Haya yalikuwa matumaini ya wengi kwa Dk. Rioba

Kabwena

Senior Member
Jun 17, 2013
104
195
Miezi tisa iliyopita Charles William, mmoja kati ya waliowahi kuwa wanafunzi wa Dk. Ayub Rioba aliandika maneno haya kuhusu kuteuliwa kwa mhadhiri huyo kuwa mkurugenzi wa TBC.

Dk. Rioba iepushe TBC na fedheha

Tarehe 14 Machi, 2016. Ilichapwa katika gazeti la MwanaHALISI

Na Charles William

SHIRIKA la Taifa la Utangazaji (TBC), limepata mkurugenzi mpya mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Dk. Ayub Rioba aliteuliwa na Rais John Magufuli, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana, aliyefikisha umri wa kustaafu.

Daktari Rioba, ambaye ni mhadhiri mwandamizi wa Chuo kikuu Cha Dar es Salaam, katika Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC), ameteuliwa kushika nafasi hiyo ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu ateuliwe kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo.

Mbali na kuwa mhadhiri wa masuala ya habari na mawasiliano kwa umma, Dk. Rioba pia ni mtangazaji na mwandishi wa habari wa siku nyingi, akifanya kazi katika vyombo tofauti vya habari hapa nchini.

Katika makala zake kwenye magazeti mbalimbali yakiwemo MwanaHALISI na Raia Mwema, kwa nyakati tofauti, tumeshuhudia Dk. Rioba akililia mabadiliko katika tasnia ya habari nchini, akichambua, akikosoa na kushauri kuhusu utendaji wa vyombo vya habari.

Sasa anayo kazi ya kuisimamia TBC, ambayo kwa muda mrefu imekuwa "shamba la bibi," ikijiendesha katika namna inayozua sintofahamu kubwa kwa wananchi wengi, huku ikijinasibu, pasina aibu, kwa kibwagizo cha “ukweli na uhakika!”

Utendaji wa TBC kama chombo cha habari umekuwa ukishuka kila iitwapo leo, huku ikipoteza watazamaji na hata kupoteza sifa ya kuitwa shirika la taifa la utangazaji kwani chombo hicho kimekuwa kikijidhalilisha na 'kuzodolewa' mara kadhaa hata na mamlaka zingine za kiserikali.

Tarehe 28 Agosti mwaka jana, wakati Tanzania ikiwa katika vuguvugu la uchaguzi, Mamlaka ya Mawasiliaono hapa nchini (TCRA), ilitoa onyo kali kwa TBC kutokana na chombo hicho kufanya ubaguzi katika kusoma magazeti yenye habari za mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa.

Adhabu hiyo ilitokana na kitendo cha aibu na fedheha kilichofanywa na TBC taifa mnamo tarehe 15 Agosti, 2015 katika kipindi chake cha televisheni cha 'Jambo Tanzania' ambacho hurushwa saa 12 mpaka saa tatu asubuhi.

Katika kipengele cha usomaji wa magazeti, mtangazaji wa TBC aliudanganya umma kwa kusema, habari kubwa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Majira ni "CCM yazidi kuwaumbua wanaomfuata Lowassa" wakati habari kubwa ilikuwa ni "Mbeya kwafurika."

Wakati akisoma gazeti la Nipashe pia, alisema habari iliyopewa uzito wa kipekee ni "Mbarawa atoa semina ya sheria za mitandao" wakati habari kubwa iliyopewa uzito katika ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ilikuwa ni "Mafuriko Mbeya" ambayo hakuisoma kabisa.

Ajabu na kweli ni kuwa mtangazaji huyo wa televisheni ya taifa alifanya vituko hivyo vya karne, huku kamera zikionesha habari hizo alizokuwa akiziruka na kuacha kusoma. Nadhani alisahau kuwa anatangaza kwenye televisheni na siyo redio.

Haikujulikana mara moja kama mtangazaji huyo alifanya kitendo hicho kwa utashi wake au la, lakini kitendo cha shirika hilo kutomuonya wala kuuuomba umma radhi, licha ya malalamiko kilionesha wazi kuwa kilichofanyika kilikuwa na baraka za uongozi wa juu.

Ni TBC hii hii ambayo mwaka 2010, iliingia matatani iliporipoti habari ya mkutano wa hadhara wa mgombea urais wa CHADEMA kwa kurusha picha za baiskeli, mikokoteni na watu waliokaa pembezoni ili kuonesha kuwa mkutano huo ulihudhuriwa na watu wachache mkoani Mara.

Ni TBC hii hii ambayo nimekuwa nikishuhudia katika migomo ya wafanyakazi, maandamano ya wananchi na hata maandamano ya wafuasi wa dini, watangazaji wake wakitimuliwa mbio kwa madai kuwa wataenda 'kupindisha habari' wanazozichukua.

Ni aibu na fedheha kwa shirika la taifa la utangazaji kuchukiwa na wananchi, kutoaminika na kuzomewa pale magari yake yanapowasili katika baadhi ya matukio ya habari na zaidi ya yote, kupewa onyo na mamlaka zingine za serikali kutokana na utendaji usiozingatia weledi wala taaluma.

Uteuzi wa Dk. Ayub Rioba, ambaye amebobea kitaaluma na kiuzoefu katika vyombo vya habari unaibua 'lepe' la matumaini ya wengi tunaomfahamu mtu huyu.

Uzoefu wa kikazi kuanzia kwenye utangazaji, uandishi wa habari na utendaji katika Baraza la Habari (MCT), ndio unaotoa mwangaza wa matumaini hayo huku kariba na wajihi wa Dk. Rioba ukichochea zaidi matumaini hayo.

Hatutegemei tena TBC ambayo sifa yake kubwa ni 'kuchonga na kupindisha' habari huku ikijifariji kwa kibwagizo 'tepetevu' cha ukweli na uhakika, itaendelea kuwa hivyo hivyo chini ya Dk. Rioba.

Tunatarajia kuwa weledi wa kitaaluma ambao Dk. Rioba ameupata katika nchi mbalimbali duniani, kuanzia shahada ya kwanza mpaka ya tatu, utakuwa ni nguzo kuu ya mabadiliko ya kiutendaji katika shirika hilo ambalo linaonekana kupoteza mvuto.

Tunatarajia kuona TBC ikirusha habari za kuwaunganisha Watanzania wote wa dini zote, vyama vyote vya siasa na rika zote, siyo TBC inayodhihakiwa na kuitwa "TBC CCM" wala siyo ile inayotaniwa na kuitwa "televisheni ya wastaafu serikalini."

Dk. Rioba amepata shahada zake tatu nje ya nchi, shahada ya sanaa katika mawasiliano ya umma (1993) Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, Shahada ya Uzamili katika uandishi wa habari kutoka Chuo kikuu cha Wales, Uingereza (1997) na Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Tampare nchini Finland (2012).

Shauku ya wengi ni kuona elimu yake ya darasani, uzoefu wake wa kikazi na kitaaluma 'ukinyunyizia' mabadiliko katika utendaji wa kila siku wa TBC na hatimaye kulipa heshima shirika hilo la umma linaloendeshwa kwa kodi za Watanzania.

Sitarajii kumuona Dk. Rioba akipitia katika mkondo uleule wa Dk. Harrison Mwakyembe na Profesa Issa Shivji, wanasheria vinara wa kuikosoa serikali kupitia maandiko yao katika vitabu ambao baadaye walikuja kuyakataa mawazo yao yaliyopo katika kurasa za vitabu vyao!

Tunamfahamu Dk. Rioba kama jasiri, asiyejipendekeza na mbunifu, hata hivyo, watu hubadilika kulingana na wakati na maslahi waliyonayo katika jambo husika.
Wakati ndiyo msema kweli, utatueleza juu ya hilo na kwa hakika historia itamtukuza au kumuhukumu mteule huyu mpya, Dk. Ayub Rioba Chacha.
 
kubwa_Lao

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
929
1,000
TBC ilikua ikifanya vizuri kipindi Tido Mhando akiwa ndio mkurugenzi mkuu....
Jamaa aliifanya kuwa ya kuaminika lkn pia alikua na mikakati ya kuwa na channel za kiingereza na Kifaransa ukiachilia mbali TBC2 ingawa sina hakika kama TBC2 bado ipo hewani.

Wengine wote wanasaka tonge tu, wacha wajilie wakimaliza watajipumzikia zao
 
MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,727
2,000
Pamoja na watu wengi kumsifia Tido Mhando akiwa TBC ni kweli alifanya mkubwa kwa utashi wake lakini kumbuka TBC ina msingi yake ktk uendeshaji wake kama taasisi ya umma.

Dr Rioba ni mzuri lakini kwa TBC ataendesha kwa kufuata msingi ya TBC na si nje ya hapo.

TBC iko makini na kazi zake na INA vyombo vya kisasa na vya gharama sana na kamwe haitafanya Fanya kazi kwa kufuata matakwa ya MTU Bali taratibu za taasisi.

Mkurugenzi Dr Rioba amepewa dhamana na Rais na anajua anachokifanya ili kuboresha shirika na maslahi ya watumishi tumwache afanye kazi.
 
ketete

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
771

hivyo unakiri wazi kwamba watu ni wazuri ila taratibu za TBC ni mbaya.
kwa nini zisibadirike basi ili chombo kiweze kuaminiwa????
 
chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,560

Kwa hiyo misingi ya TBC ni kwenda kinyume na misingi ya uandishi wa habari?
 
N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,071
2,000
Na ndicho chombo cha elektroniki chenye idadi kubwa ya wasomi tanzania lakini wanayofanya humo ndani dah ! badilikeni
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,638
2,000
Pamoja na watu wengi kumsifia Tido Mhando akiwa TBC ni kweli alifanya mkubwa kwa utashi wake lakini kumbuka TBC ina msingi yake ktk uendeshaji wake kama taasisi ya umma.

Dr Rioba ni mzuri lakini kwa TBC ataendesha kwa kufuata msingi ya TBC na si nje ya hapo.

TBC iko makini na kazi zake na INA vyombo vya kisasa na vya gharama sana na kamwe haitafanya Fanya kazi kwa kufuata matakwa ya MTU Bali taratibu za taasisi.

Mkurugenzi Dr Rioba amepewa dhamana na Rais na anajua anachokifanya ili kuboresha shirika na maslahi ya watumishi tumwache afanye kazi.
Mlau sijakuona ila kulingana na hoja zako ww utakuwa ni mzee, na nimegundua ww utakuwa ni mmoja wa washauri wa serekali hii. Kwa jinsi ulivyotoa utetezi wa uwanja wa ndege wa chato unaonyesha ni mtu usiye mbunifu lakini unayeamini katika nguvu ya dola. Watu kama nyie hamjawahi kujiajiri na hamtokaa muweze kwani hakuna chochote utakachoweza kufanya kwa uwezo wa ushawishi bali nguvu za dola. Na iwapo mtu kama ww itatokea kutakiwa kupunguzwa kazini ni lazima utashinda kwa waganga wa kienyeji kwa huna unalomudu zaidi ya kutegemea mshahara. Kama unaweza kusimama hapa bila aibu na kutetea huo udhaifu na kuita eti hiyo ni taasisi yaani ni bonge la aibu. Kwa maneno marahisi ni kwamba taasisi ya umma haijali ubora bali ni nini watawala wanataka!! Haya mawazo yako nina hakika ndio yalilyochangia kuua viwanda vya nchi hii. Ni aibu watu kama nyie ndio vimbelembele wa madaraka wakati hamjui lolote.
 
Revola

JF-Expert Member
Apr 14, 2015
1,169
2,000
Dr. Ayub Lyoba anaiendesha TBC kwa kifuata kanuni na sharia zilizowekwa nasikwa maamuzi yake binafsi kama mnavyodhani msimuhukumu hatoi mabilioni mfukoni kuiendesha TBC bali anapewa sasa habari zakumsema tulieni asimamie anchoweza kujikuna
 
MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,727
2,000
hivyo unakiri wazi kwamba watu ni wazuri ila taratibu za TBC ni mbaya.
kwa nini zisibadirike basi ili chombo kiweze kuaminiwa????
Nimesema TBC ina misingi yake ambayo ukiwa pale unatakiwa kuifuata ndiyo Serikali yenyewe.

Huwezi kuendesha kile chombo kwa utashi wako tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom