Hayati Magufuli ni Nabii wa Afrika aliyechelewa kueleweka katika ukombozi wa pili wa Mwafrika, hakuogopa vigingi vya Mabeberu

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
1,595
2,000
Usijifanye kunguru mwoga, kwani kabla ya wazungu hakuna nchi ambazo zilikuwa Na maendeleo ya watu Na vitu. Mali, misdi Na nyingine nyingi kabla ya Mabeberu zilikuwa vizuri. Sasa wewe ushatskwa Na wazungu uwezi kutoka Korea ya Kaskazini inaendeshwa Na Mabeberu? Mungu mnasomea nini kama vyuo vipo lakini uwezi hata kutengeneza wemb Na sindano mpaka uagize. Nabii Magufuri Alianza ndogo ndogo kuondoa haya.
Hayo yote ni maneno matupu ya kijipa ushujaaa wakati hakuna chochote hao wa Misri unao wasema sio wenzako hao 68% ya uchumi wa wamisri wanategemea mzungu usijivike ujinga wakati ukweli unaujua, we unaleta maswala ya hapo zamani? Acha ujinga sasa hiyo hapo zamani imeshindwaje kudumu hadi sasa?
 

ORCA ACE

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
975
1,000
Asante,
Sawa ila ulipokopi uzi wako ungeomba mtu mwingine akufanyie paragraph setting ndipo upachike hapa.

Although nabii huwa hatumii nguvu, kuruhusu kuua, nabii anakazi moja au mbili ikiwepo kuonya nk.

Sasa huyo nabii wako hakuwa na tone la unabii, it was the same like false prophet.
 

kookaburra

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
209
1,000
Mimi shida yangu iko hapo kwenye kumtanguliza Mungu, hivi ukishatasema hayo maneno basi imetosha ? "NAMTANGULIZA MUNGU" halafu baaasi??
Hakuna rewuirements zingine?
Maneno tu yanatosha kumtanguliza Mungu?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,595
2,000
Wana Jf
Nianze Kwa kumtanguliza Mungu kama Nabii Dr. Magufuri alivyopendelea kumtanguliza Mungu kila wakati.

Ninaposema Dr. Magufuri Ni Nabii wa Africa aliyetumwa kuikomboa Africa mara ya pili ninamaanisha kuwa Kwa Yale mahubiri yake ya kutaka Africa tujitathimini kupenda vyetu ili kujinasua mikononi mwa Mabeberu. Unyonyaji unaofanyika nchi nyingi Ni kutokana Na watu kukosa uzalendo Na kukumbatia njia zote za kinyonyaji kupitia mikataba feki. Mabeberu waliiteka Africa Kwa njia zote za kiuchumi, kupitia mawakala wao kama WHO, WB, UN, IMF Na nyingine nyingi. Kwa kulitambua Hilo Magufuri pamoja Na uwezo ndogo kufuatana Na anaopambana nao aliweza kuanza kufumua mikataba ya kinyonyaji. Pengine Unaweza kusema Kwa nini hakupenda democrasia iliyozidi kipimo jibu Ni kwamba mpaka Sasa hakuna democrasia ya Kweli tunayoaminishwa. Tumejionea marumbano Na watu kupoteza Maisha katika uchaguzi wa USA. Ambayo duniani tunaiona kama kiranja mstaarabu anayejua democrasia Na kuitumia vilivyo. Kwenye kudhamilia kitu cha kuleta maendeleo hakuna democrasia, ukiacha uende Na democrasia vitu vingi vitakwama kwenye utekelezaji. Tuliona miradi mingi iliyoandikwa zamani lakini iliiishia kwenye vitabu bila kutekelezwa huku Pesa ikiamishiwa Kwa vitu visivyokuwa vya maana. Katika maelezo ya mama Rais Samia amemweleza vizuri alivyokuwa anatekeleza unabii wake, unaambiwa hakupenda kudanganywa Wala longolongo. Alipenda kila mtu atimize wajibu Kwa alichoagizwa ndio maana kama ukichelewa anakutumbua Na kuweka anayejua kuwajibika. Watu wachache kupitia maono yake wanaweza kusema alikuwa Na chembe chembe za udectata lakini kumbe sivyo. Katika kupambana Na Mabeberu mawakala wa Mabeberu lazima waweke vikwazo asitimize malengo. Alipoanza kununua ndege Kwa Kashi walilalama kuwa ndege zinanunuliwa Kwa mikopo ilihari Pesa zipo. Alipoanza kupanua ubungo watu walimwona katili wakati wao hawakuwa Na hati ya kumiliki ardhi ya serikali huku wakijua ardhi Ni Mali ya serikali Kwa matumizi sahihi. Vyama vya upinzani vipo lakini vyama vinavyojinasibu kuwa wapinzani vimekaa kiualakati hivyo kukosa misimamo dhabiti kuonyesha Nia ya Kweli katika kuikomboa Tanzania. Uwezi kuwa unapambana Na adui harafu unaomba msaada Kwa adui. Adui Yetu mkubwa Ni beberu anayekaa ulaya , ndani mkitofautiana wewe unaenda kushitaki Kwa adui mkuu Na kumpa njia za kutudhuru. Mwl. Nyerere alivyokuwa anaipambania Afrika alitumia nguvu nyingi lakini hawakukosa wachumia tumbo waliokuwa wanakwamisha ukombozi wa Kweli. Tuliona walivyofanikiwa kuua ujamaa, tuliona walivyotumia viongozi wetu wa mwanzoni kwenye awamu tofauti tofauti kutekelezwa malengo Yao kuikwamisha Afrika kupitia ushauri wao wa ubinafshishaji tukajikuta tunabinafaisha kila kitu Leo hii viwanda vimekuwa magofu wajanja wanafugia mbuzi, kiwanda kinafanywa Chuma chakavu. Nabii Magufuri alipoanza kuondoa waliotelekeza viwanda Na kuvigeuza ardhi ya kukopea Na kufanya mambo kinyume ya makubaliano, WaPo viongozi ambao waliosababisha haya waliomba misamaha kupitia tungo zao za kiuandishi kama Historia ya Maisha Yao. Nina huzuni Sana Nabii Magufuri hakuacha kitabu cha Maisha yake labda kingeleta usisimuzi wa kuishi wa aliyoyaanzisha katika harakati zake za kupambana Na Mabeberu katika Vita ya kiuchumi.

