Tukiwa tunaelekea kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya Kifo cha Aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine aliyefariki April 12 mwaka 1984 kilichotokana na ajali ya Gari eneo la Dakawa Morogoro akitokea mkoani Dodoma, ninakuleta baadhi ya Nukuu bora kabisa kutoka kwake ambazo aliwahi kuzisema.
*Nukuu bora kabisa za Hayati Edward Sokoine*
“Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” – Sokoine, 26 Machi 1983
“Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa” – Sokoine, 4 Oktoba 1983
“Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, ‘mali hii umeipata wapi?'” – Sokoine, 23 Oktoba 1983
"Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam katika Serikali na mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Sokoine, 23 Oktoba 1982.
"Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na being ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi I'll bei yenyewe iweze kujirekebisha" - Sokoine, 24 Septemba 1983
Hakika, Watanzania na Taifa kwa ujumla watakukumbuka daima. Pumzika kwa amani Mzalendo, shujaa na mchapa kazi Edward Sokoine.
Sent using Jamii Forums mobile app