Hayati Magufuli alitelekeza SGR ya Tanga-Arusha-Musona ili kupendelea Mwanza na Chato

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,433
49,102
Kabla ya Magufuli kuwa Rais Sgr zilizokuwa zimepangwa kujengwa ni ya Dar Hadi Kigoma Kisha Burundi na Tanga-Arusha Hadi Musoma via Moshi.

Ila kutokana na tabia yake ya visasi, kutojali na upendeleo alihamisha Kipande hicho na kukipeleka Isaka-Mwanza huku alijua fika kabisa hiyo section Haina faida yeyote kiuchumi..

Aidha alitelekeza mradi wa Bandari ya Musoma ambao ndio ungelisha Nchi za Maziwa Makuu badala yake akaweka Nguvu kwenye bandari ya Mwanza na Chato.

Ikumbukwe vizuri ni rahisi Kwa Uganda, Rwanda na South Sudan kutumia Bandari ya Tanga na Musoma Kwa kusafirisha bidhaa Kwa kutumia reli ya Tanga -Musoma kuliko kutumia Bandari ya Dar na Mwanza na Sgr yake kutokana na umbali mkubwa..

Moja ya mambo yule bwana atakumbukwa ni roho ya visasi na kuvuruga uchumi na Mipango bila kujali athari zake kwenye uchumi..

Tanga-Arusha-Musoma ni reli ya Kimkakati Kwa Ajili ya Mizigo ya Nchi za Maziwa Makuu,Utalii, kuwezesha uchimbaji wa magasi soda na kuleta ushindani kwenye bandari ya Mombasa.
 
Kabla ya Magufuli kuwa Rais Sgr zilizokuwa zimepangwa kujengwa ni ya Dar Hadi Kigoma Kisha Burundi na Tanga-Arusha Hadi Musoma via Moshi...
We ni mpumbavu, huko Chato na mikoa yote iliyokua inapita hiyo SGR siyo kwa waTanzania? Ukisema alipendelea kwao, alipopeleka Serikali Dodoma ni kwao? Watu mmejaa upuuzi tu....

Hasira zenu ni za kipumbavu maana mlilazimishwa muache kuibia Serikali Kwa faida ya wananchi wote. Wajinga wakubwa nyie
 
We ni mpumbavu, huko Chato na mikoa yote iliyokua inapita hiyo SGR siyo kwa waTanzania? Ukisema alioendelea kwao, alipopeleka Serikali Dodoma ni kwao? Watu mmejaa upuuzi tu.... Hasira zenu ni za kipumbavu maana mlilazimishwa muache kuibia Serikali Kwa faida ya wananchi wote. Wajinga wakubwa nyie
Mpumbavu ni wewe na huyo mtu wenu.

Sgr ya Tanga-Musoma.via Moshi Ina umuhimu mkubwa kiuchumi kuliko ushuzi mnaofanya Sasa..

Kwanza ni route fupi ya kufikisha amizingo Nchi za Maziwa Makuu kuliko Kuzunguka Dar na ndio maana nusu ya Mizigo ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini inatokea Mombasa Kwa sababu hatuna reli jirani.

Pili Kuna mradi wa magasi soda engaruka inatakiwa reli Ili kusafirsha.

Tatu Sgr hiyo inapita kwenye mbuga za wanayama hivyo ingetumika kwa treni za Utalii

Na mwisho ingeleta ushindani Kwa Bandari ya Mombasa..

Sasa hicho ki Sgr Cha Mwanza kina faida ipi Kwa Nchi ikiwa hata mzigo wa huko ni kiduchu kuliko Kigoma?
 
Thread ya hovyo kabisa, rudi darasani kasome geography uone proximity ya bandari ya Mombasa na hiyo reli unayosema.

Halafu ukasome geopolitics, unafikiri watu wanajenga ili mradi tu unajenga? unaweza kujenga kwako lakini akafaidi jirani yako mnayeshindania soko moja.
 
