Hayati Magufuli ni Nabii wa Afrika aliyechelewa kueleweka katika ukombozi wa pili wa Mwafrika, hakuogopa vigingi vya Mabeberu

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
1,079
2,000
Moja kati ya alama aliotuachia baba yetu Magufuli ni demokrasia ya kipekee tunayoweza kuiita demokrasia ya kiafrica.

Tumeona nchi ikipiga hatua sana chini ya utawala wake. Demokrasia ya kiafrica inalenga zaidi haki za kiuchumi kwa wafanyabiashara wadogo kufanya biashara bila kubughudhiwa. mfano machinga kupewa uhuru wa kujitafutia riziki.

Tumeona wananchi wanapata haki ya huduma za kijamii kupata elimu bure, wanajengewa zahanati, barabara na madaraja kila kona ya nchi, umeme vijijini nk.

Demokrasia ya kiafrika Serikali haichezewi na watu wanaheshimu mali ya umma.

Tofauti ya demokrasia ya kiafrika inakuwa na mipaka ndio maana uchaguzi ukiisha tunarudi kuijenga nchi sio kuanza kuandamana kuzua taaruki kuchafuana ili serikali isifanye kazi yake.

Pia tunaheshimu mila na desturi zetu ndio maana Lissu alipotaka kuleta ushoga watanzania wakamkataa.

Tumuenzi mzee wetu Magufuli kwa kuiishi misingi ya demokrasia ya kiafrica ambayo imempa heshima kwa wananchi wake na kwa dunia.

Tuache kuiga kila kitu cha Ulaya na marekani ndio maana haya mambo ya demokrasia huwezi yaona China, Dubai, Abu Dhabi nk na wanamaendeleo makubwa.

Someni history nchi zote zenye maendeleo demokrasia imekuja baadaye sana hiyo Marekani imejengwa na watumwa na black wameanza kupiga kura juzi tu.
 

mbalaka

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
2,116
2,000
Tanzania inaongoza kidunia kuwa na weu wapya kila uchao..
sijui kwa hali hii tz ya viwanda mtaifikia vipi,ama Mareham amekwenda na ndoto yake?.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,872
2,000
Watanzania wanapenda sana matukio, kukitokea ajali wanajazana washuhudie seuse leo jeneza la Magufuli, wataenda kushuhudia ili wahadithie.
 

julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
1,185
2,000
na siasa aliamin haitajenga mabarabara.ndio mana uchaguz umeisha sasa tuijenge nchi yetu.siku zot siasa inatuchelewesha.wanannchi waliamua tar 28 oct kwenda na hapa kaz tu.kwa kuitambua ilan makin ambayo utekelzaj walke ukikamilika utaipaisha nchi kufikia uchumi wa juu.
nashauri zigawiwe kwa kila mwanamchi awe anaisoma na kuona mahali pake pamefikiwa
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,560
2,000
Mungu mkubwa sana , yaani mtu kaiba uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi mkuu , kwa nguvu kubwa ssna , kapanga kuongeza miaka miezi mitano baada ya uchaguzi kafa aiseee .
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,030
2,000
Mungu mkubwa sana , yaani mtu kaiba uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi mkuu , kwa nguvu kubwa ssna , kapanga kuongeza miaka miezi mitano baada ya uchaguzi kafa aiseee .
Wewe una roho ya karai, kalai haichagui Zuri Wala baya yote inabeba Tu. Nabii Magufuri Ni mbena maono ambaye Mungu amemwitaji haraka
 

kiboboso

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
7,674
2,000
Usijifanye kunguru mwoga, kwani kabla ya wazungu hakuna nchi ambazo zilikuwa Na maendeleo ya watu Na vitu. Mali, misdi Na nyingine nyingi kabla ya Mabeberu zilikuwa vizuri. Sasa wewe ushatskwa Na wazungu uwezi kutoka Korea ya Kaskazini inaendeshwa Na Mabeberu? Mungu mnasomea nini kama vyuo vipo lakini uwezi hata kutengeneza wemb Na sindano mpaka uagize. Nabii Magufuri Alianza ndogo ndogo kuondoa haya.
Kwa hii comment yako nimegundua unamatatizo ya akili.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,420
2,000
Nabii Eliya aliua waliokuwa wanaabudu mungu wao Baali soma

1 Wafalme 18:21-40​

Eliya aliuwa hao manabii wa baali, siyo kwa kuwa alikuwa katili. Soma vizuri utaona sababu. Soma ule mstari wa 36 taratibu utaona kama kweli Eliya alikuwa katili au alitekeleza maagizo ya Mungu.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
13,453
2,000
Ndio maana katiba mpya ni muhimu ile kudhibiti hayo "mapungufu ya kibinadamu" katika nafasi nyeti kama ya Urais.
Mugabe kitu alifanikiwa ni kuwanyang'anya weupe ardhi. Alipambana ipasavyo na kila aliyeonekana kuhatarisha nafasi yake ( kiti chake). Wasomi wengi waliikimbia nchi na kuishi maisha magumu sana. Kwa Wazimbabwe huyu jamaa hakua shujaa kama wengi tunavyomchukulia huku nje

Kuhusu JPM siwezi kumuita nabii lakini alikua mwenye uthubutu, aliyependa matokeo, alisimamia maamuzi yake na aliamini vitu vinaweza kufanyika.

Alikua na mapungufu yake kama tulivyobinadam wengine.

Kazi ameimaliza, amefunga kurasa za kitabu chake.
 

ORCA ACE

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
975
1,000
Dini nyingine zinamkera Mungu, uyu uyu awarake DC wa kisarawe??
Wana Jf

Nianze Kwa kumtanguliza Mungu kama Nabii Dr. Magufuri alivyopendelea kumtanguliza Mungu kila wakati.

Ninaposema Dr. Magufuri ni Nabii wa Africa aliyetumwa kuikomboa Africa mara ya pili ninamaanisha kuwa Kwa Yale mahubiri yake ya kutaka Africa tujitathimini kupenda vyetu ili kujinasua mikononi mwa Mabeberu. Unyonyaji unaofanyika nchi nyingi Ni kutokana Na watu kukosa uzalendo Na kukumbatia njia zote za kinyonyaji kupitia mikataba feki.

Mabeberu waliiteka Africa Kwa njia zote za kiuchumi, kupitia mawakala wao kama WHO, WB, UN, IMF Na nyingine nyingi. Kwa kulitambua Hilo Magufuri pamoja Na uwezo ndogo kufuatana Na anaopambana nao aliweza kuanza kufumua mikataba ya kinyonyaji. Pengine Unaweza kusema Kwa nini hakupenda democrasia iliyozidi kipimo jibu Ni kwamba mpaka Sasa hakuna democrasia ya Kweli tunayoaminishwa. Tumejionea marumbano Na watu kupoteza Maisha katika uchaguzi wa USA.

Ambayo duniani tunaiona kama kiranja mstaarabu anayejua democrasia Na kuitumia vilivyo. Kwenye kudhamilia kitu cha kuleta maendeleo hakuna democrasia, ukiacha uende Na democrasia vitu vingi vitakwama kwenye utekelezaji. Tuliona miradi mingi iliyoandikwa zamani lakini iliiishia kwenye vitabu bila kutekelezwa huku Pesa ikiamishiwa Kwa vitu visivyokuwa vya maana. Katika maelezo ya mama Rais Samia amemweleza vizuri alivyokuwa anatekeleza unabii wake, unaambiwa hakupenda kudanganywa Wala longolongo.

Alipenda kila mtu atimize wajibu Kwa alichoagizwa ndio maana kama ukichelewa anakutumbua Na kuweka anayejua kuwajibika. Watu wachache kupitia maono yake wanaweza kusema alikuwa Na chembe chembe za udectata lakini kumbe sivyo. Katika kupambana Na Mabeberu mawakala wa Mabeberu lazima waweke vikwazo asitimize malengo. Alipoanza kununua ndege Kwa Kashi walilalama kuwa ndege zinanunuliwa Kwa mikopo ilihari Pesa zipo.

Alipoanza kupanua ubungo watu walimwona katili wakati wao hawakuwa Na hati ya kumiliki ardhi ya serikali huku wakijua ardhi Ni Mali ya serikali Kwa matumizi sahihi. Vyama vya upinzani vipo lakini vyama vinavyojinasibu kuwa wapinzani vimekaa kiualakati hivyo kukosa misimamo dhabiti kuonyesha Nia ya Kweli katika kuikomboa Tanzania.

Uwezi kuwa unapambana Na adui harafu unaomba msaada Kwa adui. Adui Yetu mkubwa Ni beberu anayekaa ulaya , ndani mkitofautiana wewe unaenda kushitaki Kwa adui mkuu Na kumpa njia za kutudhuru. Mwl. Nyerere alivyokuwa anaipambania Afrika alitumia nguvu nyingi lakini hawakukosa wachumia tumbo waliokuwa wanakwamisha ukombozi wa Kweli.

Tuliona walivyofanikiwa kuua ujamaa, tuliona walivyotumia viongozi wetu wa mwanzoni kwenye awamu tofauti tofauti kutekelezwa malengo Yao kuikwamisha Afrika kupitia ushauri wao wa ubinafshishaji tukajikuta tunabinafaisha kila kitu Leo hii viwanda vimekuwa magofu wajanja wanafugia mbuzi, kiwanda kinafanywa Chuma chakavu.

Nabii Magufuri alipoanza kuondoa waliotelekeza viwanda Na kuvigeuza ardhi ya kukopea Na kufanya mambo kinyume ya makubaliano, WaPo viongozi ambao waliosababisha haya waliomba misamaha kupitia tungo zao za kiuandishi kama Historia ya Maisha Yao. Nina huzuni Sana Nabii Magufuri hakuacha kitabu cha Maisha yake labda kingeleta usisimuzi wa kuishi wa aliyoyaanzisha katika harakati zake za kupambana Na Mabeberu katika Vita ya kiuchumi.

Mwisho namwomba Mama Rais S.S.H aendeleze mapambano Kwa Kadri itakavyokuwa, Nabii Magufuri aliponyoosha asikubali papinde, tunakuamini kumbuka Nabii hakubaliki kwao lakini Ni wewe mshika mikoba ya maono ya aliyoyaona katika kuikomboa Africa. Kupitia viatu vyake uenda ukateuliwa kuwa Mama Wa Africa au Mwenyekiti wa AU.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom