Hayati Dkt. John Pombe Magufuli hakuwa mnafiki

simon2016

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
593
1,669
Nimeshangaa sana kwa msimamo wa mama na team nzima ilivyobadili gia angani.

Sawa Hayati hakugusa maisha ya kila mtu na alisema hajaja kuuza sura, kama mbovu iwe mbovu kama hukua upande wake basi ilikua imeishaa hio ndio ilikua kero yake hakua na sehemu ya kuingilika.

Hakuwa mnafiki kwa sababu aliwasema watu wakiwa hai na walimsikia na wakasema asijimwamba fai.

Kama kulikuwa na madudu waliogopa nini kusema wakati alizindua bunge akasema kosoeni semeni msiwe watu wa ndio. Nape na msukuma walijitoa. Ni mbunge mmoja alisema kuhusu corona na yupo mpaka leo hakufanywa kitu. Mzee alifika morogoro akaanza kupita sokoni kama research yake ili kuandaa mpango wa kusululisha tatizo la wafanyabiashara.

Mzee alikua na ubabe tu ila lengo lake lilikua zuri. Alitembea na gari njiani ili asikilize kero za watu na kero ya maji ilimuumiza sana alikua ametoa na nafasi za kujitolea miezi sita na baadae watu wata ajiliwa moja kwa moja ndani ya nchi nzima na walihitajika graduates walio mtaani kwa miaka miwili mpaka wale fresh from university ukichana na swala la madini alilo likabili vizuri.

Mzee kaacha legacy ya kuwafanya viongozi kusikiliza watu wao haraka na Raisi kuweza kupambana na wanyonyaji.

Mzee kaifanya TTCL imekua murua 4G yake ni hatari na nusu.

Mzee alionyesha mwelekeo wa nchi na Africa iweje haswa unapokua Raisi au kiongozi kwa ajili ya watu wake.

Mzee alitaka project mbili kubwa zikamilike bwawa la umeme ili aje atangaze kushusha gharama za umeme, alitaka treni ya umeme ili usafiri uwe wa haraka na salama hata kama ni mgonjwa wa kukimbizwa Muhimbili kutoka Mwanza afike haraka ukiachana na kukuza uchumi wa nchi.

Mzee alijenga meli ziwa victoria, Tanganyika na nyasa ambazo tulipewa ahadi kwa miaka mingi lakini yeye alinunua kwa udikteta huo huo na isitoshe alinunua engine na kuzipiga service meli mbovu.

Mzee aliona kwa sababu nchi haina ndege na wanalalamika ngoja tununue tunaweza na hii ilikua ajenda ya upinzani ikageuzwa ikawa silaha kubwa ili kumvuruga.

Mzee aliona viwanja vya ndege havitoshi na vingine havina uzuri vilekebishwe kikiwemo cha mwanza , basi kwa kua alijua atazeeka na atamaliza safari ya uraisi na alipanga aende kwao chato basi akaamua ajenge uwanja wao wakaona anajipendelea.

Wakashindwa kuelewa kama asingejenga bado wangesema yeye ni fala kwa nini ? Afanye mambo makubwa kwa ajili ya nchi hlf asijenge kiwanja kwao. Tena wangesema amestaafu ameshindwa kujiuliza kama angetembelewa na wastaafu ila ya Mungu ni Makubwa.

Mzee amekarabati shule kongwe zote ikiwemo kantalamba boys iliyoko sumbawanga na nyingine nyingi.

Mzee aliona watu wanalalamika wenye vyeti feki wanachukua nafasi kuliko wanao stahili akarekebisha bac likageuzwa kuwa ni tatizo ili mzee awe mbaya.

Mzee alitaka miji na mikoa kuwe na stand zilizo bora nyingi zilianza ila imekuwa kero kwa watu

Mzee alitaka ikulu iwe dodoma na shughuli za kiserikali ziwe pale kama ilivyotakiwa hili nalo likawa kosa.

Mzee alikuta ndege tausi wameisha akaongeza

Watoto wanasoma bure

Kajenga barabara

Boom ukifika chuo unakutana nalo

Watu hatuoni hayo hatuoni mwelekeo wake ulivyokua mzuri kumbe moyoni alitaka siku moja aajili na kutuacha kwenye mazingira salama .

Walishindwa kuelewa kama kajenga stand, madaraja na meli kwa nini akose uwezo wa kuwaajili na kuongeza mishahara ,Wakasahau hawataki ushoga hawataki madini yaibiwe na wanataka wazawa washike fursa mbalimbali halafu hawataki kulipa kodi na hawataki kutegemea mataifa mengine kwa kila kitu. Kumbe wanataka vizuri halafu hawako tayari kuumia akafumba macho ili litimie asee ndio maadui waliongezeka kwa Mzee.

Lakini hakutaka misaada itutawale ili ushoga uwe lazima alitaka tujitegemee na sisi ni masikini kimuonekano na matajiri kwa mali tulizo kalia akili zake zikaona ngoja wasubiri, siongezi mishahara na sitoajili mpaka wafike hapa. Mungu amesaidia yote katimiza na kilichokua kime baki ni kuzindua tuu .

Dah kwa sababu hakuwa mnafiki alisema mbele yao hili kwa nini mlishindwa ? Kwa nini hamkufanya hivi ? Huku wakiwa na macho yao mawili sio wakiwa kaburini.

Kamzika Maalim seif na maneno mazuri na wala hajawahi kumjeli, kamzika kijazi na yeye Kapumzika .

Mzee hakua mnafiki, waliobanwa waliomuona adui hawa kulala kwa kumuharibia.

Moja ya karata za kipekee alizocheza alikataa lockdown hapo ndio alioneka ni mtu wa aina yake kuna watu mpaka leo wasingemaliza Mzigo wa biashara, wasingesafili pale walipo na kwenda kwingine ndani ya nchi na wengine wasingemaliza chuo, shule ya sekondari na shule za msingi ila hilo alilimaliza na kutuweka sawa na alijua akiendekeza hali ile watu hawatoishi.

Hii leo wajuba wamemsaliti mapemaa sana na mwelekeo wa nchi unadhihilika kuyumba.

Nateseka nikiwa Dodoma -ihumwa njia ya kuelekea Chamwino ikulu.

Rest in piece Raisi niliyekukubali kwa uthubutu wako, ujasiri na kutuweka kisaikolojia vizuri juu ya corona nilijua ipo na itakuwepo ila nilikuelewa tutaishi nayo kama magonjwa mengine na matango poli yako ulinilisha yakanikaa .

Haya msiompenda JPM kalala mnateseka mkiwa wapi? Maana mtaanza Maushauri yenu .

Magufuli.jpg
 
Huwezi kuwa kiongozi wa CCM na rais wa Tanzania bila kuwa mnafiki.

Unafiki ni moja ya sifa muhimu za kuweza kazi ya kuwa rais wa Tanzania na kiongozi wa CCM.

Walioshindwa unafiki wote wameshindwa kupata kazi hizi.
Lakini JPM hakua hivyo lbd kama umeanza kumfatilia leo alikua ni mtu wa twende au ugome lijulikane moja , ubunge na uwaziri wake aliupata kwa sababu alifanya kazi kwa kujituma na ndio maana toka awe mbunge alipita bila kupingwa.
 
Lakini JPM hakua hivyo lbd kama umeanza kumfatilia leo alikua ni mtu wa twende au ugome lijulikane moja , ubunge na uwaziri wake aliupata kwa sababu alifanya kazi kwa kujituma na ndio maana toka awe mbunge alipita bila kupingwa.
Magufuli ndiye rais mnafiki kuliko wote waliowahi kutokea serikali ya Muungano Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Tena kafanya unafiki wa kijinga uliomgharimu maisha yake.

Yeye ni mtu aliyejijua ama matatizo ya moyo miaka mingi sana.

Halafu akataka kutudhihirishia yuko fit akapiga mpaka push up.

Mwisho wake akaenda kutufia akiwa rais.

Amechukua kombe la unafiki na ubinafsi kawashinda marais wenzake wote.
 
Mkuu hakuna kiongozi aliyekuwa mnafiki zaidi ya Magufuli katika Marais wote waliotokea Tanzania. Chukulia mfano mmoja tu wa kauli aliyokuwa akiirudia kila mara kuliko marais wote ya kuwa maendeleo hayana chama, ila akawatishia wapiga kura wasipochagua mgombea wa CCM hawatapewa maji
 
Chief naomba nikuulize,unahakika hakuwa mnafiki hata alipokuwa waziri?

Unataka kusema aliwaambia watangulizi wake hasiyopendezwa nayo kwao kwa kipindi akiwa waziri wao kwa namna ile ile alivyokuwa anawachambua baada ya kuwa Rais?

Kwa Taarifa yako binafsi naona Hayati ndo alikuwa mnafiki zaidi. Tena hakuwa na sitaha kwa watangulizi wake hata kidogo.Bora mama anamkosoa kwa vitendo tu. Yeye aliwafedhehesha mpaka majukwaani.
 
Mataga mnateseka sana jamani. kauli za mama za kusema msiwabughudhi watu, msiwafungie media hovyo, msiwabambike kesi watu, ataunda kamati ya kushughulikia janga la korona, kodi zidaiwe kisheria, haya yoye ni kinyume alichokua anafanya Mwendazake.

kakosolewa kistaarabu na hii inawakera sana. Haya yote yalilalamikiwa na watu hamkuyaona..sasa yanafanyiwa kazi mnaweweseka kama mna kideri cha kuku.

Mwendazake alivyoingia madarakani si alikosoa aliyetoka madarakani mbona hamkulalama kwamba na yeye alikua ni part ya serikali mbona hakujitokeza kabla alibomoa jengo ubungo baada ya kuwa Raisi akasema kua kwa kuwa sasa hakuna wa kumzuia basi na kwa mama ni hvyo hvyo..muoshwa huoshwa!
 
Huyu aongezewe muda wa kutawala, huu mkakati ulikuwa mzuri tu.
 
Umeongea ukweli wote kwasababu:

Kabla ya kuwa rais alimsifia JK kwa safari zake za nje akisema kuwa ndizo zinazofanya mabarabara yajengwe.. cha kushangaza aliposhika usukani akakandia hizo safari na kusema no useless.

Alisisitiza maendeleo hayana vyama. Kilichotokea tunakijua.

Alinyoosha wenye vyeti feki. Ila kuna watu hakuwagusa.

The guy was not hypocrite.
 
Basi inatosha acha bhana, inatosha. Historia inasema watu watawala.na viongozi waliojaribu kuwatetea wanyonge( common people) walipigwa vita, wengine waliuawa vibaya. Kumbuka hata Yesu kristo, aliuawa kisa kuwasaidia maskini
Acha kupotosha yesu kristo aliuwawa kwa kusema kweli yeye ni mwana wa mungu siyo kwa ajili ya maskini, mwendakwao hakuwa mkweli mama katuthibitishia jana kuwa hata ukutu wa mabilioni uliojegwa bado tunaibiwa, ndege zzinatengeneza faida ukweli miaka yote ni hasara
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom