Haya yasipofanyiwa kazi Tanzania itashuka kila siku

Choga Cosmasy

Member
Feb 8, 2017
18
32
Na
Cosmasy Choga

Binadamu huzaliwa na kupitia hatua zaukuaji na hawezi zikwepa,kwanza ni kutambaa na pili ni kusimamia vitu ndipo sasa hutembea kidogokidogo.

Ndivyo ilivyo katika shule, hakuna mwanafunzi anayeibukia tu Kuwa darasa la saba kwanza awali na baadae la kwanza na ndiko hupata upeo wa kuazia shule ni ukweli kwamba huwezi kwepa.

Achana na hilo,shirikiaho la soka duniani jana limetaja viwango vipya vya ubora duniani,wakati Uganda ikiendelea kuziburuza nchi za Africa mashariki Tanzania yenyewe imezidi kudidimia kila uchao wa viwango unapotoka.

Ni nani katuloga?, uvivu wetu wa kufikiri ndio mchawi namba moja kwenye soka letu na ndio maana tunashuhudia tu Uganda Afcon, hata nchi dhaifu zikituzidi ni nchi zisizo na hata amani bado zinatutupa jalalani.

Unaweza ukabakia umeduwaa kwa nini kila viwango vipya Tanzania inaporomoka au FIFA inachuki na stars la hasha tatizo ni udhaifu wa timu ndio unapelekea hayo.

Kuna mambo yanalilididimiza soka letu achana na mafanikio ya Serengeti boys zungumzia stars ambayo haijui kwa mara ya mwisho ilienda lini hata kuzisindikiza Cameroon kama ilivyofanya Uganda na Togo.

KWANZA UBOVU LIGI DARAJA LA PILI.

Ubora wa ligi daraja la kwanza unategemea nguvu ya second division liguae,bila mvuto wa ligi hii ni kazi bure,ili ligi daraja la Kwanza iwe imara lazima hii iwe bora, lakini ubora huo utatoka wapi angali ligi haina hata mdhamini?, hapa ndipo tatizo linapoazia timu hizi inabidi ziwe na wachezaji wenye viwango lakini watatoka wapi bila pesa?, tulitafakari hili na tujiulize kwa nini wachezaji wetu huenda Sweden kucheza ligi daraja la kwanza tutajua.

Kama ligi hii itaboreshwa tutapata ligi daraja la kwanza zuri ambayo italeta timu bora huku juu lakini sio sasa.

MIPANGO LIGI DARAJA LA KWANZA

Ligi daraja la kwanza imejaa ubabaishaji mkubwa,hii ni moja ya ligi ambayo inapaswa kuinua ligi kuu badala yake imekuwa njia sahihi ya matatizo huku juu.

Ukiacha daraja la pili hii ni ligi ambayo nayo haina mdhamini nini tunategemea?, ni vipi ligi kuu inaweza kuwa bora kama huku chini ni madudu?, ni vipi tunaweza pata timu bora ya taifa?, ni vipi tunaweza pata chimbuko sahihi la wachezaji wazuri wakati huku chini wapo kimazoea?, ukipata jibu ifinye tff.

Ligi daraja la kwanza ndio inapaswa kuwa imara ili ilete timu amabayo italeta mabadiliko huku juu lakini badala ya kupandisha timu kihalali timu zimekuwa zikipanda kwa maelekezo ya shirikisho la soka,nasema hatufiki kwa muundo huo tutazama Sana

MWISHO NI USIMAMIZI

Kiuhalisia maendeleo ya mtoto hujengwa na wazazi wote wawili labda tu mmoja awe kafariki,mtoto atafanya vyema kulingana na malezi anayopata hili halina ubishi ni sawa na hatua za ukuaji tu.

Kiuhalisia usimamizi wa soka letu bado upo nyuma sana licha ya tff kuwa na udhaifu lakini hata serikali ya michezo hatuna, inajua tu kuwaalika bungeni huu ndio mchango mkubwa kwake katika soka, ukija shirikisho limeshindwa kusimamia ligi hizi tatu kubwa katika misingi sahihi kote ni upangaji wa ovyo kabisa,wameshindwa kutoa huduma bora kwa wachezaji pindi wanapokuwa katika timu ya taifa,kwa hali hii tutegemee matokaeo ya Dar es Salaam tu hakuna namna.

KIPI KIFANYIKE KUNUSURU?

Nimetoa mifano ya kutosha huko juu ya sababu za kuporomoka sasa je tufanayaje?.

Timu ya taifa itafanya vyema endapo tu misingi sahihi ya usimamizi wa soka itazingatiwa,pili ni lazima ligi daraja la pili iwe bora ili kuijenga daraja la kwanza, Ligi daraja la kwanza iwe bora ili kuijenga ligi kuu ubora huo ni pamoja na kutafuta udhamini Ili timu shiriki zipate wachezaji wenye vingo na makocha wazuri wanaojua soka na si hawa wa kujalibu kama watapanda.

Ahsante
Cosmasy Choga
 
Serikali yetu ilihusika katika kukuza sio tu mpira wa miguu bali michezo kwa ujumla kulikuwa na sera madhubuti toka chini yaani shule za misingi na sekondari kutoka hapo unakuja katika taasisi za umma kulikuwa na michezo kama shimiwi na shimuta yote hayo yalifanya dhana na sera ya michezo kuwa hai achilia mbali taasisi kama majeshi tulipata kuwa na wapiganaji bora kama kina nassoro michael kina mwangata na wana riadha bora kabisa kama shahanga na wengineo.
Tukirudi penye soka taasisi na mashirika pamoja na kampuni kama sigara, pilsner, ndovu ya arusha na RTC kote nchini zilikuwa na timu mahiri kama biashara mwanza hapo ungewakuta kina Donald agay kina kichochi lemba na wengine nenda RTC kigoma ya kina sanifu iddi cheche hamza maneno list ni ndefu ukija swaalet hapo sitaji sana kina rashidi mmanga na Peter lucas wazee wenzangu watamalizia.
Shule zilikuwa chache miaka hiyo mtu anamaliza la saba mkubwa tu ana ajiriwa katika taasisi moja hapo aidha benki au halmashauri kama kibarua ila kazi yake inakuwa soka labda daraja la nne au la tatu atatunzwa hapo na baada ya misimu michache ataonwa na timu nyingine basi iliendelea hivyo. Serikali ilitunza vipaji kwa njia hiyo na anguko lilianza pale sera zilivyobadilika na kuzizika timu kama bandari mtwara swaalet na nyingine nyingi aaah ngoja nivute pumzi kwanza mambo haya yanaumiza.
 
Point sana
 
Back
Top Bottom