisadi wakubwa.
"Umeonyesha mfano, umeanza na mafisadi wakubwa wewe endelea, sisi tutawashughulikia hawa wa chini ili tukutane katikati, wewe endelea kaza uzi!" alisema Masilingi.
Masilingi alisema hawatakubali fedha za umma kufujwa na wachache na kuongeza kuwa watapambana nao, wakishindwa wataomba msaada ngazi za juu.
Akiwa wilaya ya Chato juzi, Rais Kikwete aliwashukuru wananchi kwa kumchagua John Magufuli ambaye alisema ni msaidizi wake muhimu kutokana na utendaji wake mzuri.