Hayati Magufuli: Viongozi wastaafu waachwe wapumzike

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
7,564
11,478
Kwa wanaokumbuka hii habari ya watesi wa Kikwete ndio ilipelekea Magu ang'ake na kutaka wastaafu waachwe wapumzike.

Ilikuwa katika kongamano moja ambapo Jenerali Ulimwengu alitoa kauli ya kutaka Kikwete ashitakiwe kwa kutumia pesa za walipa kodi kwenye mchakato wa katiba bila katiba kukamilika.

Ni muda mchache baada ya Kikwete kutoka madarakani.

Tunakumbuka Kikwete alipoingia aliacha Mkapa achafuliwe mno bila kutoa tamko lolote. Ilifikia Mkapa aliitwa mahakamani kutoa ushahidi wa kesi ya balozi. Na pia aliwahi kupigwa mawe kule masaki na vijana wa kijiweni tu.

Kwa sasa Samia nae anasimamia kwa umahiri uchafuzi wa Magu akiamini umaarufu wa Magu utaamia kwake.

Lakini kama ambavyo Kikwete alishtuka dakika za mwisho ndivyo vivyo mwanafunzi wake samia pia atashtuka kukiwa kumekucha.

images (10).jpg
 
Mimi kwa hili la Magufuli kuchafuliwa mitandaoni namlaumu Rais moja kwa moja kwa kua anaona na hachukui hatua yeyote.
 
Mimi kwa hili la Magufuli kuchafuliwa mitandaoni namlaumu Rais moja kwa moja kwa kua anaona na hachukui hatua yeyote.
Kwa sasa anaamini itamfanya awe maarufu. Hata JK aliamini kuchafuliwa kwa Mkapa kungempa yeye umaarufu. Ila alikuja kunuka hadi chama kikamfia mikononi. Anakuja kuwaangukia kina mkapa wamuokoe ila ikawa too late.
 
Na aliposema wastaafu wanawashwawashwa?

Au huyo hakuwa magu?
Ni kweli walianza kuwashwa! Kwa sababu zamu yao ilikuwa umekwisha, kuanza kulialia na kuonyesha umwamba wakati mambo mengi tu yaliwashinda! Huko ni kuwashwa
 
Na aliposema wastaafu wanawashwawashwa?

Au huyo hakuwa magu?
Aliwapumzisha ili wasipigwe mawe. Wakawa wanajifanya wanajitokeza tokeza. Akawaacha kina Ally Happi washughulike nao maana ye alishasema wasibughudhiwe na watulie. Ila baadhi wakawa wanawashwawashwa.
 
Back
Top Bottom