Hazina Haina Mpunga. Imefulia. Inapumulia Mashine

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Habari za chini ya kapeti zinaelezwa kuwa Ofisi ya Bwana Mkulo haina fedha. Imefulia na hali ya nchi kifedha ni tete.

Wakati huo wahisani hawana habari na wala hawataki kusikia nchi iliyotumia mamilioni ya pesa kutundika mabango ya kampeni ya JK, kuchakachua matokeo na upuuzi mwingine uliogharimu mabilioni ya pesa za kodi za wananchi eti leo inalia njaa.

Habari ndiyo hiyo.
 
Heshima ya nchi iliishia pale walipokimbiliaa kuingia ikulu....kuna nini pale ...?maana ni mzigo mkubwa sanaaa....ulee unakimbiliaa kuuza sura?/kuna nini????ona sasa nchi inavyokukimbizaaa.............ole wao watakaokimbiliaa ikulu...watatoka kwa aibu
 
Ni kweli mana hata ile mishahara waliyotangaza mafisadi mpaka leo imekua ndoto.
 
Habari za chini ya kapeti zinaelezwa kuwa Ofisi ya Bwana Mkulo haina fedha. Imefulia na hali ya nchi kifedha ni tete.

Wakati huo wahisani hawana habari na wala hawataki kusikia nchi iliyotumia mamilioni ya pesa kutundika mabango ya kampeni ya JK, kuchakachua matokeo na upuuzi mwingine uliogharimu mabilioni ya pesa za kodi za wananchi eti leo inalia njaa.

Habari ndiyo hiyo.
Source Please
 
Nasikia JWTZ huwa wakihitaji hela wanaenda TRA moja kwa moja kuzichukua, hawasubiri hazina wala wizarani!
 
Nasikia hali ilianza kuwa tete since august.other charges(OC) zilianza kutumiwa kwa fujo
 
Nyongeza ya salary za watumishi wa umma katika idara nyingi zilifanyika katika karatasi, lakini malipo bado. Kuna malimbikizo mengi tu since July, ila muungwana alichofanya ni kuwalipa cash watumishi walio katika majeshi na baadhi ya idara. Yote haya ni sababu fedha ilielekezwa katika 'mkopo' wa kununulia mabango!
 
WAna JF , kuna uvumi kuwa HAZINA IMEKAUKA, na BUDGET ZILIZOPITISHWA ZINATAKIWA KUKATWA KWA ASILIMIA NYINGI. Hizi taarifa zimezagaa kila kona nchini......Je, watoto wetu watasoma tena wakati tunalipa ada kwa installments? Je, familia zetu zitaendelea kuwepo?

tafadhali mwana jamii yeyote mwenye news atujuze.
 
Inawezekana maana kwenye ofisi nyingi za serikali hali ni mbaya!!
 
Ni kweli bajeti zimekatwa kwa aslimia 40. Lakini hakuna cha kushangaza kama rcs na dcs wanapewa handshake ya 40 million kila mmoja nje ya sheria ya mafao ya wastaafu unatarajia nini. Mwanzo cag alipinga hili lakini kanywea. Dhuluma kila mahali. Binafsi nimeanza ku question uthabiti wa utto.
 
Japokuwa sina data juu ya hilo lakini hali serikalini ni mbaya, labda ndiyo wanavuta pumzi ili DOWANS ilipwe au wafadhili ndiyo wamegoma. Tutakula nyasi mwaka huu, mvua zimechelewa.
 
Hata mimi nimezipata nyepesinyepesi kwamba serikalini watu wanahaha hakuna pesa kabisa, hata mishahara inalipwa kwa mbinde. Sasa nadhani watanzania watajua ghalama za kuvaa kofia na T-SHIRT wakati wa kampeni. :faint:
 
Yes, lisemwalo lipo, nimeenda kwene ofisi fulani wote wanalalama, yaaani ni kukavu ajabu! halmashauri moja imekopwa na serikali yake, yaani unaandikiwa kimeseji toa pesa ya kitu fulani halafu hazina itarudisha, kumbuka haya ni makusanyo ya kodi za mazao na biashara wilayani!
mahali pengine, wajina ya walimu waliopangiwa vituo wameshindwa kuripoti, hakuna pesa japo wametoa majina hayo ili kupunguza kashfa iliyoanza kuibuka kuwa wameshindwa kaujiri!!! pumbaf kabsaa
 
Kwani ile Bajeti iliyogomewa na Wahisani (DPS) ilishasainiwa? Sijawahi kusikia japo wafadhili hao walisema watatoa msimamo baada ya wiki chache. Mwenye taarifa naomba anijuze.
 
Haya mnaolipwa na serikali mbona mko kimya? si ndio tarehe zenyewe hizi? tujuzeni tujue jinsi ya kujibana ili tugawane tulichonacho
 
Back
Top Bottom