HC DK. Jakaya Kikwete Usipowawajibisha Hawa Tutathibisha kwamba Uliwaagiza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HC DK. Jakaya Kikwete Usipowawajibisha Hawa Tutathibisha kwamba Uliwaagiza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Jan 8, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mauaji ya Kinyama yaliyotokea katika Jiji la Arusha hayawezi kupita bila Watu fulani kuwawajibisha Watu kadha wa kadha

  1: OCD wa Arusha: Huyu alipaswa kuwajibishwa Mapema kabisa kwani alihusika kwa Kiasi Kikubwa kuharibu Uchaguzi wa Meya Katika Jiji la Arusha na Kushirikiana na Vijana wake Kumpiga na mpaka Kuzirai Mbunge wa Arusha Bwana Godbless Lema

  2: RPC Andengenye huyu ndiye Imediate Boss wa OCD naye anapaswa Kuwajibishwa Mara kwa Damu za Watanzania wasio na Hatia waliokuwa wana exercise haki yao ya Kikatiba ya Kuandamana kwa Amani

  3: IGM Mwema Huyu ndiye Muuaji kabisa ambaye kama Haitoshi aliamua kulihamishia Jeshi la Polisi kutoka Pande zote za Nchi kwenda Kupambana na Wananchi wa Arusha, matokeo yake wameua Watu, wamejeruhi raia, wamedhalilisha Vongozi, wameharibu mali za Watu. Mwema Damu za Watanzania wa Arusha zi juu yako na Ili Wakusamehe ni Lazima Uombe Radhi na Ujiuzulu

  4: Waziri Nahodha ambaye Jeshi la Mauaji ( Maana limeshapoteza sifa ya kuwa Jeshi la Kulinda Raia) la Polisi liko katika Wizara yako unapaswa Kujiuzulu na Kufikihswa katika Vyombo vya Sheria kwa kuamuru Jeshi linalolopwa kwa Kodi za wananchi kuua Wananchi linaliposwa Kuwalinda

  Ndugu rais HC Dk Jakaya Kikwete, nakupa Benefit of Daught kwamba Hukuwatuma hao Wauajai niliowaorodhesha hapo Juu, kwamba wao kwa kukosa Busara na Ulevi wa Madaraka Uliyowatunuku waliamua Kushika Mtutu dhidi ya Raia wema waliokuwa wanaandama kwa Amani kuelekea kwenye mkutano, Kwamba Umeguswa na Damu za Watanzania wasio na Hatia walipouawa na OCD, Angengenye, Mwema na nahodha pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha

  Mh Rais HC Dk Jakaya Kiwete, hawa wote ni wateule wako, Ili kuonesha kwamba hukuwatuma kwenda Kufanya yale mauaji ninakupa Siku Saba uwe Umeshawawajibisha hawa watu La Sivyo nitauambia Ukoo wangu na wao wawaambie Rafiki na Ndugu zao kwamba Rais wao ni MUUAJI

  Poleni Sana wana Arusha Ila Damu ya Ndugu na Marafiki zetu haijamwagika Bure maana kama Arusha ndio Mama wa Azimio la Arusha basi kwa Damu yenu kokote Mliko Mmeifanya Arusha kuwa Kitovu cha Madadiliko na Kukataa Kila aina ya Udhalimu na Uonevu wa Watawala dhidi ya Watanzania
   
 2. m

  mikest Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  ninakubaliana na wewe 100%
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  I disagree,nafikiri na yeye atoke kama unataka uwajibikaji,whats the point of giving him benefit of doubt and not those who were more likely doing what they have bn ordered to do:A S-confused1:?Uwajibikaji ungeanza kwake aliye wateua wote hao na wanaofuata maamuzi yake,au unaona vile yeye yuko juu sana basi unaamua ku-deal na wateule wake??? He does not care if the whole of your clan call him muuaji,if he care less about you and many of us in the decision that he makes daily,do you think he will care if you call him muuaji? well,i respect your opinion.
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nimempa Siku Saba za Kuwawajibisha na Kuwapeleka katika Vyombo Vya Sheria asipofanya Hivyo siyo kama Nitamuita Muuaji bali atakuwa maeprove kwamba Yeye ndiye aliyemwagiza Mwema akawaue wale Waandamanaji
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Nadhani yeye awajibike kwanza ili mengine waone njia. Tangu oct.31 ngemuona wa busara kama angekubali kuishi mkoa wa pwani akipishana na chaguo la wanainchi. Chanzo cha matatizo,I think to cure a source than treating early outcome!
   
 6. B

  Babasean Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inasemekana Side na JK ni mtu ni shemeji yake! sasa je wanaweza kuwajibishana?
   
 7. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hatutacompromise haki za msingi za wananchi,ukiua kwa upanga utauwawa kwa upanga,ukiua kwa risasi utauwawa kwa risasi,nikiwa mmojawapo wa waandamanaji waliopigwa na kuuwawa na polisi au kwa maagizo ya juu ama vinginevyo,damu hii haitarudi bure lazima wapate kwa kipimo kile kile walichofanya,,ni mwanzo wa safari ndefu ya ukombozi wa kweli na hakuna wa kuzuia,or for bullet or for blood we must win
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Natumai Mh. Rais anasoma hapa, Haitoshi Kusikitika inabidi Watu hata ikiwezekana Yeye awajibike maana huwezi kuwafuta Machozi wahanga kwa kusema kwamba Umesikitika
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ukimya wako Umenifanya Niamini Damu za Wana Mapinduzi zinakusuta sana, Unaona hata Aibu Kulizungumzia hili Jambo, Najua Uliamua kuwaua Baada ya kukunyima Kura, sasa mheshimiwa Sijui utaua wangapi Katika Kipindi cha Safari ya Kuelekea Utumwani, Kama Hasira za Kunyimwa Kura zinakufanya Uagize vyombo vyako Viue wapinzani wako napata wasiwasi maana SIRI YA USHINDI WAKO UNAIJUA WEWE NA USAALAMA WA TAIFA NA WALIOKUNYIMA KURA UNAWATAMBUA VILEVILE
   
Loading...