Kabla ya Magufuli kuwa Rais Sgr zilizokuwa zimepangwa kujengwa ni ya Dar Hadi Kigoma Kisha Burundi na Tanga-Arusha Hadi Musoma via Moshi...
Umesoma geography? SGR iende Tanga na Arusha? Hahahahaha kwa faida gani? 😂😂😂😂😂
 
Thread ya hovyo kabisa, rudi darasani kasome geography uone proximity ya bandari ya Mombasa na hiyo reli unayosema. Halafu ukasome geopolitics, unafikiri watu wanajenga ili mradi tu unajenga? unaweza kujenga kwako lakini akafaidi jirani yako mnayeshindania soko moja.
Huna hoja proximity gani unayoisungumzia?

Hata bila kuwa prof ,kutoka Musoma Hadi Jinja na Kisumu ni jirani kuliko Kupitia Mwanza .

Sgr ya Tanga-Musoma Ina kazi za kufanya ikiwemo kubeba Madini ya magadi soda,kutumika kwenye Utalii na pia inapitia Miji ya viwanda kama Arusha na Moshi.

Mwisho badala ya Kanda ya Kaskazini kutegemea Mombasa port Sasa inhetegemea Bandari ya Tanga iliyounganishwa na reli..

Hiyo ya kwenu huko Mwanza Ina kipi Cha maana itafanya?
 
Reli ya Tanga Moshi Arusha Musoma ina mgogoro wa kuathiri vivutio vya utalii vilivyoko ukanda wa kaskazini.

Suala hilo ni sawa na zile njama za kutaka kupitisha barabara kubwa ya lami ktk mbuga ya Serengeti.
Wewe hakuna vivutio vitaathirika,hizo hadithi zako ni sawa na za bwawa la Nyerere.

Reli itakuwa fenced all over labda during construction lakini Hadi Sasa Barabara inajengwa huko kutokea Mto wa Mbu..

Badala ya kuathiri vivutio itatumika Kwa treni za kitalii mbugani pia.
 
Hebu tuliza akili na tafakari. Reli ikipita Arusha kwenda Musoma na ikipita morogoro,dodoma,singinda, igunga, Shinyanga, Mwanza, Musoma ni wapi itahudumia watanzania wengi?

Ikitoka Arusha kuna miji mingapi itapita ukifananisha na huko unakoponda?

Kwanza reli haipiti chato.

Fikiria vizuri...naona chembechembe za chuki
 
Kabla ya Magufuli kuwa Rais Sgr zilizokuwa zimepangwa kujengwa ni ya Dar Hadi Kigoma Kisha Burundi na Tanga-Arusha Hadi Musoma via Moshi.

Ila kutokana na tabia yake ya visasi,kutojali na upendeleo alihamisha Kipande hicho na kukipeleka Isaka-Mwanza huku alijua fika kabisa hiyo section Haina faida yeyote kiuchumi..

Aidha alitelekeza mradi wa Bandari ya Musoma ambao ndio ungelisha Nchi za Maziwa Makuu badala yake akaweka Nguvu kwenye bandari ya Mwanza na Chato.

Ikumbukwe vizuri ni rahisi Kwa Uganda,Rwanda na South Sudan kutumia Bandari ya Tanga na Musoma Kwa kusafirisha bidhaa Kwa kutumia reli ya Tanga -Musoma kuliko kutumia Bandari ya Dar na Mwanza na Sgr yake kutokana na umbali mkubwa..

Moja ya mambo yule bwana atakumbukwa ni roho ya visasi na kuvuruga uchumi na Mipango bila kujali athari zake kwenye uchumi..

Tanga-Arusha-Musoma ni reli ya Kimkakati Kwa Ajili ya Mizigo ya Nchi za Maziwa Makuu,Utalii, kuwezesha uchimbaji wa magasi soda na kuleta ushindani kwenye bandari ya Mombasa.
 
Back
Top Bottom