Hayati Magufuli aliwezaje kuwadhibiti wahujumu wa maji na umeme?

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
14,100
15,940
Aliposema biashara ya majenereta iwe mwisho na akata kuona mabwawa yote yawe yamejaa maji iwe kiangazi au mvua iwe kipindi cha ukame ,

yote yalitekelezeka ndani ya wiki mpaka siku anafariki mabwawa yote yalikuwa full na ziada ilikuwa inasubiri na wenye mifugo waliendelea kunywesha na bwawa la nyerere lilitegemewa kujazwa maji.

Leo cha kusikitisha ngonjera zimekuwa nyingi na shughuli zisizo na lazima eti waziri anatembelea nyumba kwa nyumba kuangalia maji kama yanatoka,yule mchina aliyechepusha yupo mahabusu gani tukamtembelee au ndio kaole sanaa group.

Yule mwingine eti yupo bize kwenye vyanzo vya umeme wa maji yaani kutuzuga, tusitafute wahujumu uchumi zaidi ya hawa mawaziri wawili Aweso na Makamba yaani wamegeuka wababaishaji wakubwa sana.

JPM alitumia dawa gani dhidi ya hawa wahujumu?
Na mama anashindwa.

Angalizo 2025 haipo mbali hatutosita kuchukua hatua kali!

Tafadhwali mjitathimini Makamba na Aweso kama mnatosha sio blah blah za kisiasa!
 
Hapa ndipo nilipokuja kujifunza sio wote waliomchukia Magufuli walikuwa na sababu za msingi, wengine walimchukia kwa sababu zao binafsi hasa ikizingatiwa awamu ya nne ililea taifa letu kifisadi sana, wakapeleka mazoea hayo kwa Magufuli wakidhani angekuwa mwenzao kumbe hakuwa na habari nao.
 
Hapa ndipo nilipokuja kujifunza sio wote waliomchukia Magufuli walikuwa na sababu za msingi, wengine walimchukia kwa sababu zao binafsi hasa ikizingatiwa awamu ya nne ililea taifa letu kifisadi sana, wakapeleka mazoea hayo kwa Magufuli wakidhani angekuwa mwenzao kumbe hakuwa na habari nao.
Alipokuwa akisema wanaomchukia ni wapiga deals ilionekana kama anajisifia uongo vile. Hana hata mwaka ardhini ila mtashuhudia wenyewe na mtamkumbuka!

Awamu ya nne ilizalisha mafisadi na kuwalea kana kwamba walichokuwa wakikifanya kilikuwa ni sahihi! Ilipotokea jamaa akawa hawapi nafasi ya kuinyonya serikali ndio chuki na matusi na kejeli zilianza kila kona, oh tumepata raisi mshamba haijawahi kutokea 😅 kumbe raisi mshamba ni yule ambaye hashirikiani na wanasiasa kuibia nchi kupitia mikataba ya kinyonyaji😅 RIP Magufuli.

Utagundua chuki kubwa ilikuwa kuzimwa kwa ndoto za mafisadi na wala rushwa kukwamishwa katika michakato yao.
 
Aliposema biashara ya majenereta iwe mwisho na akata kuona mabwawa yote yawe yamejaa maji iwe kiangazi au mvua iwe kipindi cha ukame...
Makamba amejaaliwa kipaji cha kutiririsha maneno na kuyapamba kimashairi, lakini ukifuatilia utakuta hakuna vitendo! Anaongea na ana kuacha pale ulipokuwa unamsikiliza, hupati faida yoyote.

Nafikiri alipotumbuliwa na JPM, kisa cha kutumbuliwa kilikuwa ni hicho. Maneno mengi vitendo sufuri!

Makamba kama ange anza kutenda na matokeo yakaonekana, mbona hata uraisi ungemfaa? Lakini - talk talk no tangible results.
 
Back
Top Bottom