Haya ya Nigeria Hatuyataki Bongo kabisaaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ya Nigeria Hatuyataki Bongo kabisaaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tango73, Jun 27, 2011.

 1. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  [h=1]Suspected radical Islamists kill 25 in Nigeria bombing[/h]By REUTERS
  06/27/2011 03:04

  [h=2]Attackers throw 3 sets of explosives from motorbikes at drinking spot, military sources say; group wants strict Shari'a law in Nigeria.[/h]
  MAIDUGURI, Nigeria - Suspected members of a radical Islamist sect threw bombs at a drinking spot in Nigeria's northeastern town of Maiduguri on Sunday, killing around 25 people, witnesses and military sources said.

  The attackers -- who the military said were suspected members of the Boko Haram sect -- threw three sets of explosives from the back of motorbikes at around 5 p.m. (1600 GMT) and appeared to be targeting police officers, witnesses said.

  RELATED:
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Very sad indeed. Vitendo vya namna hii vikiachwa kama ilivyo kwa nigeria vinaigeuza nchi kuwa ya kinyama na seriously, extremism ya namna hii inapaswa kukomeshwa mara moja. Tusiruhusu imani moja ikandamize nyingine.
   
 3. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndio maana waniaitwa Boko HARAM
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwenu wakuu,

  Haya mambo yanaweza kutokea hata Tanzania bila kipingamizi chochote.Mkondo wa siasa hasa kipindi cha awamu ya pili ya Rais Kikwete masuala ya udini yamechukua nafasi kubwa ndani ya jamii yetu bila kukemewa.

  Serekali ya mheshimiwa Kikwete mara kwa mara imetumia mwavuli wa dini kama kinga yake dhidi shutuma zinazotolewa na wakosoaji mbali mbali.Viongozi wa dini ya kilslam wametumika kutetea,kukemea na kutoa miongozo mbali mbali ya kutetea udhaifu wa serekali iliyoko madarakani.Matamko yanayostahili kutolewa na wasemaji wa serekali wanaolipwa mishahara kwa kazi hiyo yamekuwa yakitolewa na viongozi wa dini ya kiIslam.Sakata ya mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia kuanzia Arusha mpaka huko Musoma Nyamongo yameshutumiwa na wapenda amani ndani ya nchi na nje ya nchi,ajabu viongozi wa dini ya kiIslam wamekuwa wakiunga mkono uharamia unaofanywa na jeshi la polisi kwa maelekezo ya wanasiasa.Ukitazama sababu zinazowafanya viongozi wa dini ya kiIslam kuunga mkono kila serekali inapokosolewa utakuta ni imani iliyojengeka miongoni mwa viongozi hao kwamba serekali inaongozwa na muIslamu mwenzao [Rais na Makamuwa Rais].Wakosoaji wa serekali ya Mheshimiwa Kikwete wameaminishwa na watetezi wake wanamkosoa kwasababu hawaipendi dini ya kiIslam !! Kitu ambacho sikweli hata kidogo.Najiuliza enzi za utawala wa Rais Mkapa Dr W Slaa alikuwa akimkosoa mkatoliki mwenzake sikusikia hata siku moja Kadinali Pengo akisuguana na Dr W Slaa eti kwakuwa ni mkatoliki mwenzake.Vivyo hivyo Mchungaji Mtikila na A L Mrema walikuwa wakimwaga mabomu kila nafasi inapotokea hapakuwepo kiongozi wa Dini ya Kikristo aliyewakataza kufanya hivyo.

  Taratibu viongozi wa dini ya kiIslamu wameanza kujiona ni sehemu ya serekali ya Mheshimiwa Kikwete.Wameanza bila kuficho madai ya kupewa tena nafasi [Rais] muIslamu awamu ijayo kwakuwa wakristo Nyerere na Mkapa walitawala Tanzania miaka 34.Kikwete na Mwinyi miaka 20 tu.Madai ya mahakama ya kadhi,OIC na nk ni bahadhi ya mambo yanayoshabikiwa na utawala wa awamu ya mheshimiwa Kikwete.Magazeti Al Nuru na radio Imani ya Morogoro yamepewa uhuru wa kugawa waTanzania kwa misingi ya dini bila kukemewa kwa muda mrefu sasa.Kuna dalili UWT inaratibu mpasuko wa udini kwa maslahi ya kikundi cha wateule wachache wasiojua mwisho wake ni umwagaji damu pasipo sababu za msingi.Siku hizi utasikia sheikh akihutubia waumini wake eti Tanzania kuna mfumo Kristo/katoliki bila aibu ukimwamba atoe ushaidi hana bali blah blah za udini.Siku hizi wameibuka watunzi wa vitabu wakielezea bila aibu uongo na fitina jinsi Mwl Nyerere alivyowaonea waIslamu katika utawala wake ilihali inajulikana wapo wakristo kibao waliokumbana na mkono wake bila kujali dini zao eg Osca Kambona,Marialle na nk.

  Masuala yote haya yakiachwa yaendelee hakika Boko Haram ya Tanzania itafanya yanayofanywa na Boko Haram ya Nigeria.Nimejaribu kutafakari kidogo Tanzania ingekuwa wapi leo kama Kikwete angekuwa Rais wa kwanza Tanzania kaikuta nchi imejaa amani tele anataka kuiacha inamwagika damu.
   
 5. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MBona Zanzibar yanatokea kila siku.
   
Loading...