voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,552
- 11,883
Wananchi Wako njia Panda, wengi hawaamini wala kuelewa kinachotokea mbele ya Macho yao.
Wengi wamebaki kama mayatima wasio na mtu wa kuwasemea tena.
Sasa wanabaki kushuhudia sherehe za kujipongeza kila uchao toka kundi la walamba Asali na Maswahiba wao wa Upinzani.
Kwa kile ambacho kilitokea na bado kina mlolongo wa mashaka,mpaka hapo itakapokuja kutokea kiongozi wa kukubali tuhoji. Kwamba ni nini kilitokea.
Kama imewezekana Burkinafaso nina imani hata Tanzania iko siku inakuja na kitajulikana tu.
Eti chama kile kile kilichookolewa na Magufuli ,wakati maji yalipokifika shingoni kabla ya 2015.
Sasa hivi ndio kinaongoza kumchafua kwa kauli nyingi toka kundi linalojiita "wenye chama" na Wapinzani waliokosa sera na mipango mbadala ya kupambana na CCM ili hatimae kushika Dola.
Na Wapinzani badala ya kuongelea madhira rasmi yanayowakumba wananchi huko mitaani na vijijini na jinsi ya kuweza kuibana serikali iliyoko madarakani ili kuzitatua kero hizo.
Wao wameungana na CCM-asali kupigana na kivuli cha Marehemu Magufuli.
Na hawa CCM-asali Wamesahau kwamba kabla ya 2015,wana CCM walifikia mahali wakizomewa mitaani pale walipoonekana na Sare zao za CCM.
Na wao ndio walikuwa viongozi wakati huo.
Wamesahau kwamba Magufuli alitumika kama "Survival Gear" ya kuiokoa CCM ile iliyokuwa inachungulia kaburini.
Lakini jambo moja wasilolielewa hawa walamba asali kwa sasa. Ni kwamba wanapambana na mtu ambaye hayupo tena Duniani.
Wanapambana na mtu ambae yuko ndani ya "MIOYO" ya wananchi waliomkubali kwa kazi yake ya muda mfupi.Iliyowafungua macho wananchi juu ya uwepo wa maliasili za nchi hii na jinsi ya kuzitumia.
Ukimya wa wananchi sio ushindi kwa CCM-Asali na Upinzani ulionzisha ubia kama ilivyokuwa kabla ya 2015.
Bali ni ukimya uliojaa taharuki na Hasira za kimyakimya kwa wote wanaoendekeza kejeli dhidi ya mpendwa wao Magufuli.
Na kinachotokea ni kwamba ukimya huu wa wananchi sasa unaanza kuhamia hadi kwa viongozi waandamizi ndani ya serikali.
Ndio maana tunaanza kuzisikia kauli za "kuwalazimisha Kumsemea Samia"
Zikitolewa na viongozi waandamizi ndani ya CCM.
Ndio maana tunaiona CCM ikiingiwa na hofu na kulazimika kuanza "kampeni kabla ya wakati"
Napenda kuwaambia kwamba vema wakatunza maneno yao.
Kitendo cha viongozi wa CCM na taasisi zake kukaa kimya,bila kuwakemea wanachama wao, ambao wameibuka kwa wingi hivi sasa huku wakijitahidi kumchafua Magufuli.
Ni kitendo ambacho kitawagharimu sana kwenye uchaguzi ujao 2025.
Inaweza isimtingishe Samia ndio.
Lakini wabunge wengi wakae bungeni huku wakijua wako mle wakiwa njiani kurudi Benchi mtaani.
Wanaopambana na Magufuli wako Majukwaani na Mitandaoni.
Lakini magufuli yuko mioyoni mwa wananchi,kuanzia wamachinga,wakulima,wanafunzi vyuo vikuu na kwingineko.
Kila anaejitahidi kumchafua badala yake anachafuka yeye.
Kimya kingi kina mshindo.
Sasa hata Twiga wameruhusiwa kuanza kuuzwa tena.
Sasa tunaona watu walewale wakirudi kila uchao.
Tena kwa Kasi na Ari Mpya.
commonmwananchi
100101.
View attachment 2250953