Hayati Magufuli alikuwa mtawala na siyo kiongozi

Mukua

Senior Member
Sep 30, 2021
138
250
Hayati Magufuli aliamini kuwa yeye ana akili kuliko watanzania wote na ndio maana hata alipodanganywa kwa sifa za uongo Kama sio kumkebehi kuwa anajua idadi ya samaki wote kwenye mito, ziwani, na baharini alibaki kukenua kwa kicheko.

Mtawala anapenda sifa usipo msifu una geuka kuwa adui wake mkubwa. Mtawala ana amini katika mabavu hataki mijadala katika kufikia maamuzi. Mtawala ana amini kuwa dawa pekee ya kubaki katika maamuzi yake ya kibabe ni kuwaondoa wote wenye mawazo kinzani na yake, Kama sio kwa kuwafunga jela, Basi ni kwa mauwaji.

Awamu ya tano ndio awamu iliongoza kwa kuwapoteza watanzania wengi walio kuwa na mawazo tofauti na ya mtawala.

Mtawala hata akikaa uchi usimwambie na ukthubutu atakwambia kwanini una mchunguza chunguza wakati nguo aliyovaa inampendeza, ataamuru ukamatwe.

Kuna wakati mbunge mmoja na mbobezi katika siasa za nchi hii, alizungumzia kuwa kitendo Cha Paulo kuvamia ofisi za Cloud media tena kwa mtutu wa bunduki si sawa aliambulia kufukuzwa uwaziri.

Huyo huyo mbunge alipotoa ushauri kuhusu nchi kuwa na miradi mikubwa sio kosa isipokuwa Basi iwekewe kipaumbele yaani ichukuliwe michache michache ili kulinda uchumi wa nchi, alitishiwa hata kufukuzwa ndani ya chama.

Kwa ujumla kiongozi ni yule anaye amini katika kushirikiana katika maamuzi ya pamoja. Na Kama awamu ya tano ingefanikiwa kukaa miaka yote kumi hakika ni kwamba vazi rasmi la Taifa lingekuwa ni kaniki.
 

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
895
1,000
Meza hiyo hata Kama ni chungu.
Wewe tunakuona humu! Unajua unapokaa unamzungumzia Maguguli inamaanisha alikushika pabaya na mataahira wenzako! Ndo maana kashakufa bado unamzungumzia hapa! Leta basi hata maada za mama.

Samia au maendeleo unazungumzia mtu ambaye hayupo na wala hatakuwepo tena! Ndo maana unaomekana mpumbavu usiyejitambua!
 

Manton

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,139
2,000
"Ukikuta mtu anamsimanga marehemu, hayati, au maiti ujue utu wa huyo msengenyaji, msimangaji, ulisha kufa zamani za kale,yaani kitambo, huyo ni msukule huru,ulioachwa uraini uendelea kuvunda taratibu mbele ya ubani." Hivi huyo uliye mwandika hivyo angekuwa ndugu yako, au mwanao ndo kaandikwa hivyo ungejichukuliaje, nafsi mwako?
 

Mukua

Senior Member
Sep 30, 2021
138
250
Wewe tunakuona humu! Unajua unapokaa unamzungumzia Maguguli inamaanisha alikushika pabaya na mataahira wenzako! Ndo maana kashakufa bado unamzungumzia hapa! Leta basi hata maada za mama Samia au maendeleo unazungumzia mtu ambaye hayupo na wala hatakuwepo tena! Ndo maana unaomekana mpumbavu usiyejitambua!
Babu yako amewatesa na kafanya mauwaji mengi lazima kumbukumbu zake ziwekwe wazi huyo nduli.
 

Mukua

Senior Member
Sep 30, 2021
138
250
"Ukikuta mtu anamsimanga marehemu, hayati, au maiti ujue utu wa huyo msengenyaji, msimangaji, ulisha kufa zamani za kale,yaani kitambo, huyo ni msukule huru,ulioachwa uraini uendelea kuvunda taratibu mbele ya ubani." Hivi huyo uliye mwandika hivyo angekuwa ndugu yako, au mwanao ndo kaandikwa hivyo ungejichukuliaje, nafsi mwako?
Lazima ikuguse.ulidhani atadumu, na Kama angesifiwa unge kenua meza hiyo .
 

Murashani GALACTICO

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
986
1,000
Tozonia kuna watawala wengi tuu halikadhalika kuna viongozi wengi sana ila sijaona mwakilishi hata mmoja. Sauti na maslahi ya wanyonge haijawasilishwa au kuwakilishwa ipasavyo. Hatuna wawakilishi tusijidanganye. Viongozi wetu wachumia tumbo. Nilipata kupiga story na mmoja wa waandamizi toka shirika la UN akaniambia Africa tunawapa misaada sana ila viongozi wenu ni WAPIGAJI sana kuliko maelezo maana misaada ya kifedha ikifika kwenye nchi zenu hawa viongozi wenu account zao zolizopo ulaya na america zinajaa kwa kasi sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom