Haya tuseme nchi imechukuliwa na Upinzani!

Osogoni ana point tuache kuwa pessimistic hatutafika tumeona kwa takribani kwa miaka 50 hatujafanikiwa kwasababu ya dhana hiyo. Tujaribu kudream kama Osogoni ninahakika rais atakuwa underpressure na hii ndo itatuendeleza. Tukumbuke bila kuwa na matumaini ya yajayo maisha yanakosa motivation na husababisha nchi kupiga marktime yaani kusimama palepale au kusonga mbele hatua chache tofauti na potentials zilizopo.
 
1.matajiri wapya wataibukia
2.ukabila
3.udini
4.mikataba mipya ya kuwafaidisha walio shika nchi
5.vita ya wenyewe kwa wenyewe
6.tutakuwa masikini mara mia ya sasa.
baba yake omr takuwa kafilisiwa na kutupwa korokoroni pamoja na mjomba,mpwa,shangazi na babu yake.
 
Tuseme nchi imechukuliwa na chama makini cha upinzani, unadhani katika kipindi cha kwanza cha Rais mteule nchi itakuwa katika hali gani kisiasa na kijamii?

Haya mambo ya kutabiri alikuwa anayaweza sana marehemu Sheikh Yahya Hussein. Kwa ufupi ni kuwa huwezi kutabiri nchi itakuwaje kisiasa na kijamii kwenye kipindi cha kwanza cha raisi mteule wa kufikirika.
 
Nchi hii ikichukuliwa na upinzani serikali itakuwa na kazi ya kupambana na waasi ccm, kwani hawatakubali kushindwa hivyo najua tu wataasi na kukimbilia porini kama Joseph konyi wa UG. ILA coz serikali itakayo ingia itakuwa makini tutawakimbiza kutokea huko maporini na nguo zao za kijani mpaka waingie kwenye Makalfati coz ndio maficho yao, simlimuona Gadafi? hah ha haa naisubiri sana hiyo siku yao ya kuchomolewa kwenye makalfati wakipewa ndosi na vichwa vya ukweli.
 
1.matajiri wapya wataibukia
2.Ukabila
3.Udini
4.Mikataba mipya ya kuwafaidisha walio shika nchi
5.Vita ya wenyewe kwa wenyewe
6.Tutakuwa masikini mara mia ya sasa.

Nilikuwa najua tu kuwa Masaburi at work, hili la udini liko ndani yako! Udini uko kwa utawala wa sasa yaani kwa kiongozi mmoja maana amekuwa tofauti na waliomtangulia. Hata hivyo kwenye suala la udini ukiangalia kwa jicho la umakini kabisa utakuta siyo sana tatizo la ccm kama chama ila kwa rais wao
 
Mtu mwenye busara na aliyekwenda shule hawezi kumkashifu mwingine ila anatoa mawazo mbadala, wewe ulitakiwa kutoa mrtazamo wako nchi itakuwaje endapo upinzani ukishinda that is how to build up discussion lakini ukiwa wa kushambulia wengine tu utakuwa bado husaidii taifa hili, come up wth uyour own vision!!
 
1.matajiri wapya wataibukia
2.Ukabila
3.Udini
4.Mikataba mipya ya kuwafaidisha walio shika nchi
5.Vita ya wenyewe kwa wenyewe
6.Tutakuwa masikini mara mia ya sasa.
Masaburi think tank!!
 
1. Tutaona katiba mpya ikiandikwa
2. maadili ya viongozi yakitekelezwa kwa vitendo.
3.Uchumi wa nchi ukipanda kwa kasi kwa kuwa neno ufisadi litafutika katika misamiati yetu
4. KIlimo kikipewa kipaumbele na kuondokana na tatizo la njaa kila mwaka
5.Elimu kwa wote hata wale wasio na uwezo wa kiuchumi kuipata.
6.Wtanzania kutokufa kwa magonjwa yanayotibika
7.Sayansi na teknolojia kumkomboa mtanzania
8.Soko la ajira kuongezeka kwa kasi sana.
9.Tatizo la umeme kuwa historia
10. Kufufuliwa kwa usafiri wa gari moshi.
11. Mikataba mibovu na ya kinyonyaji kufutwa na waliosaini kuwajibishwa
12.Walioiba mali ya umma kufilisiwa na kufikishwa mahakamani
13........
14.......
15.........

Namba moja na nne tu uko sawa, huko kwingine sijui unawaza nini!!!
 
20 . Wezi wa madini wakitoa mrabaha mkubwa bila kuombwa kufanya hivyo
21. Shimbo akihama nchi akifuatiwa na RA, BWM, ENL pamoja na Rz1.
22. Nyerere akienziwa kwa vitendo
23. CCM kikiwa chama cha upinzani
 
Kweli.. Ila umeuliza nchi itakuwa na hali gani. Patakuwa na utata kidogo kiuchumi,maana regime ikichange kutoka govt inayotegemea donors na wafanyabiashara wakubwa kwenda kwa govt mpya kunakuwa na woga..
 
Tuseme nchi imechukuliwa na chama makini cha upinzani, unadhani katika kipindi cha kwanza cha Rais mteule nchi itakuwa katika hali gani kisiasa na kijamii?
rais mteule nani? maana tusije tukawa tuajadili kumbe ww unamaanisha raisi mteule EL au 6.
 
1. Tutaona katiba mpya ikiandikwa
2. maadili ya viongozi yakitekelezwa kwa vitendo.
3.Uchumi wa nchi ukipanda kwa kasi kwa kuwa neno ufisadi litafutika katika misamiati yetu
4. KIlimo kikipewa kipaumbele na kuondokana na tatizo la njaa kila mwaka
5.Elimu kwa wote hata wale wasio na uwezo wa kiuchumi kuipata.
6.Wtanzania kutokufa kwa magonjwa yanayotibika
7.Sayansi na teknolojia kumkomboa mtanzania
8.Soko la ajira kuongezeka kwa kasi sana.
9.Tatizo la umeme kuwa historia
10. Kufufuliwa kwa usafiri wa gari moshi.
11. Mikataba mibovu na ya kinyonyaji kufutwa na waliosaini kuwajibishwa
12.Walioiba mali ya umma kufilisiwa na kufikishwa mahakamani
13........
14.......
15.........

Haya yanawekana kama sisiem watakubali kuachia kwa sababu hawapo tayari kabisa lkn ninavyoona lazima kwanza tuchinjane ndo kije kipindi cha mpito halafu ufanyike uchaguzi huru ndiyo mambo yatanyooka we anza kuandaa silaha tu za kupambana na polisi na wanajeshi
 
Kikwete na washikaji zake wote watatupwa rumande kusubiri kesi zao

watu weweeeeh. Japo ni assummption hapo Mwita25 umenikuna pamoja na kuwa sikuamin amin vizur baada ya kujivua gamba. Mana waweza kuta we ni ndumilakuwili ka baba riz.
 
Tuseme nchi imechukuliwa na chama makini cha upinzani, unadhani katika kipindi cha kwanza cha Rais mteule nchi itakuwa katika hali gani kisiasa na kijamii?

Hali km hii yaweza kutoka mwaka 3035, tujiandae huko
 
Hapo ndo hua nawaonea huruma my fellow Tanzanians.... Dhana na imani ya kusema kwamba kitakapo kuja chama kipya na utawala mpya basi kila kitu kitakua for the best... Haya mambo hayafanywi in one day yakanyoka... Yanahitaji mda for "Change" Ku-prevail ipasavo... Mfano tu hilo suala la mikataba, huwezi vunja mikataba bila kwanza kupitia uone tatizo lipo wapi... na ukishaona tatizo kwanza kuichora upya na kuandika mipya ambayo ni kwa maslahi ya nchi yaweza chukua forever.....

Wezi wa rasilimali za nchi msikatishe watu tamaa, Tanzania inahitaji change of the system basi, tengeneza institutions zinazofanya kazi na zinazowajibishwa. Ondoa habari ya raisi kuteua kila mtu kasoro mwanamke wa kuoa ndipo utakapoona mabadiliko makubwa na ya kasi.

Nchi ni tajiri kupindukia ila imekaliwa na wezi, change this system TZ will be an economic giant in Africa.
 
Kikwete na washikaji zake wote watatupwa rumande kusubiri kesi zao

Hizi ndoto hizi mh! mpinzani akiingia na katiba hii atapata kigugumizi kuibadilisha kwani itakua inampa manufaa yeye ya kujilinda na kuhifadhi na kuukinga utawala wake na wapinzani walio nje ya dola sasa. unakumbuka Kibaki na ahadi ya siku 100 za kubadili katiba hapo 2002? imechukua damu na maisha ya wengi na serikali ya umoja wa kitaifa kubadilisha katiba kenya nchi yenye muamko wa kisiasa kuliko TZ.

mafisadi wachache wataadabishwa kwa hukumu za kiushikaji au kurudisha mali, lakini mfumo wao utaendelea kubaki na mianya hiyo hiyo kutumiwa na watawala wapya kwa sababu wamiliki mfumo wa kifisadi au walionufaika na mfumo huo ni wengi na ndiyo wanaoshikilia uchumi sasa mpinzani na ahadi zake luluki kwa kipindi kifupi hatotaka kuwaudhi hawa wakuu wa mfumo wa kifisadi na kuutingisha na kuyumbisha uchumi kwani miaka 5 ni michache ukijifanya unabadilisha kil kitu na results zinategemewa miaka 10-15 utatupwa nje bora kuziba ziba viraka hapa na pale na kuendana na wale walioshikilia uchumi (hata Satta ameshindwa kuwafukuza wachina Zambia ameishia kuwaambia wafuate sheria ya uajiri wakati ilisemekana angewafukuza na kutaifisha miradi yao) Huwezi kubadilisha . the verdict mambo yatabadilika kidogo ila mengi yatabaki yale yale.

Complete overhaul of the system uletwa na mapinduzi ya nguvu na siyo ya kisanduku cha kura
 
Back
Top Bottom