He need your urgent help please

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Dear members,
I need your advice on this matter, my girlfriend and I
went to have a court marriage few years ago without anybody knowing not even our parent's consent. The reason is I was planning to embark on a journey abroad so the fear of losing each other prompted us to do the secret court marriage but now we have given our lives to Jesus. We would like to know if having a divorce is SIN or NOT because our parents weren't aware and didnt give any blessing (s) on our marriage. Should we divorce? Do we have to tell our parents and apologise for what we have done?, please I need your help!
Source: Friend
 
Ukiona nakuwa harsh sana, ni kwa sababu ya tough love tu.Labda tukiku scold utafikiri mara mbili kabla ya kufanya maamuzi ya ajabu.

Wewe umempa yesu maisha yako halafu unakuja hapa kuomba ushauri? Unazo kweli wewe? Yaani hapa umepaona pana authority kuliko Yesu?

Sasa na sie tusioamini katika yesu wala dini si unatukwaza tu? Kwa nini usiende huko ulikompa Yesu maisha yako wakakupe ushauri zaidi?

Umempa Yesu maisha halafu unataka ku entertain sirisiri na uongo? Kwa nini msiende kwa wazazi na kuwatubia kwa upuuzi huu mlioufanya kama kweli mnawajali?

Mie naona unatuchanganya tu hapa, mara mmeoana kisiri ili msipotezane, mara mnataka kuachana, kinachowafanya mtake kuachana ni nini, huyo Yesu?

Yesu na wazazi wapi na wapi? Mbona mnataka kuchanganya mambo?

Kama umejishtukia umeboogie step sema tu, usitake kumvika Yesu issue isiyo yake.Kama unamuamini kweli Yesu utajua kuwa ndoa kwa misingi ya ki-Yesu ni sakramenti takatifu, na huwezi kutumia "kumpokea Yesu" kama sababu ya kuvunja ndoa, if anything, kumpokea yesu kunatakiwa kuwa ndiyo kigingi cha kuimarisha ndoa.

Usije hapa kutafuta vindication on your baseless premises for dismantling your marriage.

Umelikoroga sasa linywe, tena waoneni wazazi muwaombe msamaha kwa kufanya mambo kienyeji na muwaombe baraka zao.

Ndoa si kama kununua suruali, kwamba usipoipenda utairudisha dukani.Ndiyo maana wengine hatutaki kuoa, si wajinga sie.
 
Umelikoroga sasa linywe, tena waoneni wazazi muwaombe msamaha kwa kufanya mambo kienyeji na muwaombe baraka zao.

Ndoa si kama kununua suruali, kwamba usipoipenda utairudisha dukani. Ndiyo maana wengine hatutaki kuoa, si wajinga sie.

Huyu ni mpendwa kama wewe mambo
ndio hivyo yalitokea na aliona maisha bila Yesu ni kazi bure akaamua
kumpokea Yesu na kama unavyojua kwamba mwanaume Yesu akiingia ndani
basi atachokonoa kila kitu kilichojificha na kukuacha safi. Sasa ndio
hivyo kijana aliona kwamba ameshinda na sasa anahitaji msaada kwa
maana Yesu hataki mambo ya njia za panya. anataka kuweka mambo wazi.
Nafikiri sasa unaweza kutoa ushauri kama kumpa talaka mke wake,
kuendelea kuishi naye, kuomba msamaha kwa wazazi wake au la. With
reference from the Bible. Hope you will not let him down its serious!
 
Kafanya mafundisho ya ndoa na huyo huyo.Ukiona mafundisho yanakutaka muachane naye,ufanye hivyo.Lakini kabla ya kwenda kwenye mafundisho ombeni ridhaa ya wazazi.
MSISITIZO;Kama Yesu uliyempokea anasema kwamba ULIZINI na huyo mwanamke hivyo hamuwezi kuoana basi ujue huyo sio YESU wa UKWELI.
 
kwakuwa dhamira inayokusuta sasa ni kwa sababu umempokea Yesu, unaonaje ukienda kwa viongozi wa kiroho ukapata ushauri wa kiroho kwa jambo la kiroho?
ingawa pia mnaweza kwenda kuomba msamaha kwa wazazi kwanza kama lengo ni kutengeneza
 
Kwa kuwa kampokea Yesu nadhani itakuwa ni jambo la busara hii ishu akawashirikisha viongozi wake wa dini, atapata ushauri mzuri ambao pia utamjenga kiroho.
 
Jamani kuweni wastaarabu mnakuja na jazba badala ya kusema nini kifanyike mnashusha lugha maneno makalimakali hii haisaidii kamwe,
Mimi nadhani humu kuna watu wenye HEKIMA zao watamisaidieni mtapata solution kwa ajili ya hilo tatizo.
 
Jamani kuweni wastaarabu mnakuja na jazba badala ya kusema nini kifanyike mnashusha lugha maneno makalimakali hii haisaidii kamwe,
Mimi nadhani humu kuna watu wenye HEKIMA zao watamisaidieni mtapata solution kwa ajili ya hilo tatizo.

Can you be specific?
 
Can you be specific?
Kaka anajua kwamba kuna viongozi wake wa dini lakini bado ana wasiwasi
ndio maana anahitaji ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kama wewe.
Ingekuwa vizuri kama ungerejea hata katika Biblia kumpa imani zaidi.
Ingawa nao huo ni ushauri mzuri. Jaribu kumsaidia kama wewe ni kijana
ambaye unaijua Biblia. Yeye ni kama mtoto mchanga katika uokovu. Nafikiri umenielewa ikiwezekana waweza kufunga na kuutafuta uso wa Mungu kwa ajili ya swala hili.
 
Back
Top Bottom