Hayati Magufuli anashambuliwa kila kona. Siyo kesi, ila mambo yaende; yasipoenda wananchi watawazomea kila kona

Nasubiri baada ya miaka miwili nitawapima kwa indicator zifuatazo
1. Thamani ya pesa yetu shilingi dhidi ya dola ya kimarekani
2. Mfumuko wa bei hasa bei ya mafuta (petrol & Dieseli)
3. Madeni ya nchi
4. Miradi mipya ya maendeleo
5. Ajira
6. Upandaji wa mishahara na madaraja
7. Hospitali mpya na vituo vya afya
8. Huduma za kijamii pamoja na elimu
9. Miundo mbinu ya barabara, reli nk
10. Umaliziwaji wa miradi iliyoachwa
11. Hali ya madawa ya kulevya nchini pamoja na ufisadi
12. Kuongezeka kwa makusanyo serikalini
 
Power and speed is nothing without control,kama ubabe wake wote ule mwisho wake ni huu wizi na ugumu wa maisha tunaoupata,tunaendaje mbele nayeye katukwamisha??tunahitaj kuweka mambo sawa kwanza Ili twende mbele,,that's why unaona lazima hii misukule yake tuipige chini
 
Sawa, lakini alituaminisha kabana mianya ya rushwa kweri kweri kumbe porojo
muulize mtaakamu yeyote wa uhalifu duniani atakuambia unapunguzwa haumalizwi!

Magufuli alijitahidi sana kuupunguxa
 
Huyu alifurushwa kutoka TRA anaweza akatumiwa vilevile. Sisi tuliona siku ya tatu baada ya maziko hii ripoti kupokelewa na ilikuwa Jumapili.

Wapambe nuksi wakaanza kumchafua mwenda zake kwamba ingekuwa ni yeye angekuwa kanisani akihutubia kutoka madhabahuni. Mungu akawa amewasahaulisha na wakasahau mwendazake ilikuwa ni zake pia kuapisha jumapili.

Mareheme siku ya tatu kaburini watu walianza kumpakaza hii oil chafu kama mafuta.
Kama unapingana na CAG lete naww ushahid wako Ili umsafishe mwendazake,

Ukweli lazima usemwe tuh,alikua kibaka,ni kibaka tuh no way out lazima tuseme
 
Spidi aliyokuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ni challenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani kuifikia baada ya kifo chake

Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.

Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai

Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge

Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.
Magufuli anavuna alichopanda.
Wakati wa uhai wake mlikuwa mnamshangilia kila afanyalo kwa unafiki tu.

Mlikuwa mnapalilia kitumbua chenu kisiingie mchanga.

Watu walilazimishwa kumshangilia na kumuimbia nyimbo za mapambio.
 
muulize mtaakamu yeyote wa uhalifu duniani atakuambia unapunguzwa haumalizwi!

Magufuli alijitahidi sana kuupunguxa

Kapunguza wapi?angewepo leo hapa ukweli huu tusingeujua,lazima angembana CAG asiongee...

Yule mwizi tuh,na tutaujua ukweli mwingi saiz,tulieni
 
Spidi aliyokuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ni challenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani kuifikia baada ya kifo chake

Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.

Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai

Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge

Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.
kinachofurahisha zaidi walewale waliompamba, wale wale waliokwenda kupokea ndege kwa mbwembwe - leo hii hata arobaini bado wanahoji Tuendelee kuzinunua ama tusiendeleeee.....? Wale wale waliojenga NYUNGU pale Muhimbili ndiyo walewale leo wanavaa barakoa na jengo lile halina mteja hata mmoja.

Hawa ndiyo wanasiasa na hii ndiyo Tanzania yetu.

Kama unabii ni kutabiri yajayo basi Lema anastahili ..... yote haya aliyatabiri kinagaubaga!!
 
Kwa akili zako kabisa unasema SGR imeleta hasara? Kweli tuma safari ndefu. Hiyo bilioni 3 ni tozo ya vibali ambayo ingepatikana kama hao wafanyakazi wa kigeni wangelipiwa vibali vya kazi. Kuna idara za serikali zinazopaswa kufanya ukaguzi sehemu za kazi ili kuona kama wafanyakazi wa kigeni wamefuata taratibu. Unaweza kuta kuna kipengele katika mkataba wa ujenzi ambacho kinamruhusu contractor kusamehewa hiyo tozo. Kama hakuna hicho kipengele basi bado idara husika inaweza kudai hizo pesa na zikalipwa. Kudai eti SGR ni hasara inaonyesha aidha unaongozwa na chuki dhidi ya Magufuli au huna uelewa. Kwanza gharama za kujenga SGR ukilinganisha na gharana zilizopangwa kutumika wakati wa JK utaona kuwa mkataba wa sasa ni nafuu mno.

Mkuu kuwa muelewa ,CAG amesema wazi kuna wafanyakazi wa kigeni wameajiriwa kufanya kazi kwenye SGR huku wakiwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini.....Kitendo tu cha kufanya kazi bila vibali ina maana serikali imepoteza Tsh 3.5 Bilioni ,ngoja niweke sawa ili kukufurahisha ,serikali imepata faida ya Tsh 3.5 Bilioni kutokana na makusanyo ya vibali vya wafanyakazi wa kigeni wa SGR.

Kama wangekusanya ingekuwa ni Faida kwa serikali ila kama hawajakusanya sijui nini tuite mkuu? Kinyume cha faida ni nini?
 
Mkuu, mbona tulikua tunaambiwa kila pesa iliyokua inatumika ni kutokana na mapato yetu ya ndani? Unataka kusema tulikua tunakopa tena?
Hajaacha deni tu acha uongo.kaacha vitu vilivyotumia hiyo pesa pia.Eti kaacha deni utafikiri hizo pesa alikopa akaenda kuweka pesa kwenye akaunti yake uswisi.

Lugha ya ki layman utafikiri mtu hata shule hukwenda. Hiyo miradi kila mkoa na wilaya huioni au ? Elimu bure huioni au ? umeme kila kijiji huuoni au? barabara kila kona huoni au? vituo vya afya kote nchini huoni au nk

Kipindi chake nchi ilikuwa inakopesheka na madeni yalikuwa yanalipika bila shida.Wakopeshaji walituamini

Twende sasa ni challenge kwa serikali iliyopo itamudu kukopesheka na kulipa madeni na kuendesha miradi nchi nzima kama Magufuli alivyomudu? muda ni mwalimu mzui.let us wait and see tuone matusi kwa Magufuli kama yana mantiki
 
kinachofurahisha zaidi walewale waliompamba, wale wale waliokwenda kupokea ndege kwa mbwembwe - leo hii hata arobaini bado wanahoji Tuendelee kuzinunua ama tusiendeleeee.....? Wale wale waliojenga NYUNGU pale Muhimbili ndiyo walewale leo wanavaa barakoa na jengo lile halina mteja hata mmoja.

Hawa ndiyo wanasiasa na hii ndiyo Tanzania yetu.

Kama unabii ni kutabiri yajayo basi Lema anastahili ..... yote haya aliyatabiri kinagaubaga!!
ungetarajia kwa utu uzima wao ambao wengi wanao na mishahara mikubwa wanayolipwa ingewabadilisha kuwaondoa kwenye unafiki na kuwa wapigania wanyonge kama Magufuli lakini wapi.Hili limenistua .Mijitu ina watoto wakubwa sio tegemezi tena halafu bado minafiki .Shenzi type

Tunakoenda tunahitaji kizazi kipya cha wa wanasiasa hawa wengi waliopo ni hopeless kabisa .
 
Mkuu kuwa muelewa ,CAG amesema wazi kuna wafanyakazi wa kigeni wameajiriwa kufanya kazi kwenye SGR huku wakiwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini.....Kitendo tu cha kufanya kazi bila vibali ina maana serikali imepoteza Tsh 3.5 Bilioni ,ngoja niweke sawa ili kukufurahisha ,serikali imepata faida ya Tsh 3.5 Bilioni kutokana na makusanyo ya vibali vya wafanyakazi wa kigeni wa SGR.

Kama wangekusanya ingekuwa ni Faida kwa serikali ila kama hawajakusanya sijui nini tuite mkuu? Kinyume cha faida ni nini?
SGR haikaleta hasara, fikiria kama isingejengwa je bado ungesema tumepata faida? Kilichokosekana ni tozo ambayo haikulipwa na ambayo hata sasa inaweza kudaiwa na ikalipwa.
 
Hajaacha deni tu acha uongo.kaacha vitu vilivyotumia hiyo pesa pia.Eti kaacha deni utafikiri hizo pesa alikopa akaenda kuweka pesa kwenye akaunti yake uswisi.

Lugha ya ki layman utafikiri mtu hata shule hukwenda. Hiyo miradi kila mkoa na wilaya huioni au ? Elimu bure huioni au ? umeme kila kijiji huuoni au? barabara kila kona huoni au? vituo vya afya kote nchini huoni au nk

Kipindi chake nchi ilikuwa inakopesheka na madeni yalikuwa yanalipika bila shida.Wakopeshaji walituamini

Twende sasa ni challenge kwa serikali iliyopo itamudu kukopesheka na kulipa madeni na kuendesha miradi nchi nzima kama Magufuli alivyomudu? muda ni mwalimu mzui.let us wait and see tuone matusi kwa Magufuli kama yana mantiki
Nilikua Ddodma St Gemma Hosp huku mtaani kusema Magu mbaya hawakuelewi yaani wamama wale wanamsifia na wanasema kabisa bila Magu mwanangu asingesoma yaani huyu baba sijui yani km tutapata km yeye.Mama SAMIA ajipange sana akifanya masihhara atazomewa kweli
 
Mwendazake ni raisi m'bovu kuwahi kutokea katika sayari hii na karne hii.

Mwendazake alimzidi hadi Mobutu Seseseko Wa Zamboanga Wa Zaire.

Mwendazake alikuwa mropokaji na mkurupukaji sana na amelitia taifa laana kubwa kusema uwongo wake.

Mwendazake alikuwa hajiamini maana alijenga bifu na wafanyabiashara eti serikali ndo ifanye biashara ..

Mwendazake hakupaswa kuzikwa kwa heshima, yeye alipaswa kufanyiwa kama Gaddafi alivyofanyiwa.

Mwendazake bora Mungu alimchukua mapema. Sasa hivi atakuwa kuzimu huko anakaangika kweli kweli.

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Kura zilipigwa au zililazimishwa kweli kupenda Chongo utaita kengeza
Na hao ndio population kubwa ya Tanzania zaidi ya asilimia 80 na ndio wanyonge wenyewe waliompigia kura na ndio alijitahidi kuwapelekea miradi mingi na elimu bure nk

Ndio aliosimama nao.Lisu alisimama na wanaoielewa akaambulia kura milioni moja

Magufuli akasimama na wasiojielewa wenye elimu duni na uelewa duni na machinga na ma ntilie nk.

Nakubaliana na wewe alisimama na wengi wa chini hakusimama na wachaje wa juu au middle class
 
Back
Top Bottom