Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
Hicho kiatu kiliitwa raizoni (rise on) wengine walikiita platform. Viatu hivyo ilikuwa ni fasheni iliyopamba moto mwishoni wa 60's na mwanzoni wa 70's. Ilikuwa tunavaa raizoni, suruali za pekos na shati la slimfit. Kichwani tunachana afro. Hapo mambo yoote yanakaa sawa. Mkuki moyoni ilikuwa vile viatu vilivyokuwa na "ncha kali" mbele na tulivivaa sana miaka ya sitini (enzi za kucheza twist), bila kusahau kuchana way (wei) kwenye nywele. Vidosho walikuwa wanatumia bati la moto (lililotobolewa na misumari) kuchoma nywele ili ziwe laini kama za wazungu. We acha tu; hawa vijana wa sasa (akina Diamond) wanafikiri eti na sisi hatukutesa enzi zetu.Da! mkuu, umenikumbusha mbali sana.
Hiki kiatu kilikuwa chaitwa laizoni au mkuki moyoni.
Kama nakumbuka vizuri kiatu hiki kilitengenezwa kati ya mwaka 1983 au 1984 na kuingizwa madukani mwaka 1985...
samahani hivi kwa kipindi hicho hiyo redio ilikuwa shilingi ngapi.
UNAKUMBUKA ILIKUWA NI MWAKA GANI HIYO RADIO NA HICHO KIATU CHA RAIZONI? WENGI WATAFELI HAPO......
Mwaka huo 1984 nilikuwa bado kijana nina umri wa miaka 20 mkuu nimetumia hiyo Radio na hicho kiatu cha Laizoni ninakumbuka sana asante umekumbuka mambo ya zamani Old is gold.Da! mkuu, umenikumbusha mbali sana.
Hiki kiatu kilikuwa chaitwa laizoni au mkuki moyoni.
Kama nakumbuka vizuri kiatu hiki kilitengenezwa kati ya mwaka 1983 au 1984 na kuingizwa madukani mwaka 1985.
Nakumbuka maduka ya Bora lile la mtaa wa Samora na lingine lilikuwa pale Keko karibu na karakana za kutengeneza samani.
Ila hiyo Radio Cassette inanikumbusha Enzi ya Vijana Jazz na kaseti zao ambazo ilikuwa ni necessity wakti huo kujikumbusha.
Radio hizo zilikuwa ikiingizwa nchini na jamaa wa Matsushita Electric Company limited.
Mkuu, pia nawe unakumbuka "shati la ndege"? lilikuwa maarufu sana lile shati kiasi cha watu wengine kuuzuiwa makaratasi kwenye mfuko wakidhani wanauziwa shati hilo.
Nakumbuka mjomba wangu alinunua hiyo radiocassette kwa sh 1,800!samahani hivi kwa kipindi hicho hiyo redio ilikuwa shilingi ngapi.
Nakumbuka mjomba wangu alinunua hiyo radiocassette kwa sh 1,800!
Bwana mdogo we bado kinda!!Da! mkuu, umenikumbusha mbali sana.