Hayati Magufuli anashambuliwa kila kona. Siyo kesi, ila mambo yaende; yasipoenda wananchi watawazomea kila kona

Usimtishe SSH. Hao kska zako wakikosea wasisemwe? Ukweli usisemwe? Kumbuka hata mjomba wako alikuwa akisisitiza.."msema kweli ni mpenzi wa Mungu" au nasema uongo ndugu zangu?

Rais wa mpango na kusudi la Mungu wa Mbinguni hatishiwi huambiwa ukweli ili awe huru. Shetani na mawakala wake ndio hutafsiri huku ni kutishiwa. Shetani ni Baba wa Uongo wote.
 
Ni ujinga kunyamazia uchafu wa vyombo vya usalama ukitegemea mbeleko yao. Jeshi kubwa na imara kushinda majeshi yote ni Umma

Kama yeye ni msafi kama usemavyo kwa nini basi anatqka kuendelea kukalia mchakato wa Katiba mpya uliogharimu mabilioni ya Shilingi za walipa kodi wa Taifa hili na akiwa kati ya wanufaika wa mabillioni hayo? Tena mnufaika namba 2 kwa muktadha wa cheo alichokuwa nacho.
 
Ametuachia deni la Trillioni 18 katika kipindi chake cha miaka 5 tu. Hili pia linapaswa lilipwe.
Kabla yake jumla ya deni ilikuwa trillioni ngapi? Unapokosoa linganisha pia kwa vipindi tofauti.
 
Hajaacha deni tu acha uongo.kaacha vitu vilivyotumia hiyo pesa pia.Eti kaacha deni utafikiri hizo pesa alikopa akaenda kuweka pesa kwenye akaunti yake uswisi.Lugha ya ki layman utafikiri mtu hata shule hukwenda. Hiyo miradi kila mkoa na wilaya huioni au ? Elimu bure huioni au ? umeme kila kijiji huuoni au? barabara kila kona huoni au? vituo vya afya kote nchini huoni au nk

Kipindi chake nchi ilikuwa inakopesheka na madeni yalikuwa yanalipika bila shida.Wakopeshaji walituamini

Twende sasa ni challenge kwa serikali iliyopo itamudu kukopesheka na kulipa madeni na kuendesha miradi nchi nzima kama Magufuli alivyomudu? muda ni mwalimu mzui.let us wait and see tuone matusi kwa Magufuli kama yana mantiki
Umemjibu vizuri sana

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Spidi aliyokuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ni challenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani kuifikia baada ya kifo chake

Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.

Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai

Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge

Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.
Kwani kimebadilika nini? CCM si ile ile na uongozi ni wale wale CCM?

Ameondoka Aliyekuwa Rais na ameingia Makamu ambaye alikuwa msaidizi wa Mwendazake.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Ametuachia deni la Trillioni 18 katika kipindi chake cha miaka 5 tu. Hili pia linapaswa lilipwe.
I really do not give a damn as long as now I get water in my home for the first time since I was born!! Viva Magufuli.
 
View attachment 1747010

Mmesikia serikali ya wanyonge? Serikali takatifu ya shujaa wa Afrika, tuliyeambiwa amefuta ufisadi? Ngoja nikutajie machache;
Ujenzi wa SGR umesababisha hasara ya 3.5Bil kwa kuajiri wafanyakazi wa kigeni wasiokua na vibali.

Kigwangala alitumia 172M kuandaa Kili challenge lakini pesa hizo hazijulikani zilitumikaje (hazina risiti).

Akaunti ya jeshi la zimamoto ilitumika kupitisha 261M. Yani watu walipiga "mchongo" wakakosa akaunti ya kupitishia, wakatumia akaunti ya zimamoto. Zilipoingia wakazitoa wakasepa. Just imagine watu wana ujasiri wa kupitisha pesa chafu kwenye akaunti ya jeshi? Halafu tunaambiwa mwendazake alinyoosha nchi.
Wasafi walipewa 140M, TBC 201M na Clouds 629M kutangaza tamasha la Urithi Festival. Lakini hakuna mkataba wala risiti yoyote ya kujustify malipo hayo.
18Bil zilizokusanywa ktk wilaya 135 hazikufika serikalini. Yani zilikusanywa lakini wajanja wakalala nazo mbele.

3.9Bil zilitolewa kukarabati ndege ya ATCL iliyopaki tangu mwaka 2015, lakini hela imeliwa na ndege haijakarabatibwa. Yani watu walitafuna milioni 3,900 halafu hawakupaka hata rangi.Hayo ni baadhi tu ya "madudu" ya serikali takatifu ya mwendazake. Sijaongelea HESLB, TANAPA, TANROADS, SGR, Stligler's gorge, Stand ya Magufuli. Huko kuna madudu ya kutisha.

Lakini tuliaminishwa serikali ya mwendazake haikua na doa. Watu waliokosoa waliitwa vibaraka. Serikali takatifu haikutaka kunyooshewa kidole.
Tujifunze kutofautisha mtu msafi na anayeficha uchafu. Mwendazake hakua msafi bali alijua kuficha uchafu. Ndio maana akaminya uhuru wa habari. Hatukusikia skendo kama za Escrow tukadhani serikali yake ni safi, kumbe kuna skendo kubwa zaidi ya Escrow lakini zimefichwa uvunguni.Ndio maana nasema afadhali JK aliruhusu media ziwe huru. Skendo za Richmond, EPA, Escrow aliacha wananchi wajue. Lakini mwendazake alifunika skendo zisifike kwa wananchi.

Ndio maana watu wamemtania CAG atoe pia ripoti aliyopanga kumpa mwendazake, maana angekua hai asingethubutu kusema ATCL imepata hasara ya mabilioni, au SGR imeleta hasara, au mradi wa Stigler's umejaa madudu. Angeficha kwa sababu ndivyo mwendazake alivyopenda.

Tunahitaji viongozi wasafi, sio wanaojua kuficha uchafu.!

By Malisa Godlisten
Kwa akili zako kabisa unasema SGR imeleta hasara? Kweli tuma safari ndefu. Hiyo bilioni 3 ni tozo ya vibali ambayo ingepatikana kama hao wafanyakazi wa kigeni wangelipiwa vibali vya kazi. Kuna idara za serikali zinazopaswa kufanya ukaguzi sehemu za kazi ili kuona kama wafanyakazi wa kigeni wamefuata taratibu. Unaweza kuta kuna kipengele katika mkataba wa ujenzi ambacho kinamruhusu contractor kusamehewa hiyo tozo. Kama hakuna hicho kipengele basi bado idara husika inaweza kudai hizo pesa na zikalipwa. Kudai eti SGR ni hasara inaonyesha aidha unaongozwa na chuki dhidi ya Magufuli au huna uelewa. Kwanza gharama za kujenga SGR ukilinganisha na gharana zilizopangwa kutumika wakati wa JK utaona kuwa mkataba wa sasa ni nafuu mno.
 
Spidi aliyokuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ni challenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani kuifikia baada ya kifo chake

Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.

Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai

Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge

Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.

Mawazo ya kuwa na Magufuli day na ujenzi wa SANAMU zake yangalipo?
 
Hadi sasa mama kashafeli, mwezi mmoja madarakani ATCL haina uwezo wa kutoa GAWIO wakati enzi za mwendazake mi faida hadi raha.
mama kafeli je wkt atcl imekuwa iki make hasara since kufufuliwa kwake?
yeye anaridhi shirika na hali yake. na hili jambo si la kurekebisha ndani ya mwezi mmoja. hamna hiyo kitu
 
Nenda kaseme au umtukane Magu hadharani ndo utajua ... Kumsema marehemu vby sio vyema ndg yangu
Bado hujatoka chumbani kwako? Ile report ya cag imevuruga kila kitu Cha magu na kila mwananchi mwenye akili timamu na mzalendo amemdiss Sana magu kwa kuwaaminisha vingine na kutenda tofauti! Toka nje uingie kitaa uwasikie wanazengo!
 
Apumzike kwa amani ya bwana popote alipo iwe Mbinguni au Ahera

Rais wetu aliamini viongozi ambao walionekana ni wasomi na wabobezi sana pasipo kujua kuwa kuna mambo yalipaswa kujadiliwa na bunge letu tukufu.
 
apumzike kwa amani ya bwana popote alipo iwe mbinguni au ahera

raisi wetu aliamini viongozi ambao walionekana ni wasomi na wabobezi sana
pasipo kujua kuwa kuna mambo yalipaswa kujadiliwa na bunge letu tukufu
Tuseme tu, alikuwa mshauri wa washauri wake
 
Kwa ushahidi wa ripoti hii ya CAG Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi,fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda.
 
Spidi aliyokuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ni challenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani kuifikia baada ya kifo chake

Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.

Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai

Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge

Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.
Nakuomba dadavua na ripoti ya CAG.
Ni kama kaburi la halaiki alilotumia mwendazake limefunuliwa likiwa na uvundo wa maiti.
 
Akija kushtuka miaka minne imepita kilichofanyika ni kumpaka matope Hayati.
Kimsingi matope ya Hayati, Yeye hawezi kuwa msafi hata kidogo. Angeendelea kupiga kazi tu, habari za matope apige chini. Yameshatokea tuangalie namna ya kuendelea.
 
Spidi aliyokuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ni challenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani kuifikia baada ya kifo chake

Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.

Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai

Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge

Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.
Kwa wanaoona Mbali utagundua tatizo kubwa ni sheria zetu mbovu, kwani mkaguzi anatumia sheria na ukifuata sheria hakuna hata mradi mmoja utakamilika, kwani zina mlolongo mrefu sana na hapo ndio upigaji mkubwa unatokea pia.
 
Mama ana roho ya ubinadamu,mambo mengi maovu yaliyofanyika chini ya mwendazake yanafichuka,kutokana na ripoti ya CAG.
Mwendazake alikuwa anapambana kuwamaliza wapinzani,wawekezaji huku kukiwa na mianya lukuki ya upotevu wa fedha za umma
Kumbuka unaemuita mama, alikuwa sehemu ya hayo maovu yaliyotendeka, leo anatofautishwaje na mwenda zake.? Anahusika asilimia zote.
 
Spidi aliyokuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ni challenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani kuifikia baada ya kifo chake

Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.

Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai

Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge

Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.
Jamaa umeandika kwa upole sana

Tofauti na tulivyozoea humu jukwaani
 
Back
Top Bottom