Haya Wana-Yanga Afrika, kazi kwenu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya Wana-Yanga Afrika, kazi kwenu!

Discussion in 'Sports' started by Mphamvu, Apr 9, 2012.

 1. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho CAF, Simba SC sasa watawavaa El Ahly Shandy ya Sudan baada ya Al Ahli Shandi kuwachapa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji jumla ya magoli 3-0.

  Katika mchezo wa leo El Ahly Shandy wameibuka na ushindi wa goli 2-0 kwenye Mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa huko Mjini Shandi, Mji ambao uko Kilomita 150 Kaskazini Mashariki ya Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum.

  Bao zote 2 za Al Ahli Shandi zilifungwa na Nadir Eltayed katika Dakika za 14 na 60. Hivyo El Ahly Shandy wamewatoa Ferroviario de Maputo kwa jumla ya bao 3-0 baada ya pia kuwatungua huko kwao Maputo bao 1-0.
  12147.gif
  Al-Ahli ambao nembo yao ni hiyo hapo juu, wanashika nafasi ya nne katika ligi kuu ya Sudan, wakiwa na pointi 37, ambazo ni 31 nyuma ya vinara wa ligi hiyo,Al-Hilal baada ya mechi 26 kuchezwa.
  Jezi ya nyumbani ya Al Ahli Shandi ni ya rangi ya buluu tupu kama inavyoonekana hapo chini.
  Al Ahly.....jpg
  Kama ilivyo utaratibu wetu wa siku zote, ni zamu ya klabu hii ya Sudan kupewa sapoti kubwa na washabiki wa Dar es salaam Yanga Afrika ili waweze kutoa upinzani katika mchezo wa raundi ya 16 utakaochezwa hapo Uwanja wa Taifa Aprili 29 na marudiano huko mjini Shandi majuma mawili baadae.
  Kuhusu jezi, washabiki wa Yanga wanaweza kuvaa jezi za klabu ya Chelsea, ambazo zimetapakaa kwa wingi jijini Dar, hii ni kuwaepusha gharama za ziada za kutafuta jezi halisi za Ahli, na pia kuwakomoa wafanyabiashara uchwara wanaotumia uhasama wetu mtamu kujipatia fedha za bwerere.
  Nawasihi juhudi za kutafuta taarifa zaidi za timu yenu ya muda zianze mapema ili siku ya siku muje uwanjani mkiwa 'full detailed'. Na katika hili mna baraka zangu zote, kwa roho safi.
  Tulianza na Kiyovu, ikaja zamu ya ES Setif, na sasa ni Al-Ahli Shandi ya mjini Shandi, Sudan.
  Karibuni wadau wa Yanga Afrika ya Umoja wa Mataifa, chama kongwe kabisa humu nchini na lililopigania Tanganyika huru.
  Habari kwa hisani ya: SPORTS IN BONGO: Simba kukwaana na Wasudani katika Raundi ya 3
  Picha kwa hisani ya:http://www.koorasudan.com/
  Taarifa za klabu kwa hisani ya:http://au.eurosport.com/football/teams/al-ahli-shandi/teamcenter.shtml
   
 2. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hamna shida, siye tutapeta na yanga mtaishia kunawa siye tunakula
   
 3. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  hivi lile pambano la frances cheka na stephano mwasika ni lini vile?nasikia pia tegete amekubali kupanda ulingoni kuzinyuka na japhet kasseba.
  Simba mpira Yangu masumbwi!
   
 4. M

  Masuke JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu Yanga watanunua sana jezi.
   
 5. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  kumbeeee!:nod:
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Nimewashauri hapo juu. Wasihangaike kununua jezi za Ahli, maana wanaweza kuvaa za Chelsea London na mambo yakawa mswano.
   
 7. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Hawana wasiwasi, Tibaigana atawapigania...
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Siku imefika na lile neno lipate kutimia.
  Way to go SSC!
   
 9. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kila la Heri Simba!
   
 10. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Simba kapakatwa pub
   
 11. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kila la heri All Ahly piga simba 8 bila.Kudadeki
   
 12. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Daaaah...!! Unauza sumu Mkuu?
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  ...bila shaka amepakatwa na jimama. Rahaaaaaa......
   
 14. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa sahihi mkuu, kwenye suala la kujiangusha, Ahli wameshinda 8-0!
   
 15. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  .....baadhi ya Wana Yanga wameanza kununua Jezi nyekundu kuelekea pambano la Mei 5, 2012.
   
Loading...