Haya Wana-Yanga Afrika, you broke my heart! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya Wana-Yanga Afrika, you broke my heart!

Discussion in 'Sports' started by Mphamvu, Apr 30, 2012.

 1. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Washabiki wa Dar es salaam Yanga Afrika, ya Umoja wa Mataifa jana mmeniangusha.
  Kwanza, mlikuja kwa uchache sana pale Uwanja wa Taifa kitu ambacho si kawaida yenu, halafu mkajitenga, mkakaa mbali sana na wenzenu wa Simba.
  Lakini tuache hayo ya mikao ya kiwanjani, kuna tabia mbaya sana mliionesha kwa timu yenu ya muda, Al Ahly. Kwanza mlikuja bila jezi za bluu za Ahli, why? Mbona za Mazembe mlinunua kwa wingi, halafu kwanini hamkuipa sapoti ya kutosha, zaidi ya kusubiri Simba wapaishe mpira ndo mzomee. Ushabiki ni pamoja na kuipa matumaini timu yako hata kama unaona inapumulia mashine. Nyie mnafikiri kama sisi tusingeshangilia Zamalek kwa ari wangepata lile goli la kusawazisha?
  Mapenzi hayako ivo jamani, kama umeamua kuolewa, shurti ulale bila chupi, sasa ushabiki wa nusu nusu wa nini? Haiwezekani SSC kupata goli moja tu, nyie make kimya mpaka mwisho wa mchezo. Mmesahau kama Simba na Yanga ni watani wa jadi, ni jukumu lenu kuiombea Simba njaa wakati wowote, masaa 24, siku saba za wiki, au jana upepo ulikuwa hausomeki?
  Siku nyingine kama hamwezi kushangilia wapinzani wetu ni aheri mkatulia majumbani kwenu mkatuacha tuujaze uwanja wenyewe, haiwezekani watu mje kuishangilia Shandy halafu jjukwaa lenu liwe kama soko la Karume, yaani yametundikwa mashati tu.
  Kiburi chenu kimewaponza, sasa sisi waleeÂ…
  Na huu utani wa jadi naona hamna nia nzuri nao, sas hivi tutajitoa. Nataka muelewe kwamba Tanzania ni nchi pekee ambayo timu ya nje ikija kucheza hata na timu ya taifa, ina uhakika wa kupata mashabiki wa kutosha, nyie hamjivunii hilo? Sasa mbona mnataka kuitia doa sifa hii ya pekee?
  Chondechonde, next time msirudie kichefuchefu cha jana.
  Yanga Afrika, DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO!​
   
Loading...