Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 10,526
- 13,013
Kamfufue uzikwe weweHabari wanaJamiiForums
Natumaini ni wazima wa afya binafsi nilikuwa naumwa Sana angalau sasa hiv nina unafuu nilikuwa nina Malaria tuombeane nipone kabisa.Tuje kwenye mada husika hapo juu unajua nimekuwa mfuatiaji kiasi fulani wa jukwaa Hili nimegundua kuwa members wa jukwaa hili hawana tofauti na ushabiki wa Simba na Yanga au Teams zile ambazo zipo mitandaoni sijui Team diamond,Team kiba n.k tunachukulia siasa kama ushabiki badala ya kuchukulia kama maisha.
Kupitia siasa nchi ndio inajengwa watu wamekuwa wakiabudu viongozi as if ni Mungu wakiwasapoti hata kama wanakuosea hapo unajiuliza hawa wanatofauti ipi na Team diamond au Team kiba? Wanaushabiki wa vyama as if hivyo vyama vinawasaidia kuondoa umasikini wa maisha yao wamefanywa mandondocha na wanajiona ok yaani Unaweza kukuta mshabiki wa Chadema anamshambulia shabiki wa CCM analipwa kutetea ujinga lakini na yeye mwenyewe anafanya kile kile anachofanya mwenzake.
Nije kwenye lengo kuu la uzi wangu kiukweli kutokana na hii nchi ilivyo mtu kama Magufuli ndio mtu pekee ambaye alituonesha uelekeo mzuri wa kutupeleka mbali. Hii nchi kuna baadhi ya mnatatizo yanazalishwa na watu kwa lengo lakupiga pesa na kama hakuna strong President ambaye ni mzuri kwenye ufuatiliaji kupigwa kuzidi kutaendelea, Mfano mzuri tangu aingie Magufuli madarakani hakujawi kuwa na shida ya maji kama ilivyo sasa hiv huku kwetu Kimara hii inaenda siku ya 5 maji hayatoki Waziri husika uko alipo anafanya Nini wanawanchi wanateseka jitu limekaa linakula kiyoyozi watu wa aina hii wakitumbuliwa baadhi ya watu especially wenye itikadi ya vyama wanasema Magufuli ana roho mbaya wakati hata yanatokea Mama samia anazurura nchi za nje.
Umeme sasa umekuwa unatikatika tofauti na kipindi Cha Magufuli kama unakumbukumbu vizuri Magufuli kama ajaingia madarakani wakati wa kampeni aliwapiga beat Tanesco na kweli tangu aingie ukusikia hata ile kasumba ya maji ya kidatu yamepungua.
Magufuli kakuta nchi ambayo nchi jirani zinachukua rasimali zetu ovyo ovyo Mara unasikia twigs kapandishwa ndege n.k lakini mwamba tangu aingie kuna wachina wameukumiwa vifungo virefu, mambo ya kutoroshwa mali asili kazibiti.
Kiufupi hii nchi Magufuli aliichukua likiwa imeoza na ndio maana akawa anajenga misingi we jiulize mtu kafariki muda mrefu still anapokea mshahara ndio maana akaanzisha kampeni ya kushafisha mafanyakazi hewa.
Kuna miradi Mingi hapo awali inachukua muda mrefu kukamilika ingawa haikustahili ifike huko ni kwasababu viongozi wetu hawakuwa wasimamizi tofauti na Magufuli ndio maana umeona chini yake flyover imekamilika kwa wakati madaraja mengi yamekamilika kwa wakati kwasababu hakiona mkandarasi haendi sambamba na kasi ya mradi anamfukuza hii imesaidia sana.
NB: Tanzania ina muhitaji mtu kama Magufuli ili ipige maendeleo tofauti na hapo nchi itakuwa unarudi nyuma kwa mambo mengi sana.