Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa anawalenga kina nani kwenye hii speech yake?

Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
17,176
46,193
Wakuu heshima kwenu.

Nilikuwa Youtube nacheki baadhi ya hotuba za Mwalimu Nyerere nikakutana na hii ambayo alikuwa anatoa maneno makali kuhusu Viongozi au Wanasiasa "Malaya Malaya"..

Pia akaongezea kuwa JWTZ ni jeshi ya Wananchi na sio jeshi la vibaraka..Pia akang'aka kuwatafuta mmoja baada ya mwingine i.e hao "Malaya Malaya"..akimaanisha kuwa wananunulika kwa fedha.

Naomba kuuliza wakuu,Mwalimu alikuwa anawalenga kina nani?..na kilitokea kitu gani hadi kumfanya mwalimu awatafute mmoja baada ya mwingine hao "Malaya Malaya"??

Historian itamlenga kambona. Ila kama una maana ya hivi Sasa kwa kweli sihusiki.... Sijasema maneno hayo mm wala siungi mkono hoja
 
Boys to Men,Kikwete na Lowassa.Kikwete alikuwa anafatilia hela kwa Lowassa.
Kikwete si wanasema alikuwa kijana pendwa wa Mwalimu..na kama angekuwa ni yeye anayesemwa hivi sidhani kama angepata hata Urais,maana angemalizwa kisiasa mapema tu
 
Okay Okay..So basically Mwalimu alikasirishwa na kukubalika kwa Kambona?..hakuna jingine mkuu?
Kambona alim-mix mzee wetu vibaya mno kipindi jeshi lenyewe ulikua huwambii kitu kuhusu kambona waliaza kumwiga Hadi kunyoa upigaji pasi nguo ,mzeee akaona asinitanie kambona akakaliwa kooooni namzee mpaka Leo amebakia kwenye maandishi na fikra zake lakini fikra zakambona enzihizo Leo ndo zinatutesa miaka 60 bado mawaziri wanaongea uongo mfululizo
 
Kumbe kambona ndo aliyemtoa Mwalimu lile povu lote..okay mkuu,shukrani kwa kuelezea hili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom