Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Enzi za utawala wake Wasiojulikana walishika chati, watu wengi walipotea, wengi waliuawa, possible ameenda ili hivyo vitendo visiendelee.
Wasiojulikana hata yeye JPM alikuwa anawasikia,hakujua wanatoka wapi,kaondoka kawaacha,Sasa hivi wanakula nchi,kigogo kasema anarudi kuungana nao.
 
Aliyemtuma Kingai na Mahita kumuua na kumtupa mozes lijenje ndio unayemtetea hapa? Aliye amuru mateso kwa makomandoo Adamoo na Lingwenya ndio unamsemea hapa? Tuache bhana tunajua kushughulika na wasaliti
Hizo zote sanaa tu. Una hakika Moses Lijenje kafa?
 
Kuna baadhi uliyoyasema ni ya kweli tupu, mengine hapana.

Kwa sisi tuliowaumini, kwa ufupi tunajua kuwa:

1) Maisha ya mwanadamu hupangwa na Mungu

2) Kiongpzi awe mbaya au mzuri, Mungu atakuwa ameruhusu, na mara nyingi kwa makusudi fulani

3) Kifo ni kwaajili ya kila mmoja

4) Kifo hakichagui umri

Ambayo hukuyasema:

1) Magufuli alikuwa ni mtawala mbaya sana. Kwa matendo ya kuua, kuteka na kubambikizia watu kesi, alijiweka karibu zaidi na upande ulio kinyume na Muumba wetu aliyetukataza sisi sote kuyatenda hayo aliyokuwa akiyatenda.

2) Mungu huweza kuruhusu hata mtu mbaya kuwa mtawala kwa makusudi yake. Mungu hashindwi kitu. Hachelewi wala hakawii bali hutenda kila jambo kwa wakati ufaao kwa kadiri ya hekima yake. Aliruhusu Yuda awe miongoni mwa wafuasi wa Yesu. Aliruhusu Herode ambaye aliua watoto wote wa kiume ambao umri wao ulikaribiana na umri wa Yesu, kuwa mtawala. Anaruhusu hata majambazi na wauaji waendelee kuishi, lakini haimaanishi kuwa wanampendeza. Bali huruhusu wawepo kwa makusudi maalum. Kuna wakati, mtawala mbaya huja kama adhabu kwa wanaoongozwa kwa sababu wamemsahau Mungu wa kweli. Au kutaka kudhihirisha ukuu wake na jinsi hekima yake ilivyo tofauti na ya mwanadamu. Aliruhusu Hitler na Musollini wawe watawala. **** wakati aliruhusu Taifa lake teule kuingia utumwani, na wakati mwingine kulitoa utumwani kwa mkono wake wenye nguvu.

3) Kifo hakiondoi haki ya watu kukusema iwe kwa mema au mabaya. Matendo mema au mabaya ni shule kwa sisi tunaoendelea kuishi. Ndiyoaana Yida anaendelea kusemwa mpaka leo. Herode anasemwa. Hitler anasemwa. musolini anasemwa.

4) Japo sisi sote mwisho wa maisha yetu hapa Duniani ni kifo, lakini ukweli kifo kilikuja kwetu wanadamu kama adhabu, siyo kama zawadi.7 Na hata kwa hekima ya mwanadamu, adhabu ya kifo ndiyo kubwa kuliko zote (japo mimi sioni kama kifo chenyewe ni adhabu ambayo mwanadamu anaweza kumpa mwanadamu mwenzake). Lakini Kristo alikibadilisha kifo kutoka kuwa adhabu na kuwa ndiyo njia ya kumwendea Mungu aliyetuumba ili tukatoe hesabu ya matendo yetu tulipoishi Duniani. "Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi. Lakini, kama kwa kuishi nitaweza kufanya kazi yenye faida zaidi, basi, sijui nichague lipi! Nakabiliwa na haya mawili yaliyo sawa. - Paulo"

5) Funzo tulilolipata kutokana na kifo cha huyu mwenzetu aliyekuwa na mamlaka makubwa ya kibinadamu ni kuwa hata ukiwa na cheo kikubwa kiasi gani, hata uwe na majeshi yenye nguvu kiasi gani, hata uwatishe wanadamu wenzako kiasi gani, bado wewe ni mwanadamu ambaye kuzaliwa kwako na kufa kwako hakuna tofauti ni mwingine yeyote, tuheshimu utu, uhai, haki na heshima ya wanadamu wenzetu. Tutambue pia, maisha yetu Duniani ni ya muda tu, kama huyu aliyeogopwa na akamtisha kila raia kutokana na utawala wake wa mkono wa chumaj, akalindwa kwa majeshi ya wazi na ya siri, mwenye uwezo wa kupata matibabu popote kwa gharama yoyote, ameondoka, sisi tuliobakia tuna nini cha pekee hata tuone tuna uwezo wa kuwadhulumu wanadamu wenzetu kwa vile tu pengine tuna mamlaka fulani, utajiri, n.k?

6) Tumgeukie Mungu, tumshukuru kwaajili ya maisha ya huyo mwenzetu maana kwa kupitia maisha ya huyo mwenzetu, tumejifunza mengi, meme na mabaya. Mabaya yake, yawe onyo kwetu, na mazuri yake tuyaishi.
Dah! Umejibu vzr sana aisee mungu akubariki
 
Ila kuna kitu ktk maandiko umekisahau.
" MTU MWEMA AKIFA DUNIA HUOMBOLEZA LKN MUOVU AKIFA NI FURAHA KWA ULIMWENGU"
 
Back
Top Bottom