- Madakitali wanashauri kuepuka kula nyama kuepuka mafuta lakini ukweli mboga mbadala ni adimu.
- Wanasema tule mbogamboga lakini ukitembelea huko zinakolimwa ni sumu tupu tunakula.
- Wanashauri ule samaki lakini huyo samaki mwenyewe ukiangalia tangu avuliwe ziwani huko Mwanza, asafilishwe hadi afike dar es salaam mwezi mzima anakuwa tayali kageuka sumu.
- Ukisema ule chipisi basi huko nako utakutana na mafuta ya korie yanakusubiri.
- Ukiamua ule mihogo labda nayo uagize sumbawanga maana ukinunua inayolimwa hapa mjini nayo imetiwa mbolea na sumu kibao za kukuzia.
- Haya ukiamua ule matikiti yanalimwa Kwa kudungwa sindano nayo ni sumu tupu hapa mjini.
- Ukiamua ule kuku, ndo kabisaa hawa boila ni sumu tupu.
- Ukiwasha A.C nyumbani kwako au kwenye gari nayo ni sumu tupu ni hatari kiafya wanasema
- Ukivaa nguo mtumba ni hatari kwa afya yako.
- Ukinywa soda ni sumu tupu, kandoro kuna kipindupindu, Maji ya chupa ndo kabisaa chlorine tupu.
- Ukichimba kisima mjini, jilani yako anachimba karo la choo, ukiiunga dawasco hayo mabomba yanako pita ni aibu tupu.
- Ukifanikiwa kukwepa kooote watakubana kwenye mionzi ya simu na TV nayo ni sumu tupu.