Hayati Mwl Nyerere: Chama Cha Mapinduzi kina kansa ya uongozi ambayo isipotibiwa itakiua Chama kizima

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
2,262
1,901
"Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi hakiwezi kuepuka​
lawama. Lakini kuilaumu Kamati Kuu ni kukiri kwamba sasa Chama Cha Mapinduzi kina
kansa ya uongozi ambayo isipotibiwa itakiua Chama kizima. Pengine kwa nchi yetu hii​
lisingekuwa jambo la kutisha kama tungekuwa tumeanza kuona chama kizuri cha upinzani​
ambacho kinaweza kuiongoza nchi hii badaIa ya CCM. Hakijaonekana bado. Chama Cha​
Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake,​
mazoea ya watu, na ubovu wa vyama vya upinzani, kinaweza kuendelea kuchaguliwa na​
Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza. wakachoka, wakasema,​
"potelea mbali:" wakachagua Chama chochote, ili mradi tu watokane na kansa ya uongozi​
wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa nchi yetu unataka yasemwe"-Hayati Mwl Nyerere​

"Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni​
jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza​
kuiongoa nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya
nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama​
kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho​
kingekilazimisha Chama Cha Mapmduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila​
kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao"-Hayati Mwl Nyerere​

Maneno hayo hapo juu yanapatikana katika ukurasa wa 42 na ule wa 45 katika kitabu cha Mwl kiitwacho UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA alichokiandika mwaka1994 lakini baada ya kukipeleka kwa wachapishaji (Mkuki na Nyota), Serikali ilikataa kisichapishwe ikabidi Mwl akakichapishe Zimbabwe. Alipokileta nchini ili kukisambaza Seriakali ikakipiga 'ban'; ingawa wapo wajanja wachache waliopata nakala ya Kitabu hicho.​

Mwl alipofariki mwaka 1999, mwaka 2010 Serikali ikatengeneza CHAPISHO LA KIZAZI KIPYA kwa kuyaondoa maneno yote ambayo yalionekana ni sumu kwa CCM. Sitakuwa na maneno mengi, nitakachofanya ni kuwapa nukuu tu ili mjue yanayotokea sasa yalitabiriwa na Mwl takribani miaka 18 iliyopita.​
Katika ukurasa huo wa 45 mpaka ukurasa wa 46 Mwl anaendelea kusema....​
"Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalili zozote za kuondoa kansa ya​
uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama​
Cha Mapinduzi, Chama hili kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu​
ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasi wasi!​
Wazalendo Watanzania hawana budi wapende kuona demokrasia halisi ndani ya Chama Cha​
Mapinduzi: Hii ina sura mbili".​

"Kwanza, ni lazima kurudisha tena uhuru na utaratibu wa kujadili masuaIa yote makubwa na​
kufikia uamuzi baada ya mjadala.​
Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kutoa maamuzi muhimu. Kwa​
sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja; vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha​
ya kutumia akili na kupata hoja safi ya kumjibu mpinzani katika mjadala. Viongozi hawa​
wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; na hawatakuwa na haja ya kutumia akili.​
Kichini chini baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho. Na kama tukiacha​
utamaduni wa woga ukazagaa tutakuwa tunakaribisha udikteta".​

"........ Washindania urais wapo, tena moto moto. Chama kinajua​
hivyo, na wananchi wanajua hivyo. Chama Cha Mapinduzi hakina budi kitafute utaratibu​
mzuri wa kuwashindanisha wataka urais hawa kwa njia ya wazi wazi. Tutafanya makosa​
makubwa tukikubali kuteua mgombea urais kwa kutumia mzengwe. Njia ya mzengwe​
ilitufaa tu wakati tulipokuwa hatuna washabiki wa urais. Na inaweza kufaa kama mnataka​
kumteua mwenzenu ambaye mnaamini kuwa ndiye anayefaa, lakini hapendi misukosuko ya​
kushindania uongozi".​

Hivi Mwl Nyerere ni mzimu unaoishi? Nimebahatika kupata nakala ya hiki kitabu. Ukikisoma chote hutashangaa yanayotukia sasa.​
Mungu Ibariki Tanzania.​
 
Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
1,063
2,799
Kwa kweli. Kungekuwa kuna chama imara cha upinzani ningekipigia kura fasta sana 2005 badala ya Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete ambaye mpaka leo hii bado anatusumbua na ndio kansa kuu.
 
Deeboyfrexh

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
2,944
4,497
Hiko chama pinzani hakiwezi kusimama kwa namna yeyote ile kama Tume ya uchaguzi ni ya CCM, Polisi ni wa CCM na hata Mahakama ni ya CCM! Kinachotokea ni kujikomba komba kwa wapinzani ili wapate ulaji CCM kitu ambacho kinaondoa kabisa dhana ya upinzani

Suluhu: Katiba itakayoondoa ties zote za kichama kufungamana na mihimili ya serikali kwanza.
 
Ujima

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,087
1,533
Kwa kweli. Kungekuwa kuna chama imara cha upinzani ningekipigia kura fasta sana 2005 badala ya Jakaya Mrisho Khalfani Kikwete ambaye mpaka leo hii bado anatusumbua na ndio kansa kuu.
Kikwete ni kansa kumzidi nyerere?
 
Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
2,262
1,901
Hiko chama pinzani hakiwezi kusimama kwa namna yeyote ile kama Tume ya uchaguzi ni ya CCM, Polisi ni wa CCM na hata Mahakama ni ya CCM! Kinachotokea ni kujikomba komba kwa wapinzani ili wapate ulaji CCM kitu ambacho kinaondoa kabisa dhana ya upinzani

Suluhu: Katiba itakayoondoa ties zote za kichama kufungamana na mihimili ya serikali kwanza.
Uko sahihi kwasababu ukisoma kitabu chote moja ya hoja kuu ni Katiba mkuu.
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
12,064
6,190
"Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi hakiwezi kuepuka​
lawama. Lakini kuilaumu Kamati Kuu ni kukiri kwamba sasa Chama Cha Mapinduzi kina
kansa ya uongozi ambayo isipotibiwa itakiua Chama kizima. Pengine kwa nchi yetu hii​
lisingekuwa jambo la kutisha kama tungekuwa tumeanza kuona chama kizuri cha upinzani​
ambacho kinaweza kuiongoza nchi hii badaIa ya CCM. Hakijaonekana bado. Chama Cha​
Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake,​
mazoea ya watu, na ubovu wa vyama vya upinzani, kinaweza kuendelea kuchaguliwa na​
Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza. wakachoka, wakasema,​
"potelea mbali:" wakachagua Chama chochote, ili mradi tu watokane na kansa ya uongozi​
wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa nchi yetu unataka yasemwe"-Hayati Mwl Nyerere​

"Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni​
jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza​
kuiongoa nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya
nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama​
kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho​
kingekilazimisha Chama Cha Mapmduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila​
kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao"-Hayati Mwl Nyerere​

Maneno hayo hapo juu yanapatikana katika ukurasa wa 42 na ule wa 45 katika kitabu cha Mwl kiitwacho UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA alichokiandika mwaka1994 lakini baada ya kukipeleka kwa wachapishaji (Mkuki na Nyota), Serikali ilikataa kisichapishwe ikabidi Mwl akakichapishe Zimbabwe. Alipokileta nchini ili kukisambaza Seriakali ikakipiga 'ban'; ingawa wapo wajanja wachache waliopata nakala ya Kitabu hicho.​

Mwl alipofariki mwaka 1999, mwaka 2010 Serikali ikatengeneza CHAPISHO LA KIZAZI KIPYA kwa kuyaondoa maneno yote ambayo yalionekana ni sumu kwa CCM. Sitakuwa na maneno mengi, nitakachofanya ni kuwapa nukuu tu ili mjue yanayotokea sasa yalitabiriwa na Mwl takribani miaka 18 iliyopita.​
Katika ukurasa huo wa 45 mpaka ukurasa wa 46 Mwl anaendelea kusema....​
"Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalili zozote za kuondoa kansa ya​
uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama​
Cha Mapinduzi, Chama hili kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu​
ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasi wasi!​
Wazalendo Watanzania hawana budi wapende kuona demokrasia halisi ndani ya Chama Cha​
Mapinduzi: Hii ina sura mbili".​

"Kwanza, ni lazima kurudisha tena uhuru na utaratibu wa kujadili masuaIa yote makubwa na​
kufikia uamuzi baada ya mjadala.​
Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kutoa maamuzi muhimu. Kwa​
sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja; vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha​
ya kutumia akili na kupata hoja safi ya kumjibu mpinzani katika mjadala. Viongozi hawa​
wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; na hawatakuwa na haja ya kutumia akili.​
Kichini chini baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho. Na kama tukiacha​
utamaduni wa woga ukazagaa tutakuwa tunakaribisha udikteta".​

"........ Washindania urais wapo, tena moto moto. Chama kinajua​
hivyo, na wananchi wanajua hivyo. Chama Cha Mapinduzi hakina budi kitafute utaratibu​
mzuri wa kuwashindanisha wataka urais hawa kwa njia ya wazi wazi. Tutafanya makosa​
makubwa tukikubali kuteua mgombea urais kwa kutumia mzengwe. Njia ya mzengwe​
ilitufaa tu wakati tulipokuwa hatuna washabiki wa urais. Na inaweza kufaa kama mnataka​
kumteua mwenzenu ambaye mnaamini kuwa ndiye anayefaa, lakini hapendi misukosuko ya​
kushindania uongozi".​

Hivi Mwl Nyerere ni mzimu unaoishi? Nimebahatika kupata nakala ya hiki kitabu. Ukikisoma chote hutashangaa yanayotukia sasa.​
Mungu Ibariki Tanzania.​
AMEN, AMEN.
 
Ujima

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,087
1,533
Udhaifu wa chama hiki pendwa ulishaonekana tangu kipindi waasisi wake wakiwa hai na wakatoa maonyo yao ingawa walizibwa midomo au kupuuzwa.
Yeye alishindwa nini kutengeneza chama imara wakati yupo madarakani?
 
NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
5,103
8,969
Mwaka 2025 chama Cha umoja party kitatwaa madaraka kwa msaada wa the state!! mama atashupaza shingo na kuchukua fomu lakini kina Majaliwa na Bashiru wataenda kuimarisha chama hiki na kuchukua dola!!
 
ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
12,064
6,190
Hoja yangu ni kwamba huyo mwalimu anasoma hili andiko? Yeye kwanza ndiyo ameharibu chama chetu Cha mapinduzi
Mwalimu alipoondoka alikuachieni chama imara kilichojitambua na kuthamini nguvu ya hoja, ndio maana hakuogopa mijadala wala ujio wa upinzani. Lakini kutokana na kuutupa uadilifu, MLIOBAKI mnazidi kuogopa mno mawazo na hoja kinzani kila uchao. Mwendo wenu ni wa hoja za nguvu ndio unazidi kuwamaliza.
Kwa HULKA YAKE, hakuna binadamu yoyote anaethamini uonezi kwa wengine, wala yeye binafsi kukandamizwa. Lakini unapoona kuna watu wanamshangilia DHALIMU basi huo ni ugonjwa unaotokana na uoga/ujinga wa kupandikizwa na pia unafiki unaokuja kwa sababu ya njaa zinazoendekezwa.
Ninyi mngekuwa wakweli ndani ya nafsi zenu, juhudi zenu za kujijenga upya na kuimarisha uadilifu HASA ndani ya chama chenu, zingeonekana, na SIO kuongezeka kwa matumizi ya WAZI ya maguvu ya dola, badala ya kukua kwa uhuru, haki na demokrasia. AMEN
 
Ujima

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,087
1,533
Nipishe hapa takataka wewe. Ulitaka baba yako ndio awe raisi wa kwanza? Au wewe ni Kikwete uliyefurahia Nyerere kufa kwasababu angekuwa hai uraisi ungeonea kwenye kideo. Useless maggot.
Eeeeh! Makasiriko ya nini **** we
 
Fursakibao

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
4,802
6,683
Hiko chama pinzani hakiwezi kusimama kwa namna yeyote ile kama Tume ya uchaguzi ni ya CCM, Polisi ni wa CCM na hata Mahakama ni ya CCM! Kinachotokea ni kujikomba komba kwa wapinzani ili wapate ulaji CCM kitu ambacho kinaondoa kabisa dhana ya upinzani

Suluhu: Katiba itakayoondoa ties zote za kichama kufungamana na mihimili ya serikali kwanza.
Hapa ndipo watanzania inatakiwa tuseme basi tuingie barabarani bila chama cha upinzani kutushawishi.

Ila naona tunaelekea huko soon
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom