Haya yalisemwa 2005....na bado hali ni ileile (au imezidi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya yalisemwa 2005....na bado hali ni ileile (au imezidi)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CAMARADERIE, Jul 6, 2011.

 1. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Rais ajaye atakuna nyoyo zetu kwea kuikabili rushwa vilivyo?

  Rushwa ni donda ndugu, na ni kansa inayotisha kwa sasa nchini Tanzania tunafikiri ya kuwa watu wote waliobainika kujihusisha na rushwa, hata kama walishinda kesi zao mahakamani : ni vizuri wasipewe haki ya kuchagua viongozi wa taifa hili.
  Hii ni kuonyesha jinsi taifa inavyotaka sote tujipange sawa tukiwa na chuki kwa adui huyu rushwa wa maendeleo ya nchi. Mwandishi mmoja aliandika ya kuwa "mke wa Kaizari alituhumiwa kuwa ni mzinzi.Kaizari akaunda Tume ikamtakasa ni aibu kwa mke wake kuhutumiwa, akamdukuza"
  Watu ardhi , siasa safi, na uongozi bora lazima vihakikishe kwamba nchi iko imara kiuchumi, na uongozi ukiwajibika kwa watu katika majukumu yake. Uongozi ni wa muhimu katika maisha ya watu, nao watu ni wa muhimu ili uongozi uwepo.
  Pande zote mbili zinategemeana , bila ya mmoja, mwingine utayumba na hautaona nafasi kwa mwingine. Kwa hali hiyo, upande mmoja (viongozi) hauna budi kuwajibika zaidi ya upande mwingine kwa sababu unadaiwa kulinda makusudio ya taifa.
  Upande wa viongozi siku zote lizima ufuatwe na kundi kubwa la wananchi . Wananchi hawapaswi kumchagua au kuwachagua viongozi kamna hawajui sifa zao nzuri za uongozi . Sifa za awali za msingi za viongozi watakaochaguliwa na watu ni imani kwa maendeleo ya nchi , na kuwa na mamlaka ya uwajibikaji kwa wananchi.
  Hapa kwa lugha ya msahafu viongozi ni mawakili wa Mungu, ni watendaji katika wajibu wa uwakili kwa nafasi watakazopewa . Watatenda kwa mamlaka yatokanayo na neema ya Mungu, na uzoefu kwa msaada wake. Ni viongozi wa wananchi wanaowakilisha makusudio ya taifa kwa wananchi wao: katika hali ya maendeleo na maadili mema.
  Viongozi watakaochaguliwa na wananchi ni wajumbe watakaopewa mamlaka ya kulinda yatokanayo na wajibu.Watapewa mamlaka ya uwakili ambao hushia kwenye wajibu tu.Wataongoza wananchiu kwa kuzingatia wajibu kwao, kama watataka wananchi wawapende na kuwafuatana katika maongozi yao.
  Kiongozi ye yote afuataye wajibu kwa watu, watu vile vile humfuata kionogzi huyo . Zamani baada ya uhuru, kabla ya viongozi hawajachafuliwa na ufisadi, walizingatia kutafuta wajubu kwa jamii, nayo jamii ilifuata maongozi yao.
  Viongozi waadilifu wana sifa ya pekee waliyojadiliwa kutokana na juhudi zao katika wajibu wao . Hupenda kuwakusanya watu katika utendaji wao. Kusudi kubwa la kufanya hivyo linatokana na unyenyekevu wao. Ndivyo walivyo na ni wakweli wa Mungu na watambuzi wa shida za wananchi.
  Aidha wanajua kwamba wananchi siyo mali yao, bali ni mali ya Mungu , Kwa hiyo kionogzi ili wananchi wamchague na baadaye kuendelea kumfuata , hana budi kutumia uwezo wake wote kuwatumikia . Alama ya mapendo ya kiongozi kwa wananchi itaonekana kwa njia ya kuwahudumia , kuwajali , na hata kuwatembelea. Kwa matendo haya kiongozi hawatajiwa kuwa mtawala wa kutawala watu, bali wa kuwaongoza njia , pia yenye ni kivutio cha uhakika cha wale awaongozao, cha kutii na kushika maagizo yake kwa uhuru.
  Utii kwa viongozi chimbuko lake ni mahusiano ya karibu baina ya wakubwa na wadogo yanayotokana na huduma za wajibu wa wakubwa kwa wadogo (wananchi), na wadogo kwa wakubwa(viongozi) . Pande zote mbili hukutana katika njia moja inayounganisha siku zote na mapendo katika maisha yao.
  Kiongozi wa watu hahitaji kutumia nguvu (kutawala) ili watu wamduate , bali matendo yake katika wajibu wake tu ndiyo fimbo yake ya uongozi.
  Wananchi wanaowatii viongozi wao hufaidika, na uongozi unaotumiwa nguvu zote zaidi katika wajibu kuliko katika mamalaka waliyo nayo hufaifika pia . Na nguvu katika wajibu kwa wananchi, ni mamalaka ya utendaji yanayolenga matakwa ya watu kwa maslahi yao katika,
  " Sababu ya rushwa kukithiri miongoni mwa familia makuhani waliokuwa walafu na mahakimu wafisidi , nabii huyu alitabiri maangamizi ya mji mkuu Yerusalemu na kupatikana viongozi mwadilifu anayetarajiwa kuwa mlishi wa kundi kubwa la watu.Watanzania, kama ni kufanya utabiri , basi iwe ni maangamizi ya viongozi wote ambao wamefanya rushwa kuwa mradi mama wa kujipatia "malipo ya udhalimu Rushwa haeindelezi vipaji vya watu vya kubuni uwekezaji wa rasilimali za nchi kwa kuhakikisha kwamba dalili zote za ufisadi miongozi mwa viongozi na wananchi zinango'olewa . Ni ushauri wangu kwamba rais ajaye atimize wajibu wake wa kwanza kwa suala la ufisadi kama kipingamizi cha kuanza katika juhudi zake zote za uongozi wa taifa hili."
  maendeleo.
  Tuone tena yaliyomo kwenye msahafu kuhusu kuwajibika katika mamalaka. Mtumishi wa Mungu Timotheo alisifiwa sana na mkuu wake wa kazi Mtakatifu Paulo , kutokana na sifa zifuatazo alizokuwa nazo.
  Aliwajibu kwa watu, aliwapenda, alitafuta matakwa yao si yake binafsi, alitafuta nafasi ya kuwahudumia kwa ajili ya Mungu na watu wake, na hakutafuta heshima kutoka kwa watu (Wafilipi 2:19-23).

  Kutumia nguvu ya mamlaka badala ya wajibu wa kutafuata heshima kutoka wka watu. Kwa sababu heshima ikitafutwa, uongozi huanza kutafuta nafasi za kuangalia tabaka za watu. Wengine hukaribishwa na kusikilizwa na kuwajali zaidi kwa sababu ya hali zao nzuri, lakini wengine haungaliwa kwa jicho la hasira lifukuzalo.
  Ni makosa ya uongozi kama utakumbatia zaidi mamalaka kuliko wajibu , na matokeo yake ni kutafuta heshima kwa nguvu na pengine bila kujali kuwahudumia watu. huko ni kutumikiwa na watu badala ya kuwatumikia.
  Kwa hali hiyo, hakuna haja ya kufuata uongozi ambao mwelekeo wake kwa watu ni kutafuta maslahi kwao . Kwa kawaida tabia ya mwelekeo kama huu hupima kama utafaidika au la katika uduma zake kwa watu.
  Mungu anapowataka viongozi moyo wa rehema wao hutanguliza na kudai sadaka, au Mungu anapotaka macho ya viongozi ili yaone maumivu ya umasikini , wao hufumbua yote ili wasione chochote. Au bwana anapoitaka mikono ya viongozi ili aitumie kwa lengo lake, humpa kwa muda mfupi sana na kuondoka kwa sababu kazi ni ngumu mno.
  Au bwana anapotaka midomo ya viongozi kukemea dhuluma nchini, wao wanawong'ona ili wasishitakiwe. Hii ni roho mbaya inayokuwa si mbali tu na watu, bali pia mbali na Mungu. Matokeo yake ni kukataliwa na wananchi baada ya kushikamana na mamlaka yao kwa kutafuta heshima kazini bila kuwajibika.
  Dunia imashuhudia kwamba endapo kipaumbele cha viongozi kinageuzwa na kuwa maslahi kwanza, basi chanzo cha maovu au uharibifu katika maisha ya wananchi ni fedha . Nikirudi katika msahafu, viongozi watafutao maslahi tu; Nabii Mika alisema yafuatayo: Waneijenga sayuni kwa damu , na Yerusalemu kwa uovu , . Wakuu wake hukumu ili wapate ajira, na manabii wake ili wapate fedha " (Mika 3:10-11)
  Sababu ya rushwa kukithiri miongoni mwa familia , makuhani waliokuwa walafi, na mahakimu wafisidi , nabii huyu alitabiri maangamizi ya mji mkuu Yerusalemu , na kupatikana kiongozi mwadilifu aliyetarajiwa kuwa mlishi wa kundi kubwa la watu . Watanzania kama ni
  Aidha wajua kwamba wananchi siyo mali yao, bali ni mali ya Mungu Kwa hiyo , kiongozi ili wananchi wamchague na baadaye kuendelea kufuata , hana budi kutumia uwezo wake wote kuwatumikia. Alama ya mapendo ya kiongozi kwa wnanchi itaonekana kwa njia ya kuwahudumia kuwajali , na hata kuwatembelea . Kwa matendo haya kiongozi hatarajiwi kuwa mtawala wa kutawala watu, bali wa kuwaongoza njia pia yenye ni kivutio cha uhakika cha wale awaongozao , cha kutii na kushika maagizo yake kwa uhuru.kufanya utabiri , basi iwe ni maangamizi ya viongozi wote ambao wamefanya rushwa kuwa mradi mama wa kujipatia "malipo ya udhalimu"
  Rushwa haiendelezi vipaji vya watu vya kubuni uwekezaji wa rasilimali na nchi, kwa kuhakikisha kwmba dalili zozote za ufisadi miongoni mwa viongozi na wananchi zinaong'olewa . ni ushauri wangu kwamba rais ajaye atimize wajibu wake wa kwanza kwa suala la ufisadi kama kipingamizi cha kwanza katika juhudi zake zote za uongozi wa taifa hili.
  Ushirikishwaji wa viongozi na wananchi nchini katika janga la rushwa upangwe kwenye safu ya mbele ili kutekeleza azma ya maangamizi ya tabia ya kupenda rushwa miongoni mwa wananchi. Nayo mitego ya PCB ni kama mitego , ndani ya nyumba, au paka ambaye harufu yake inajulikana: na hivyo panya hujificha kwa kuhofu kukamatwa na paka (PCB)
  Njia nzuri ya kuangamiza rushwa ni kuruhusu nafasi huria ya watu wote ya kupeleka kwa siri maoni yao kwa tume maalumu ya kuidhabiti rushwa. Liwe ni zoezi la kila mwaka wakati wote na taarifa za siri shidi ya wahusika (watajwa) zifanywe kwa makini.
  Katika msahafu, vita dhidi ya ufisadi ilikuwa wazi kwa yerusalemu nzima:"Basi , kwa ajili yenu. sayuni utalimwa (utakombolewa) kama shamba lilimwavyo , na Yerusalemu utakuwa magofu ; na mlima wa nyumba(vifusi) utakuwa kama mahali palipoinuka mistuni (Mika 3:12).
  Ubaya ukikithiri hutafutiwa dawa na hatima yake kwa gharama yoyotre kama ile ya kukomboa makao makuu ya nchi(Yerusalemu) yaliyogeuzwa yakawa magofu.
  Hapa tanzania magofu yatakayosababishwa na rushwa itakuwa ni kifumba macho na kuwang'oa wote wanaobainika kuwa na tabiya hiyo mbaya . Rushwa ni mwiba katika mwili wa taifa . Ukichomwa naa mwiba mguuni, kazi ni kuhakikisha kwamba mwiba ule unango'lewa.

  Tahadhari ya tangu sasa tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwishoni wa mwezi huu , ni kuondoa magugu ya kubaki na viongozi watakaoneza mbegu za uadilifu nchi nzima kwa kuwajibika zaidi katika majukuu ya maendeleo ya taifa bila ya kutafuta malipo ya udhalimu.
  Magugu haya ndani ya ngano safi miongoni mwa watanzania yataondolewa hapo juu , pamoja na kutumia Uchaguzi Mkuu kama nafasi ya pekee ya kutokuwachagua viongozi ambao wana historia ya ubaadhirifu , lakini bado hawajakamatwa na kupelekewa kwenye vyombo vya haki.
  Ni matumaini yangu kwamba hata Mungu yuko upande wa Watanzania ambao wako mstari wa mbele katika vita dhidi ya rushwa . Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Juhudi za maangamizi ya tabia ya ufasidi na bariki uchaguzi Mkuu wa 2005

  Kutoka gazeti la RAI

  ISSN 0856-4973
  Na Mwandishi Maalumu.

   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  CCM 'chenge hausiki na kashfa ya rada'

  Nape 'chenge ni gamba'
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Namkumbuka sana huyu babu.....hii baiskeli ilikuwa ina itwa SWALA usiniulize ilitengenezwa wapi

  [​IMG]
   
 4. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu kimoja ndugu zangu wanajamvi napenda tukielewe...
  Saikolojia inasema:
  Mwanadamu ana tabia zake ambazo huwa kwa kawaida ni KINYUMENYUME!
  Ndio maana ukiweka bango ukutani:
  USIKOJOE HAPA.
  Utakuta kojo linataka kutoboa ukuta huo
  ama ukiweka tangazo:
  USITUPE TAKA HAPA
  hapo waweza juta maana utakuta rundo la taka na ziada zake...
  Ndio maana wenzetu wakakomeshea kwa kusema
  AHSANTE KWA KUTOVUTA SIGARA HAPA!
  ama:
  AHSANTE KUWEKA TAKA KWENYE KAPU LA UCHAFU!
  au:
  AHSANTE KWA KUWEKA MJI SAFI!

  Je kwanini walifanya hivyo? Sisi hatuna muda wa kutafiti wala kujiuliza!!

  Ndio maana ofisi zinazoongoza kwa MLUNGULA ni zile zenye MABANGO
  "HATUPOKEI RUSHWA HAPA"
   
 5. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Rushwa ni adui wa haki tuliimbishwa! hatukuwa tukiijiua rushwa wala ubaya wake wakati huo!
  Tulipokua ili mambo yaende haraka uliambiwa lete chai wakati hukwenda pale na birika au chupa ya chai!
  Tulipoendelea kutafuta kazi ama tiba tulitakiwa kuwa na shati la mikono mirefu au kwenda MTUKULA!
  Ambae hauelewa lugha hizo alikwama!
  Ilianza kama KIPELE!
  LEO HII NI JIPU LINALOOZESHA MWILI!
  TUNASHINDANA KUTOA NA KUPOKEA RUSHWA!
  Ndio maana tunapata ajira leo na kujenga makasri kuliko ya wastaafu waliofanya kazi miaka!
  Ndio maana leo tunaendesha magari ya kifahari kuliko ya wafanyibiashara maarufu!
  hakuna anaehoji wapi tumepata uwezesho!
  wala hakuna atakaeuliza ni kwa mshahara upi tumemudu kupata mafanikio hayo!
  Wala hakuna anaedadisi tunawezaje kusomesha watoto wetu shule zinazozidi pato letu lote la miaka miwili kwa muhula mmoja!
  TUNANUKA! TUMEVUNDA KWA RUSHWA NA MILUNGULA!!
   
 6. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha mbali...
  Baiskeli hiyo ikitengenezwa Tanzania, jirani na kiwanda cha kusindika nyama! Kama viivyo viwanda vingine VYOOTE leo vingi vyake ni maghala ya wachuuzi wanaotoa mali duni nje ya nchi kutuuzia!!
  Kama zilivyokufa Matsushita na Philips ndivyo livyoondoka SWALA na ndugu zake kwani mpaka babu anang'atuka hali ya viwanda ilishakuwa hoi! Babu wa watu akajionea atakufa bure kwa presha WATANZANIA HATUBEBEKI akang'atuka auone mwisho wetu!
   
 7. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  I can bet $1,000,000 JK hana baiskeli
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  You are right !
   
Loading...