Hazina yawachefua wafadhili

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Hii ni robo ya pili ya mwaka wa fedha 2013/14 hakuna fedha yoyote ya basket fund iliyofika katika halmashauri zote nchini,fedha hizi ni michango ya wafadhili kutoka mataifa mbalimbali ya ulaya na marekani.
Taarifa zilizopo ni kuwa fedha za mwaka wa fedha uliopita yaani 2012/13 hazikutumika zikaisha na sababu yaweza kuwa ni kama hihii ya ucheleweshaji wa fedha.

Matakwa ya wafadhili ni pamoja na kuitaka hazina ipeleke bakaa ya mwaka wa fedha uliopita,yaelekea hazina ilishatafuna hii bakaa hivyo hawana cha kupeleka.wazungu wamedinda na matokeo yake ni miradi na uendeshaji wa halmashauri kukwama hasa hasa katika sekta ya afya.

Wabunge na madiwani wa ccm ndio waathirika wakubwa katika hili na hivyo chadema kuendelea kupata turufu ya kupendwa na wananchi.

Leo hii wabunge wanabweka kuwa miradi haitekelezwi lakini hawajui chanzo ni madudu ya wizarani hasa hasa wizara ya Mgimwa aliyewasilisha bajeti kwa mbwembwe na madaha.

Kuna baadhi ya watu wanasema fedha hizi zinaandaliwa kuiokoa ccm kwa chaguzi za 2014/15.

Source:Ka-nzi kalichokuwa kwenye ukumbi wa majadiliano.
 
Ukweli ni kwamba, kwa mtindo wa serikali tuliyonayo hakuna haja ya kupewa misaada.
Bajeti inayopitishwa na Bunge huwa ni maelezo tu ambayo hayafuatwi hata siku moja. Kwangu mimi mwananchi sioni sababu yoyote ya kuomba au kupewa misaada. Naomba sana wakomae ili tujifunze kuendesha serikali na hasa kipindi hiki kifupi kabla ya 2015.

Rais Moi wa Kenya alipobanwa mbavu, alijifunzxa na leo hii Kenya inaendesha nchi kwa bajeti ya kodi zake. Pale Z'bar tulipobanwa kwa zile vurugu, adabu ilikuja na tukazitafuta pesa ktk kodi. Iweje leo tunaweka rais anayejivunia safari za kuomba misaada?

Eti safari Za Rais ni za manufaa. yapi?
 
Mkuu hata mimi nashangaa ni kivipi halmashauri zimeweza kuvumilia jambo hili.....misaada ni ya nini hasa?
Kinachoshangaza bado serikali inaendelea kulazimisha watu watengeneze bajeti kwa kutegemea hiyo misaada!sasa hivi halmashauri zinajiaandaa kuwasilisha bajeti dodoma.
 
Back
Top Bottom