Hayati Magufuli alivyoifilisi familia ya Jamal Malinzi

Muwe mnatumia akili kidogo, uchaguzi wa 2015 ulifanyika tarehe 25 October, na akatangazwa mshindi tarehe 30 October 2015, kwahiyo kutoka November 2015 alipoapishwa JPM hadi June 28 2017, walikuwa wanamuogopa Malinzi wasimkamate?,vitu vingine kama hamna data muwe mnakaa kimya. Malinzi alifanya ufisadi mkubwa sana, kama unabisha waulize ndugu zake, kwanza jiulize ni ndugu gani wa Malinzi mwenye uwezo wa kutoa milioni 847, Ili kumtoa Malinzi ndani huku nyuma akifilisika?,mtaje hapa maana ndugu zake wanafahamika wote.
Ulipendelea akiapishwa tu,Jamal atiwe pingu?Unaonesha uzuzu sana.
 
Uchaguzi wa mwaka 2015 ni miongoni mwa chaguzi ngumu kuwahi kutokea nchini ukiacha ule wa 1995 .
EL alimkaba vilivyo JPM mpaka akakosa usingizi.

Bajeti ya kampeni ya CCM ilipwaya kwa mchaka mchaka ule ikabidi itafutwe njia mbadala ili mamvo yaende.
Wafanyabiashara mbalimbali na taasisi mbalimbali wakaombwa kuchangia na kuahidiwa kurudishiwa pesa zao baada ya uchaguzi.

Kama muujiza shirikisho la mpira nchini TFF likapokea bilioni kadhaa sio nyingi sana ili kuendeleza program za michezo nchini. Vigogo wa chama kubwa wakazinusa,kesho yake mbio mpaka ilala karume zilipo ofisi za TFF ,wimbo ukiwa uleule tuazimeni pesa tutarudisha after uchaguzi. Jamal akagoma akiogopa ma auditor wa FIFA endapo wangetua nchini ghafla wakakuta akaunti haina pesa itakuwaje.

Vigogo wakaondoka mikono.mitupu.
Tarehe 28 june 2017 Nissan Patrol nyeupe inatinga viwanja vya karume wanashuka wanaume wanne wanawatia pingu Jamal Malinzi na katibu wake Mwesigwa Celestine na maofisa wengine wawili wa TFF.

Hawakuliona jua mpaka tarehe 10 dec 2019 miaka miwili na nusu,walishtakiwa kwa uhujumu uchumi,utakatishaji fedha,forgery,matumizi mabaya ya fedha na kutia hasara kuasi cha dola 375,418 sawa na milioni 847 wakati huo.
Uchunguzi ulipofanyika ikaonekana hizo pesa zipo au zilifanya kazi ya TFF ila kulikuwa tu na makosa kidogo ya kiuhasibu,kuna nyaraka hazikukamilika na zilihitaji maelezo ili zikamilike.

Bwana mkubwa hakuelewa hilo akasisitiza plea bargain ,pesa zilipwe.si mlikataa kuchangia kampeni.

Akaunti ya Jama Malinzi ikakutwa na Milioni zisizozidi 100. Celestine Mwesigwa milioni 19 Wale maofisa wawili Nsiande mwaya mhasibu ,na karani Flora kwa pamoja walikutwa na milioni kama tano tu kwenye akaunti.

Jamal akataka kuvimba kama mbwai mbwai tu acha nifungwe, Damu nzito kuliko maji,ndugu zake Jamal walikuwa wanajiweza wakachangishana wakalipa plea bargain ifisi ya DPP.Milioni 847

Kesho yake wakaenda mahakamani akapigwa faini ya shilingi laki tano tu na kuachiwa huru. Milioni 847 sio pesa ndogo,baadhi ya biashara za zimekufa kwa kukosa mtaji na zilizobaki zinayumba. Jiulize wewe na familia yako mtauza nni kupata milioni 800 kumtoa ndugu yenu jela
Taifa linahitaji kuponywa majeraha aisee
 
Nchi kama Tz unahitaji kufinya watu ili nchi inyooke.
Sasa hapo ulikuwa unamfinya malinzi na hao maskini wengine ili kunyoosha Nini hasa? Unfortunately majitu Kama wewe Ni utaishi Miaka mingi ila ningekuwa na namna ya kukupata nakudedisha kiukatili kabisa ili wengine wajifunze..

Hapa Tzn ukiwa tajiri uwe upande wa CCM maana huwa yanakuja tuu Mara tunaomba mafuta sijui mchango wa upuuzi gani kwenye chama na ushenzi wa dizaini hiyo,usipofanya hivyo ndio hayo ya kubambikiwa makesi n.k.

Ili kukomesha ushenzi Kama huu na mtu awe huru na Pesa zake na atimiaje Ni lazima tupate Katiba mpya walau ita guarantee security kiasi fulani..
 
Shetani hajawahi kosa watetezi..

Imagine watu wanapiga 1.5T afu hakuna Cha kuwafanya..

Lakini Kuna wizi mkubwa Sana umefanyika awamu ya Mwendazake Hakuna anayejali..

Kuna jamaa wa usalama ila Ni junior aliniambia hata hizo Pesa alizouliza Mpina kwamba haziko trap Wala trat zaidi ya Til.3 watu walishazila kinyemela na Hakuna Cha kufanya ndio kina Mwigulu wanazunguka zunguka tuu hawana majibu na Bunge kibogoyo badala lizichukue hizo kuwa hoja Wala hawana habari.
 
Jamal akataka kuvimba kama mbwai mbwai tu acha nifungwe, Damu nzito kuliko maji,ndugu zake Jamal walikuwa wanajiweza wakachangishana wakalipa plea bargain ifisi ya DPP.Milioni 847

Kesho yake wakaenda mahakamani akapigwa faini ya shilingi laki tano tu na kuachiwa huru. Milioni 847 sio pesa ndogo,baadhi ya biashara za zimekufa kwa kukosa mtaji na zilizobaki zinayumba. Jiulize wewe na familia yako mtauza nni kupata milioni 800 kumtoa ndugu yenu jela
Duh...!. Japo sina any facts for or against to substantiate the facts of this story, but I seriously doubt the correctness of these facts presented here kwasababu familia ya Malinzi tunaifahamu, milioni 800 ni kama punje tuu ya mchele kwa familia hiyo, ni familia ya wacha Mungu wanao mtanguliza mbele Mungu kwenye kila kitu, hivyo Jamal hakutoka kwa plea bargain, kwasababu ya uadilifu.
Sorry siamini hii story!.

Naendelea kusisitiza JPM hakuwa malaika, ila pia hakuwa shetani kama watu wanavyo mdemonise sasa, naomba niendelee kuwajulisha mahali JPM alipo sasa Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani, msiendelee kuhangaika bure na kujichumia dhambi za bure kumsingizia marehemu.

P
 
Sio kweli. Malinzi alishakula keki yake kwa kuifisidi TFF. Akaambiwa alizochuma zimemtosha, atafute shughuli nyingine ya kufanya, akajiona mwamba. Akakomaa; akagombea kwa kipindi cha pili.
Kilichompata hatokisahau maishani...
Hata kama unayosema ni kweli, bado kuna shida kubwa! Kwanini DPP atumike kama fimbo ya kuchapa usioelewana nao?
 
Back
Top Bottom