tony92
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 2,387
- 3,634
Haya majuisi ya malimao na tangawizi yamesababisha vidonda vya tumbo kwa wanannchiTangu kuzuka kwa Corona nchini China mwaka 2019, mataifa mengi duniani yaliamua kuja na mbinu za kupambana na Corona kwa kufungia watu ndani(lockdown) kuvaa barakoa, social distance na mengine mengi ikiwemo Chanjo.
Tanzania tuliamua kuishi na Corona kwa kukataa kujifungia (lockdown) na shughuli ziliendelea kama kawaida na watu wakisafiri huku na huko, hata watalii kipindi cha Corona walikuwa wengi sana Tanzania.
Baada ya miaka miwili kupita tangu Corona izuke mataifa yaliyoongoza kwa vifo ni Marekani, China, India Brazil etc hayo mataifa ni tajiri yana mitungi ya oxygen mingi ,wana barakoa, na walijifungia.
Tanzania chini ya hayati rais Magufuli tuliamua kutumia njia za asili kama kunywa juice ya Tangawizi na malimao, kupiga nyungu na kumtanguliza Mungu mbele etc na matokeo yake impact ya Corona ni ndogo sana na tuliweza kuingia uchumi wa kati.
Cha kusikitisha baada ya miaka 2 ya Corona kupita ,tume iloyoundwa na rais Samia Suluhu licha ya hiyo kamati kujaa maprofesa wa afya inataka kutuaminisha kwamba watanzania si lolote si chochote na tunatakiwa tujifunze kwa waliofanya lockdown huko nchi za nje.!!!
Lakini ukweli ni kwamba ukipima impact ya Corona Tanzania inaonyesha tumefanikiwa sana na tulitakiwa tujivunie haya mafanikio hadharani na kuitaka dunia ije ijifunze Tanzania mbinu tulizotumia.
Hivi sisi watanzania nani aliyeturoga? Pamoja na ushahidi wote uliotuzunguka ukionyesha tumefaulu vita ya Corona bado maprofesa wetu wanataka tufanye kama walivyofanya India, Marekani, Rwanda?
Na Chadema nao wanashqngilia?