Hayati Magufuli bado anawanyima usingizi wapinzani wa Tanzania

Yes ni kweli ndani ya uongozi wa huyu jamaa wapinzani bado hawaamini kwa katiba gani na sheria ipi ilimpa mamlaka kuzuia shughuli za kisiasa zote, mikutano ya hadhara na hata wabunge kutokwenda kwenye majibo mengine kufanya kazi ya siasa. Mbali zaidi bado hawaamini namna jamaa alivyoharibu uchaguzi mkuu wa 2020, yaani kifupi pamoja na kutangulia mbele ya haki ila kaacha machungu na mambo ya ajabu makubwa mno nyuma yake. Yaani ni mengi jamaa aliasisi - manunuzi (Bulk procurement) ya viongozi wa upinzani, viongozi wa upinzani kujeruhiwa / kupotea nk yote haya yanabakia kwenye record yake.
 
Historia imeandikwa na hakuna anaeweza ifuta kwamba John Pombe Magufuli ni rais bora kabisa kuwahi kutokea Afrika.

Dunia nzima na Watanzania wote wanajua namna alivyoipenda nchi yake na namna alivyowapigania Watanzania haswa wale wa hali ya chini.

Hii ni kitu hakuna anaeweza kuja kuifuta hata ishuke mbingu leo. Watoto wa uswahilini wanasemaga "imeisha iyooo"

Lakini wapinzani wa nchi hii hiyo kitu hawataki kabisa kukubaliana nayo, na ni kama bado wanamuogopa sana Magufuli.

Bado wamewekeza kupambana na Magufuli, wakilala wakiamka anaewasumbua sio kiongozi aliye madarakani. Wao anaewasumbua ni marehemu aliyepumzika kabulini.

Ama kwa hakika CCM inapaswa kujivunia sana Magu maana kama ni kazi ya kusimamisha chama dola aliifanya kwa mafanikio makubwa.

Haya mashambulizi ya wapinzani kwa marehemu inaonesha kabisa wanajua aliyewafuta kwenye ulimwengu wa siasa wanamjua na wanajua mpaka wananchi wamewapuuza na still wanamuamini sana hayati Magufuli.

Kiukweli hawaamini wanachokiona, mtu amekufa lakini bado ana nguvu mitaani kushinda walio hai.

Kuna siku atatokea mwanasiasa ataubiri sera na misimamo ya Magufuli na atawasumbua sana wapinzani.

Mama Samia amesafishiwa njia anachotakiwa ni kuteleza tu kwa kasi kubwa.
Làbda anawanyima usingizi hao waliokuzaa, nobody else
 
Wapinzani hawapambani na John mtoto wa Magufuli ila wanapamba na raisi wa awamu ya tano ili watawala wengine wasije kufanya Yale ambayo kwao waliona hayakua mazuri.. Ni jambo la kawaida kwene siasa na ulimwengu wa utawala... Hata Burundi nkurunzinza kafariki lakini warundi hasa waliokuwa wapinzani huendelea kuongelea utawala wake, hiyo ni jambo la kawaida Dunian kote once ikishika nafasi ya umma hata ufe people will still talk about your regime.... Hamna binadamu anaeogopa mtu aliekufa hiyo haipo labda kama anamatatizo yake ya akili..
JPM ni talk of the town....kila kona kuna kilio cha kumkumbuka JPM...hata ukimchukia vipi kuna namna lazima ukubali aliweza kuconnect na watu wa chini.. ndio maana bado wapinzani wanamuona ni kikwazo kwao
 
Anawanyima usingizi nyie MATAGA ambao kwa upande mmoja mmegoma kabisa kuamini kuwa Mwendazake amefariki, na upande mwingine mnaendelea na ndoto za alinacha kuwa "ataendelea kuwa hai kupitia the so-called legacy yake."

Tatizo la nyie wahuni, "kila baya" lahusu WAPINZANI. Mfarakano kuhusu Magufuli upo ndani ya CCM, lakini haiwazuwii ninyi kugeuza kuwa suala hilo limebebwa na WAPINZANI.

Bottom line is, MTAPATA SHIDA SANA unless you come to terms with the reality kuwa Mwendazake is gone.... forever.
Karibu Tanzania upite kwenye mitaa usikie wananchi wanayoongea kila leo kuhusu JPM.... mtaani ni hero upende ama usipende.

Usifikiri wapinzani wanamuogopa mpaka leo for no reason, wanaipata feedback ya ukweli.

Anyways, pole najua kurudi bongo ni kitu ulishasahau...hauna maisha tena, hauna identity....upo kama kasha 🤔🙈🙈😂
 
JPM ni talk of the town....kila kona kuna kilio cha kumkumbuka JPM...hata ukimchukia vipi kuna namna lazima ukubali aliweza kuconnect na watu wa chini.. ndio maana bado wapinzani wanamuona ni kikwazo kwao
Ni jambo la kawaida kwa kila kiongozi unapokua madarakani lazm utakubalika mahala nakuna mahala hutokubalika... Hata wakati wa JPM Kuna watu weng tu waliona ni heri wakati wa JK, kumbuka nchi ya Tanzania haina watu wa hali ya Chini peke ake... Uwe Chini au juu maadam ww ni mtanzania unahaki ya kuneemeka na uongozi uliopo madarakani... Ni sahihi Kuna maeneo wanamkumbuka lakn kaa ukijua sio watu wote na pia vilevile Kuna wa Tz kibao wanaona afadhali wanaona samia ni bora kuliko JPM... Na ndo Maan ikaitwa nchi inawatu wengi so huwezi ukawa please wote JPM hakuwa Mungu... Kama nyerere baba wa Taifa alisemwa na kusimangwa who is magufuli
 
RIP THE BEST EVER PRESIDENT OF JMT, MUNGU ALIMTUMA KUFANYA KAZI MAALUM YA KUWEKA MIFANO KISHA AKAMUITA AKAMPE KAZI NYINGINE YA UTUKUFU MBINGUNI....
I miss my President soo much...
Kamfuate umbusu. Wewe itakuwa muuaji uliyetekeleza mauaji yote kwa amri yake
 
JPM ameshafariki,lakini bado kuna watu wanateseka naye, Pamoja na wao kwa sasa kushika madaraka, vyeo kushangilia kifo chake.
Bado wanajihisi inferior mbele marehemu

jamaa alikuwa chuma kweli kweli, jiwe hasa

Hata hivyo wote tutakufa, na kifo sio adhabu
Stop nonsense, Hilo jitu limeua watu! Mengine ya kuona Mali naweza samehe, lkn siyo roho za watu.
 
Historia imeandikwa na hakuna anaeweza ifuta kwamba John Pombe Magufuli ni rais bora kabisa kuwahi kutokea Afrika.

Dunia nzima na Watanzania wote wanajua namna alivyoipenda nchi yake na namna alivyowapigania Watanzania haswa wale wa hali ya chini.

Hii ni kitu hakuna anaeweza kuja kuifuta hata ishuke mbingu leo. Watoto wa uswahilini wanasemaga "imeisha iyooo"

Lakini wapinzani wa nchi hii hiyo kitu hawataki kabisa kukubaliana nayo, na ni kama bado wanamuogopa sana Magufuli.

Bado wamewekeza kupambana na Magufuli, wakilala wakiamka anaewasumbua sio kiongozi aliye madarakani. Wao anaewasumbua ni marehemu aliyepumzika kabulini.

Ama kwa hakika CCM inapaswa kujivunia sana Magu maana kama ni kazi ya kusimamisha chama dola aliifanya kwa mafanikio makubwa.

Haya mashambulizi ya wapinzani kwa marehemu inaonesha kabisa wanajua aliyewafuta kwenye ulimwengu wa siasa wanamjua na wanajua mpaka wananchi wamewapuuza na still wanamuamini sana hayati Magufuli.

Kiukweli hawaamini wanachokiona, mtu amekufa lakini bado ana nguvu mitaani kushinda walio hai.

Kuna siku atatokea mwanasiasa ataubiri sera na misimamo ya Magufuli na atawasumbua sana wapinzani.

Mama Samia amesafishiwa njia anachotakiwa ni kuteleza tu kwa kasi kubwa.
Wakati mwingine msiwe mnaweka upumbavu wenu in public, Magufuli alikuwa muuaji katili asiye na huruma ndo maana Mungu alimchukua haraka ili kuinusuru Tanzania, nyie mnaomwambudu hamieni Chato kwenye kaburi lake labda atafufuka aje kuwaongoza
 
Historia imeandikwa kwa jitu katili , muuaji kuwahi kutawala Tanzania.
Azory Gwanda, Ben Saanane, maiti za kwenye sandarusi Coco Beach, MKIRU
Habari.

Kuna watu waliimba na kuhubiri,
Kusujudu na kurukaruka.
Kunywa bia na kuponda bata la kufa mtu kwamba kwa maisha yao yatakuwa bora mno baada ya Magufuli.

Leo ni miezi 8 bila Magufuli lakini kila wakigeuka huku hakuna umeme, wakigeuka hakuna maji ,wakigeuka huku mbolea lakini moja, wakigeuka huku wanafukuzwa kwenye migodi ,wakigeuka huku wanafukuzwa kwenye mitaa, wakigeuka huku Mungu wao yuko jela kwa ugaidi.

Leo ndiyo wamejua Magufuli alikuwa anafanya kwa ajili yao?
Jinga kabisa na bado mtaendelea kuwa watumwa hivyo hivyo.
Waliowadanganya wamtukane Magufuli wote wamepata mabwana Ulaya wanalishwa bure.

Malipo ni hapa hapa duniani.
 
Upinzani unapata shida sana mpaka sasa kupambana na legacy yake. Jpm ndio aliwapoteza upinzani kwa wananchi kwa kupiga kazi. Sasa hivi wako bize kumchafua ila wapi...
Kumbe kuwapoteza wapinzani kwa ukatili wa kuua na kubambika kesi nayo ni sifa?
 
Naunga mkono hoja, hata mimi hili niliwahi kulisema humu
P
Best president wa kuua na kubambika kesi?
 
Back
Top Bottom