Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,684
- 36,045
Tuliyasema haya wakati akiwa hai na tutayasema wakati huu ambao hatunaye.
Kwanza Wamachinga hawakuzi uchumi wa nchi hii kwa kiwango kikubwa bali wanaukuza uchumi wa China, India na Thailand maana huko ndiko zitokazo bidhaa wanazouza.
Serikali ya Magufuli iliwatumia wanyonge kama mtaji wake mkuu wa kufukia mashimo yake ya kisiasa.
Huwezi mtu kumwacha achafue mji eti kisa mnyonge asibughuziwe.
Aliyejenga Machinga complex nadhani ni Kikwete huyo ndiye unaweza kusema kuwa ana harufu ya huruma kwa wamachinga.
Dar es salaam ina wilaya tano kama sikosei. Kila wilaya ingepata soko la wamachinga lililojengwa kisasa na kugawa vizimba kwa wamachinga hiyo ndio huruma kwa wamachinga.
Kariakoo ingebaki na maduka ya Jumla tu.
Mji ungenoga, wananchi wangerahisishiwa huduma.
Mtu aweke banda lake kwenye mtaro umwache tu kisa mnyonge. No.