Wanitakiani
JF-Expert Member
- Apr 18, 2008
- 641
- 135
Wacha wakatwe tu hizo ela zao. Wazee hawa hawa si ndo wanasema ccm imewalea, ccm inawafanya waishi kwa amani, afu kipindi cha uchaguzi si wanaipigia kura ccm, huku wakiwa na nyuso za furaha kwenye ma t-shit na makofia yao ya njano na kijani...
Baba mwanaasha endelea kuwapini mpaka wakome!
Jamani si wazee wote wanaoipigia chapuo CCM! Kuna wazee wamezinduka siku nyingi, kwa mfano baba yangu mie ni mstaafu na anapokea hizo laki 3 kila baada ya miezi 6! yaani kama sisi watoto wake hatumpi tafu mzee anaadhirika! Wazee wengi wastaafu ni wale ambao walikuwa waaminifu na watiifu kwa serikali yao, walilelewa chini ya Azimio la Arusha hivyo hata kuiba hawakujua! Hao ndio wanaopigika kwa sasa maana waliamini kwenye mshahara tu.
Kwa nini wasiwakate Wabunge??? kuwakata wazee hao dhambi hiyo itakuwa juu yao wao pamoja na vizazi vyao!