Hayati Dkt. Magufuli aliligeuza suala la Wamachinga kuwa mtaji wake wa kisiasa

Mukua

Senior Member
Sep 30, 2021
156
202
Ikumbukwe kuwa wakati wa utawala wake alijaribu sana kucheza na akili za watu, hasa akitumbukiza neno la Watanzania wanyonge.

Ni yeye huyu huyu alitoa amri kuwa wamachinga watafutiwe maeneo maalum ya kufanyia biashara zao, na ukweli ni kwamba zoezi hilo lilianza na kukatokea mtafaruku mkubwa sana kati ya wale walio lisimamia Hilo zoezi na wamachinga wenyewe.

Na alipogundua kuwa amefeli kwa hilo, akaja na sera yake ya kisiasa kuwa hao watu wasibughudhiwe kwani ndio walio mpatia kura nyingi kwenye uchaguzi, (na kuna clip ili tembea sana mitandaoni akiwa anaongea huyu huyu mama Samia juu ya hao wamachinga kwamba ndio waliowapa kura) bila ya wao kujua kuwa alikuwa ana waanda kwa uchaguzi unao fuata kwani alishaona, na Kama sio kuwa na mashaka kuwa atashindwa kwenye uchaguzi huo.

Kiujumla alishindwa kwenye zoezi la kuwaondoa wamachinga.

Mama na Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan amefaulu kwa hilo, miji imekuwa misafi na wafanya biashara walio tii na kuelekwa kwenye maeneo elekezi wanaendelea na biashara zao bila bughudha.

Haya ni mafanikio kwa Serikali ya awamu ya sita. Ambayo serikali ya awamu ya tano ilishindwa kuyafikia.

HONGERA AWAMU YA SITA KAZI IENDELEE
 
Ulianza vizuri nikakupa na like lakini nimeitoa (Haya ni mafanikio kwa Serikali ya awamu ya sita. Ambayo serikali ya awamu ya tano ilishindwa kuyafikia.)
 
Ule ulikuwa ulimbukeni mkubwa, nguvu kazi ilipungua Sana, kijana akipata 50,000 , biashara Chinga!
Viongozi wafikirie kukuza uchumi kuongeza tija uzalishaji, sio mtawanyo huduma na bidhaa.

Taifa la kichinga, vibaka na wadangaji hatuwezi kupiga hatua.

Kuaminisha vijana maisha Ni mepesi Sana,kuishi geto, kubet, hata Bei dada poa ilishuka 1000 Tzs.
 
Ulianza vizuri nikakupa na like lakini nimeitoa (Haya ni mafanikio kwa Serikali ya awamu ya sita. Ambayo serikali ya awamu ya tano ilishindwa kuyafikia.)
Asante kwa kuona hayo mapungufu, na ndivyo mijadala inavyo takiwa kuwa, ndugu Babati.
 
Serikali inarusha peremende masikini mnakanyagana na kusongana kuipigania,yenyewe inakaa kutazama.

Mleta mada huwenda huna kazi, au una kikazi cha kuunga unga, au jobless mtarajiwa, ila umefungiwa ktk kuta za unafiki kujifanya nawewe ni toplayer.

Machinga ni shemeji zako, wajomba zako,baba zako wadogo, jirani zako, watoto wa mfanyakazi mwenzako nk.

Una ungana na wapumbavu wengine wanaoamini CCM inaiba kura, lakini huwa inatoa hongo ili ipigiwe kura pia,na kurubuni watu kama machinga, sijui ili iweje wakati inaweza kujiibia kura tu inavyotaka ktk sanduku!

Kamsikilize JPM alipokuwa akiongea ikulu juu ya machinga na bi samia akiwepo, ndio utajua kauli yake haikuwa na mzaha wala upuuzi ulioandika hapa.
 
Ukweli lazima usemwe kiongozi, Johnthebaptist, kwani Hilo wewe haukuliona kweli?
Wamachinga waliletwa na CHADEMA wakati wameshika majimbo ya Dar es salaam wakisaidiwa na mzee Lowassa.

Nia ya CHADEMA ilikuwa ni nzuri tu maana ililenga kujenga utu pasipo ajira!
 
Kesho utakuja kufungua uzi wenye kichwa cha habari "Mjiajiri" ndiyo unafiki wenu
 
Ule ulikuwa ulimbukeni mkubwa, nguvu kazi ilipungua Sana, kijana akipata 50,000, biashara Chinga!

Viongozi wafikirie kukuza uchumi kuongeza tija uzalishaji, sio mtawanyo huduma na bidhaa.

Taifa la kichinga, vibaka na wadangaji hatuwezi kupiga hatua.
Nguvu kazi ipi iliyopungua?
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom