Haya yote yalikuwemo wakayapinga, leo wanayapongeza

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
377
1,000
Ipo hivi.........

Kuitenganisha mihimili ya dola ifanye kazi kwa kutokuingiliana ilikuwa ni sehemu ya mapendekezo ndani ya rasimu ya Warioba.

Kuundwa kwa mahakama ya juu (Supreme court) ilikuwa ni moja ya mapendekezo ndani ya rasimu ya Warioba.

Matokeo ya Rais kuhojiwa mahakamani ilikuwa ni moja ya mapendekezo ndani ya Rasimu ya Warioba

Rais kuondolewa kinga ya kutoshtakiwa kwa makosa aliyotenda wakati akiwa Rais ilikuwa ni moja ya mapendekezo ya Rasimu ya Jaji Warioba

Uhuru wa vyombo vya habari na waandishi wa habari ilikuwa ni moja ya mapendekezo ndani ya rasimu ya Jaji Warioba.

Jaji mkuu kutokuteuliwa na Rais ilikuwa ni moja ya mapendekezo ndani ya rasimu ya Warioba.

Je bado tunaihitaji Rasimu ya Warioba?
 
Top Bottom