Mwisho namwomba Mama Rais S.S.H aendeleze mapambano Kwa Kadri itakavyokuwa, Nabii Magufuri aliponyoosha asikubali papinde, tunakuamini kumbuka Nabii hakubaliki kwao lakini Ni wewe mshika mikoba ya maono ya aliyoyaona katika kuikomboa Africa. Kupitia viatu vyake uenda ukateuliwa kuwa Mama Wa Africa au Mwenyekiti wa AU.

Msikilize mwenyewe hapa:

 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
5,267
2,000
Screenshot_20210321-075606~2.jpg
 

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,257
2,000
Unamuita mzungu beberu kumbe uhai wako umebebwa na pace marker iliyotengenezwa na beberu huyohuyo...maajabu hayataisha duniani hii.
 

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
3,335
2,000
Mchumia tumbo anaweza kuwa wewe Kwa kuwa unamawazo ya kinyonyaji kupitia maelezo yako. Usihukumu Magufuri Nabii wa africa
😂😂😂😂 Usipaniki. Mi nadhani umwite hata mungu wako ni sawa kwangu haina athari.usipaniki tulia bwana mdogo maisha bado yanaendelea. Nmekushauri kuwa unaweza mwita mungu wako kabisa si jambo baya....nyie mnaoishi kwa kulamba viatu vya watu mna shida sana. Huwa hamna dini,hamna jinsia wala rangi.
 

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
3,335
2,000
Mjinga aliye waaminisha kwamba kiongozi anaye chukia wazungu ndiye shujaa wa africa aliwatia ujinga wa kiwango cha juu sana kwa sababu hakuna africa inayo weza ku survive bila mzungu hakuna hivyo mawazo ya aina hiyo ni kujilisha upepo tu.
Huu ni upumbavu ambao wamekuwa nao waafrika wengi sana. Na unafiki mkubwa. Wanasema wanawachukia wazungu huku wakitumia asilimia 80 ya bidhaa zao. Sijaona mimi kiongozi ambaye akiumwa sababu ya chuki zake kwa wazungu anaamua akalazwe kwa mganga wa kienyeji bagamoyo au tanga.

Sijaona ambao wanatumia punda kusafiri,hawatumii simu,computers na kila innovation ya kizungu. Sijaona. Mi nashauri tuwachukie wazungu na vitu vyao vyote tubaki na afrika na uafrika wetu.
 

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
1,595
2,000
Usijifanye kunguru mwoga, kwani kabla ya wazungu hakuna nchi ambazo zilikuwa Na maendeleo ya watu Na vitu. Mali, misdi Na nyingine nyingi kabla ya Mabeberu zilikuwa vizuri. Sasa wewe ushatskwa Na wazungu uwezi kutoka Korea ya Kaskazini inaendeshwa Na Mabeberu? Mungu mnasomea nini kama vyuo vipo lakini uwezi hata kutengeneza wemb Na sindano mpaka uagize. Nabii Magufuri Alianza ndogo ndogo kuondoa

Huu ni upumbavu ambao wamekuwa nao waafrika wengi sana. Na unafiki mkubwa. Wanasema wanawachukia wazungu huku wakitumia asilimia 80 ya bidhaa zao. Sijaona mimi kiongozi ambaye akiumwa sababu ya chuki zake kwa wazungu anaamua akalazwe kwa mganga wa kienyeji bagamoyo au tanga.

Sijaona ambao wanatumia punda kusafiri,hawatumii simu,computers na kila innovation ya kizungu. Sijaona. Mi nashauri tuwachukie wazungu na vitu vyao vyote tubaki na afrika na uafrika wetu.
Hahahaaaa umemaliza mkuu, jitu eti linawachukia wazungu halafu limezungukwa na security systems za hao hao wazungu, hadi unajiuliza hivi hii mijitu ina akili kweli?

Maana tulitarajia tukute mtu analindwa na sime, mikuki, mishale , mapanga ya jadi , kombeo nk. Hapo labda tungemuamini kweli hawapendi wazungu

Ni sawa na kumchukia mke halafu bado unakula vyakula anavyo kupikia unavaa nguo anazo kufulia halafu bado unadai anataka kukuua ni ujinga wa fikra tu.
 

The Icebreaker

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
8,792
2,000
Hayo yote ni maneno matupu ya kijipa ushujaaa wakati hakuna chochote hao wa misri unao wasema sio wenzako hao 68% ya uchumi wa wamisri wanategemea mzungu usijivike ujinga wakati ukweli unaujua, we unaleta maswala ya hapo zamani? Acha ujinga sasa hiyo hapo zamani imeshindwaje kudumu hadi sasa?
Kwahiyo mkuu wewe unashauri nini kifanyike ili kuondoa huo utegemezi toka kwa hao wazungu?
Ushauri wako ni upi kwenye hilo? au unataka mzungu ategemewe na wengine mpaka Dunia itakapoisha?
 

MICHAEL JACKSONN

Senior Member
Mar 16, 2021
189
250
Sawa ila ulipokopi uzi wako ungeomba mtu mwingine akufanyie paragraph setting ndipo upachike hapa.

Although nabii huwa hatumii nguvu, kuruhusu kuua, nabii anakazi moja au mbili ikiwepo kuonya nk.

Sasa huyo nabii wako hakuwa na tone la unabii, it was the same like false prophet.
kawaida ya slow leaners huwa wanaelewa kwa muda mrefu.


wewe utachujua miaka 2 kuja kukiri.
 

polokwane

JF-Expert Member
Dec 16, 2018
1,595
2,000
Kwahiyo mkuu wewe unashauri nini kifanyike ili kuondoa huo utegemezi toka kwa hao wazungu?
Ushauri wako ni upi kwenye hilo? au unataka mzungu ategemewe na wengine mpaka Dunia itakapoisha?
Yaan jamaa yangu kifupi tu ni kwamba kwa sasa waafrica hasa weuzi tumesha chelewa sana na hakuna namna yeyote ya kufanya tukaacha utegemezi kwa wazungu na tukabaki salama,

vinginevyo tuamue kujitoa muhanga wafe wengi lakini hao wachache waanze kufanya innovation zenye asili ya africa kitu ambacho hakiwezekani kabisa so wacha maisha yaendelee maana utegemezi wa mtu mweusi kwa mtu mweupe ni wa kisayansi ni ngumu kupambana nao aisee.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom