Hayati Magufuli alikuwa sawa kwenye suala la covid19. Makampuni yaliyotengeneza vipimo vya covid19 yashitakiwa kwa kuwa vipimo vina kasoro

Huu ugonjwa tunaambiwa wanaougua na kupona ni wengi kuliko wanaokufa, unajua tatizo mkuu ni kwamba huyo Magufuli anaonekana ubishi wake kwenye corona ndio umefanya hadi nae aje kupata corona na ikamuondoa hivi ndivyo ambavyo hata wewe una mtazamo huo, sasa ndio wengine tunaposhangaa kuwa mbona huyo alichanjwa chanjo ya corona kwa hivyo yupo salama sasa huku kuonekana kafa kwa ubishi wake kunatoka wapi?
Hapa jukwaani, kunawatu unaweza kuwasikiliza na usiwaelewe wanasimamia msimamo upi. Tatizo letu nikwamba tumejawa na usiasa+chuki binafsi kwa kiasi kikubwa ndio maana inafika mahara mtu anashindwa kuwa na msimamo thabiti juu ya jambo fulani na kulielezea kwa upana watu wakaelewa.
Unaambiwa mtu alipata chanjo, wakati huohuo kafa kwa corona, wakati huohuo chanjo inahitaji sio chini ya muda wa miaka saba ili iweze kuwa efficiency na hapa ndio kwanza tupo mwaka wa pili tangu ugonjwa ulipuke.

Mimi nadhani tukubari wazi kuwa njia alizokuwa anatumia JPM kwa namna moja ama nyengine zilikuwa sawa kwa style yake sababu, hakuna mahara ambapo imethibishwa chanjo sahihi ambayo inaouwezo wakupambana na huu ugonjwa effective.
 
Back
Top Bottom