Hayati Magufuli bado anawanyima usingizi wapinzani wa Tanzania

happyxxx

Senior Member
Nov 14, 2020
195
1,000
Historia imeandikwa na hakuna anaeweza ifuta kwamba John Pombe Magufuli ni rais bora kabisa kuwahi kutokea Afrika.

Dunia nzima na Watanzania wote wanajua namna alivyoipenda nchi yake na namna alivyowapigania Watanzania haswa wale wa hali ya chini.

Hii ni kitu hakuna anaeweza kuja kuifuta hata ishuke mbingu leo. Watoto wa uswahilini wanasemaga "imeisha iyooo"

Lakini wapinzani wa nchi hii hiyo kitu hawataki kabisa kukubaliana nayo, na ni kama bado wanamuogopa sana Magufuli.

Bado wamewekeza kupambana na Magufuli, wakilala wakiamka anaewasumbua sio kiongozi aliye madarakani. Wao anaewasumbua ni marehemu aliyepumzika kabulini.

Ama kwa hakika CCM inapaswa kujivunia sana Magu maana kama ni kazi ya kusimamisha chama dola aliifanya kwa mafanikio makubwa.

Haya mashambulizi ya wapinzani kwa marehemu inaonesha kabisa wanajua aliyewafuta kwenye ulimwengu wa siasa wanamjua na wanajua mpaka wananchi wamewapuuza na still wanamuamini sana hayati Magufuli.

Kiukweli hawaamini wanachokiona, mtu amekufa lakini bado ana nguvu mitaani kushinda walio hai.

Kuna siku atatokea mwanasiasa ataubiri sera na misimamo ya Magufuli na atawasumbua sana wapinzani.

Mama Samia amesafishiwa njia anachotakiwa ni kuteleza tu kwa kasi kubwa.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,828
2,000
"Kazi ya kusimamisha chama dola aliifanya kwa mafanikio makubwa"

Hayo "mafanikio makubwa" umeyapima vipi kama hapakuwepo na vyama dola vingine vya kushindana nae?

Kama unakiri CCM ni chama dola basi hakistahili kuwepo Tanzania, Tanzania inataka vyama vya siasa ndivyo sheria yetu inavyotamka.
 

mweusi asili

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
1,659
2,000
Dunia nzima na Watanzania wote wanajua namna alivyoipenda nchi yake na namna alivyowapigania Watanzania haswa wale wa hali ya chini.
hebu tuambie amepigania nini kwa watanzania wa hali ya chini?,

umasikini umepungua au umeisha?

huduma za msingi zimeboreshwa?

vipi kuhusu ajira na kujiajiri?

je wananchi walipewa nguvu ya kuamua mambo yao na yakatelezwa?

je sheria na katiba ilifanya kazi na kulindwa?

vipi kuhusu kutoa na kupata habari au haki za kujieleza?
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,473
2,000
Historia imeandikwa na hakuna anaeweza ifuta kwamba John Pombe Magufuli ni rais bora kabisa kuwahi kutokea Afrika.

Dunia nzima na Watanzania wote wanajua namna alivyoipenda nchi yake na namna alivyowapigania Watanzania haswa wale wa hali ya chini.

Hii ni kitu hakuna anaeweza kuja kuifuta hata ishuke mbingu leo.
Ama kwa hakika CCM inapaswa kujivunia sana Magu maana kama ni kazi ya kusimamisha chama dola aliifanya kwa mafanikio makubwa.

Mama Samia amesafishiwa njia anachotakiwa ni kuteleza tu kwa kasi kubwa.
Naunga mkono hoja, hata mimi hili niliwahi kulisema humu
P
 

zlatan9

JF-Expert Member
Oct 25, 2016
473
1,000
JPM ameshafariki,lakini bado kuna watu wanateseka naye, Pamoja na wao kwa sasa kushika madaraka, vyeo kushangilia kifo chake.
Bado wanajihisi inferior mbele ya marehemu

jamaa alikuwa chuma kweli kweli, jiwe hasa

Hata hivyo wote tutakufa, na kifo sio adhabu
 

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
2,596
2,000
Hata Adolf Hitler anakumbukwa hadi leo, miaka 76 baada ya kifo chake. Kukumbukwa si kigezo cha kuwa mtu alikuwa bora.
Wengine wanaokumbukwa:
  1. Idi Amin wa Uganda
  2. Jean Bedel Bokassa wa Central Africa Republic
  3. P.W. Botha kaburu mbaguzi mkuu wa South Africa
  4. Pol Pot wa Cambodia
  5. Samuel Doe wa Liberia
Na wengine wengi wa aina hiyo. Na wote hao wana mashabiki wao wanaoamini kuwa hao watu walikuwa viongozi wazuri sana wa kuigwa.
Kwa hiyo si ajabu ukiwa shabiki wa huyo uliyeamua kumshabikia. Walisema wahenga "ndege wafananao huruka pamoja".
Ruka naye tu kaka Pascal Mayalla
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom