dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 22,121
- 49,376
KWA KIFUPI SANA LAKINIMkuu, marehemu ni kabla hajazikwa na akizikwa ni hayati. Kama kuna kamusi nyingine tuhabarishane
Hayati ni neno la kiarabu likimaanisha uhai, kwa hiyo mtu aliyekufa na kuacha Legacy yaani bado kuna vitu alifanya kwa manufaa ya jamii au dunia na bado vinaishi huyu ndiye huitwa hayati kwa maana kafa lakini bado anaishi kutokana na legacy aliyoiacha wala siyo lazima kuwa maarufu au tajiri.
hata Masikini anaweza kuacha Legacy, kwa mfano anaweza kusema ana eneo lake ligeuzwe kujengwa shule au hospitali au kisima au msikiti au kanisa na ikafanyika hivyo huyu ni hayati maana kaacha legacy kile alichokuwa akimiliki pamoja na umasikini wake bado kinaishi na kinainufaisha jamii aliyoiacha.
Mwingine anaweza kufundisha ujuzi vijana na wale vijana wakanufaika na ule ujuzi na ukanufaisha jamii, kwa hiyo elimu yake aliyoitoa bado inaishi na inainufaisha jamii huyu naye ni hayati.
Lakini ukifa na kashfa kibao za ufisadi wa mali, ufisadi wa mapenzi au dhulma au uchawi yaani kifo chako kikaleta nafuu kwa jamii, basi wewe ni marehemu tu huwezi kupewa heshma ya kuitwa hayati.
Kwa hiyo kila mtu ajitathmini kama yeye akifa ataitwa Hayati au Marehemu?
Source: Tofauti kati ya Hayati na Marehemu hii hapa.