Hayati Edward Sokoine, Waziri Mkuu aliyekufa huku akiacha mashati matatu na viatu ‘pea’ 2 tu

wewe umerud tena africa? zanzibar sasa tunatawa wenyewe
Kuacha mashati matatu na viatu ‘pea’ 2 tu ndio kipimo cha uongozi bora? Karume kafa kaacha magorofa kwa ajili ya malofa na walalahoi Zanzibar nzima! Yupi bora? Toka lini mmasai na Mashati?
 
Huyu Sokoine alikuwa mtu wa pekee. Yaliyoandikwa ni machache. Nadhani hulka yake ni ile ambayo mtu hawezi kujifunza au kuiga, inatakiwa uzaliwe nayo, na Mungu awe amekuumba hivyo.

Nakumbuka siku ile ya kifo chake, tulikuwa darasani, ikatokea minong'ono kuwa Sokoine amefariki, hakuna mwanafunzi aliyebaki darasani, na hakuna mwalimu aliyeuliza kwa nini wanafunzi tunatoka madarasani bila ya kuruhusiwa na walimu maana nao nadhani walichanganyikiwa. Nilikuwa Njombe sekondari, na mwezi ule aliofariki ndiyo mwezi ambao Sokoine alifika Njombe akitokea Songea.

Mwaka ule kulikuwa na upungufu mkubwa wa chakula kwa maeneo mengi ya nchi. Wakati kule Dodoma watu walikuwa wanakufa kwa njaa, Songea mahindi yalikuwa yanaoza kwa sababu hakuna malori ya kuyasafirisha mahindi kupeleka maeneo yenye njaa.

Siku ambayo Sokoine alikuwa akitoka Songea, wote tulikuwa Njombe mjini tukisubiri kumpokea Sokoine na kisha tuisikilize hotuba yake lakini tulipungiwa tu mkono, tukaambiwa kuwa hatahutubia, alikataa hata kula chakula, alikunywa tu maziwa, akaenda Makambako. Kule Makambako malori yote yaliyokuwa yametoka kuteremsha shaba ya Zambia, yaliyokuwa yakielekea Zambia yalielekezwa kwenda Songea kuchukua mahindi na kuyateremsha Makambako, zoezi hilo kwa siku ya kwanza alilisimamia yeye mwenyewe. Baada ya wiki 2 mahindi Songea yakawa yamekwisha. Wakati watu wa Njombe, Makambako na Songea wakiwa bado wanakumbuka tendo hilo, mara tukasikia Sokoine amefariki! Hakuna ambaye hakusikitika. Na matangazo ya siku ile, na ule wimbo wa, 'Edward Sokoine x3 Kwa heri hatutausahau kamwe.

Sokoine alikuwa na wake wawili, japo tunaambiwa alikubali kwa sababu alichokuwa amefanyiwa ilikuwa ni heshima kubwa kwa Wamasai. Baada ya kuoa mke wake wa kwanza, wakwe baada ya kuridhika sana na tabia ya mkwe wao, ukoo wa mke wa kwanza walikaa chini na kujadili ni zawadi gani ya kumpa mkwe wao ambaye matendo yake yamewafurahisha, wakaamua kumpa binti mwingine kutoka kwenye ukoo wao.

Lakini pia wakati ule wa maziko ilielezwa kuwa kuna wakati Sokoine alitaka kuwaacha wake zake wote wawili ili awe padre wa Kanisa Katoliki. Ili hilo liweze kufanyika kwa mtu aliyekwishaoa alitakiwa apate ridhaa ya wake zake, hasa yule mke wake wa ndoa. Wake zake hawakuridhia.

Inaelezwa kuwa kuna matukio mawili tu yaliwahi kumtoa Mwalimu machozi, kifo cha Sokoine na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM walipoonesha kutoukubali uteuzi wa Rashid Kawawa kuwa Katibu Mkuu wa Chama. Japo hakusema wazi, lakini inaonekana, hakuna mtu ambaye Mwalimu alimwamini kama Sokoine.

Kitu ambacho sifahamu mpaka leo, kifo cha Sokoine ilikuwa ni ajali ya kawaida au ya kupangwa? Siku ya kifo chake, tulielezwa kuwa Mwalimu alimpigia simu Sokoine kuwa asisafiri kwa gari, asafiri kwa ndege. Je, kuna taarifa zozote ambazo Mwalimu alikuwa nazo? Au ni zile hisia tu ambazo binadamu unaweza kuwa nazo wakati fulani ambapo jambo baya linapotarajiwa kutokea?

Kazi ya Mungu haihojiwi na binadamu yeyote, tena tunaambiwa kuwa maisha ya binadamu aliyezaliwa na mwanamke ni mafupi sana, lakini Sokoine alifariki mapema mno! Mungu Mwenye Rehema amjalie pumziko la milele na pale alipomkosea Mungu wake basi apate msamaha kutokana na yale mema aliyoyafikiria na kuwatendea wanadamu wenzake.
A true leader ànd a true distinguished son of TZ ànd Africa with no selfish ambitions and personal gàins but to him TÀNZANIA and it's PEOPLE came first and foremost!he worked very hard to solve wananchi problems and not for himself,family and friends he sacrifriced everything he can for the betterment of the country and that's despite being popular and loved by wananchi he died very poor,may our almighty GOOD LORD keep resting this national heroe's soul in Eternal peace!
 
Back
Top Bottom