Hayati Magufuli atakumbukwa sana kwa matendo yake mema aliyotuachia

Yaani mpka Ndugai ameamua kuwa mkosoaji hii hatari. Walifikiri wakiwamaliza wapinzani wao watakuwa salama. Dhambi ya ubaguzi inawala Sasa.
 
Kama ww ni mfuasi wake mwaminifu, mfuate kaburini. Acha kutuchosha na hadithi za Ibilisi....
 
Mimi najaribu kumkumbuka kwa Mambo machache ambayo jamaa ameacha Legacy au kumbukumbu ya daima nchini. Sidhani Kama Kuna mtu mwenye Akili timamu anaweza kusahau kazi zake.

Kwanza Magufuli alikuwa kimbilio la wahanga mbali mbali, kwa mfano wahanga wa tetemeko kule Bukoba walisaidiwa kwa Hali na Mali na utawala wake, misaada ilimiminika huko Bukoba mpka nafasi ya kuiweka ikawa haitoshi.l

Pili wakati wa utawala wake demokrasia ilikuwa Sanaa kiasi kwamba hadi wapinzani waliruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano mchana na usiku popote pale nchini.

Tatu uchumi umekuwa kwa Haraka Sana na kusababisha kuongezeka kwa bei za mazao ya kilimo Kama Korosho, Mahindi, Mpunga na kahawa kiasi kwamba wakulima kwa Sasa wanakenua meno tuu kwa furahaa.

Ukija kwa wafanyakazi serikalini maisha yao yalikuwa mazuri Sanaa, aliwapandisha mishahara kwa wakati na kuwapandisha vyeo stahiki kila wakati na hii ilisaidia Sana wafanye kazi kwa ari kubwaa.

Ukija upande wa haki za Binadamu anastahili pongezi kubwaa. Hakupenda uonevu kabisaa. Hakupenda mauaji ya raia ,utesaji,utekaji Wala kubambikia watu makosa ya uongo.

Ukija katika utawala Bora jamaa alikuwa vizuri, Bunge likawa huru na Mahakama ikawa huru kweri kweriii. Mapato na matumizi ya pesa za walipa kodi yakawa swafiii. CAG alipokuwa anakagua mahesabu ya ofisi yake Ikulu hakupata dosari yeyote zaidi ya kumsifu kwa matumizi Bora za pesa wanyonge.

Pia hakupenda Ile tabia ya kutembea na maburungutu ya pesa za walipa kodi na kuzitapanya mabarabarani. Alikuwa mtu smart Sanaa.Aliamini ktk utawala wa sheria siku zote.

Kwa kuwa Biblia inasema mtu akifa na matendo yake huambatana nae basi tunaamini kwa matendo haya aliyo tutendea atakuwa sehemu sahihi.
Mbona umeandika KINYUME chake? Anyway, wenye akili tumekuelewa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
drakelaugh.png
 
Back
Top Bottom