Hayati Mwalimu Nyerere aliyefanya mambo ambayo hatimaye yamesababisha CCM iendelee kubaki madarakani

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,203
4,677
Hayati Mwalimu Nyerere aliyefanya mambo ambayo hatimaye yamesababisha CCM iendelee kubaki madarakani. Yeye ndiye mpishi wa mambo mengine ambayo yamekifanya chama hicho kiwe hapo kilipo sasa.

•Jeshi Imara la Kizalendo
Wakati mara rafiki zake, Milton Obote wa Uganda na Kwame Nkrumah wa Ghana wakiondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi, Nyerere alinusurika na tukio la Maasi ya Jeshi ya mwaka 1964. Alichofanya Nyerere ni kulivunja jeshi lililokuwapo ambalo alilirithi kutoka kwa wakoloni na kutengeneza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Jeshi hilo lilitengenezwa na kufumwa katika itikadi ya ukombozi, ujamaa na lisilo na ukabila, udini huku askari wakipandishwa vyeo kutokana na umahiri wao na si kwa vigezo vingine. Matokeo yake, jeshi hilo la kizalendo halikumsumbua tena kama ambavyo wenzake wengi barani Afrika.

• Lugha ya Kiswahili

Ni Nyerere ndiye aliyepandisha hadhi lugha ya Kiswahili ambayo iliwaunganisha Watanzania na kuwa lugha ya kisiasa. Kwa sababu hiyo, CCM kikaweza kuwa chama kilichoweza kufika nchi nzima kwa viongozi wake kuzungumza lugha moja inayoeleweka kwa wananchi. Ziko nchi ambazo hata mawasiliano ya vitu vidogo ni ya taabu kwa sababu watu ndani ya serikali, majeshi na kwenye vyama hawazungumzi lugha moja na wakaelewana.

• Kuheshimika na Wananchi
Nyerere hakuwa malaika lakini mtindo wake wa uongozi ulimfanya aheshimiwe na wengi wa Watanzania. Baba huyu wa Taifa hakuwa fisadi, alikuwa mzungumzaji mzuri kwenye majukwaa na kupitia maandishi yake na hakuonekana kuwa na upendeleo wa wazi wazi kwa watu wa dini, kabila au eneo alilotoka.

• Mfumo Imara wa Uongozi wa Juu
Mwalimu Nyerere pia ndiye aliyesimika mfumo wa utawala wa Tanzania ambapo Rais anakuwa ni Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. Haya ni mamlaka makubwa sana kupewa mtu mmoja. Mfumo huu unampa Rais - kiongozi wa chama tawala; CCM tangu Uhuru, madaraka makubwa ya uteuzi wa viongozi wa vyombo vya serikali na dola na chama hicho kimekuwa kikitumia faida hiyo ipasavyo nyakati za uchaguzi.

•Kubadilisha Marais
Ukiondoa Nyerere, hakuna Rais mwingine wa Tanzania ambaye ametawala kwa zaidi ya miaka kumi. CCM imekuwa na utaratibu wa kuheshimu Katiba ambapo Rais aliye madarakani atatawala kwa miaka kumi tu na kumwachia mwingine.

Kwa kuhakikisha wateule wake wanakaa madarakani miaka kumi tu, CCM imehakikisha Watanzania wamekuwa hawachoki kwa kuona sura moja tu kwa miaka zaidi ya kumi. Mara nyingi, mgombea anayechukua nafasi ya aliyetangulia anakuwa na sifa na haiba tofauti na mtangulizi wake.

Nyerere alikuwa mwanafalsafa, mhafidhina na mcheshi, mbadala wake Ali Hassan Mwinyi akawa mtu rahimu, muungwana na mpenda mabadiliko, Mkapa akawa makini na mshaufu huku Jakaya Kikwete akiwa tena mcheshi, mtu wa watu na muungwana wa pwani. Baada ya miaka yake kumi, John Magufuli amechukua nafasi yake naye ni tofauti na mtangulizi wake kwa haiba na utendaji kazi.

•Mgawanyo wa Keki ya Taifa
Namna pekee ya kuelewa hili ni kuangalia nchi jirani ya Kenya.

Wakati nayo ikielekea kutimiza miaka 60 ya Uhuru wake mwaka 2023, imefanikiwa kuwa na marais wanne; Jomo Kenyatta, Daniel Arap Moi, Mwai Kibaki na Uhuru Kenyatta. Hiyo maana yake ni kuwa Wakikuyu wametoa marais watatu miongoni mwa marais wanne waliowahi kutawala nchi hiyo.

Ni Moi pekee ambaye hakuwa Mkikuyu -akitoka katika kabila la Wakalenjini.

Jambo hili limekuwa likizua hali ya sintofahamu na kuhisi kutengwa kwenye mgawo wa keki ya taifa miongoni mwa makabila mengine makubwa nchini humo kama vile Wajaluo, Waluhya, Wakalenjini na watu wa makabila ya pwani ya Kenya.

Hali ni tofauti kwa Tanzania. Nyerere alikuwa Mzanaki kutoka Kaskazini mwa Tanzania, Mwinyi anatoka Zanzibar, Mkapa anatoka Kusini, Kikwete akatoka Pwani na Magufuli anatoka Kanda ya Ziwa.

Marais wote wa Tanzania wametoka katika makabila tofauti miongoni mwa zaidi ya 120 yaliyopo.

Hii maana yake ni kuwa hakuna upande au kabila la Tanzania linaloweza kusema limeongoza kwa kutoa marais wengi. Kitendo cha kuwa na Rais madarakani humaanisha kwamba watu wa eneo analotoka Rais huweza kufaidika kwa namna moja au nyingine na uwepo wa kiongozi miongoni mwao. Inaweza isiwe waziwazi lakini pasi na shaka, kuna kipande cha keki ya taifa kitamegwa kwa kuzingatia ukweli wa Rais kutoka katika eneo fulani.
 
Wewe na ulichoandika ni ovyo kabisa.
Kinaaminika na wewe na siyo wote na ndio maana kuna vyama 19 nchi hii. hii inaonyesha kutoaminika
 
Back
Top Bottom