omtiti
JF-Expert Member
- Jun 19, 2019
- 1,022
- 1,590
Bado mnateseka ,Maku za mama zenu ,na badoJPM aliamini kuwa yeye ana akili kuliko watanzania wote na ndo maana hata alipo danganywa kwa sifa za uongo Kama sio kumkebehi kuwa anajua idadi ya samaki wote , kwenye mito, ziwani, na baharini alibaki kukenua kwa kicheko.
Mtawala anapenda sifa usipo msifu una geuka kuwa adui wake mkubwa.
Mtawala ana amini katika mabavu hataki mijadala katika kufikia maamuzi.
Mtawala ana amini kuwa dawa pekee ya kubaki katika maamuzi yake ya kibabe ni kuwaondoa wote wenye mawazo kinzani na yake, Kama sio kwa kuwafunga jela, Basi ni kwa mauwaji.
Awamu ya tano ndio awamu iliongoza kwa kuwapoteza watanzania wengi walio kuwa na mawzo tofauti na ya mtawala.
Mtawala hata akikaa uchi usimwambie na ukthubutu atakwambia kwanini una mchunguza chunguza wakati nguo aliyo vaa inampendeza, ataamuru ukamatwe.
Kuna wakati mbunge mmoja na mmbobezi katika siasa za nchi hii , alizungumzia kuwa kitendo Cha Paulo kuvamia ofisi za Cloud media tena kwa mtutu wa bunduki si sawa aliambulia kufukuzwa uwaziri.
Huyo huyo mbunge alipotoa ushauri kuhusu nchi kuwa na miradi mikubwa sio kosa isipokuwa Basi iwekewe kipaumbele yaani ichukuliwe michache michache ili kulinda uchumi wa nchi, alitishiwa hata kufukuzwa ndani ya chama.
Kwa ujumla kiongozi ni yule anaye amini katika kushirikiana katika maamuzi ya pamoja.
Na Kama awamu yatano ingefanikiwa kukaa miaka yote kumi hakika ni kwamba vazi rasmi la Taifa lingekuwa ni kaniki.
Tumshukuru Mungu kwa kutuhurmia watanzania.