Haya sasa, aliyeonyesha dole msafara wa Trump afukuzwa kazi!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,782
5c3f2ce6-c313-11e7-bcc4-77f3d6fc373e.jpg

Ilikuja habari hapa na watu kuanzia kusifia mwanamama aliyekuwa kwenye baiskeli na kuuonyeshea msafara wa Raisi wa USA kidole cha kati, sasa huyu mama Juli Briskman amefukuzwa kazi kwa kitendo hicho, Waafrika hatuwaelewi Wazungu ingawaje tunafikiri tunawaelewa!

Huyo mama alipata mashabiki hapa kwamba ni demokrasia na sisi tuige, lkn wakati huwo huwo hao wanaosifia kwamba ni demokrasia hakuna alitetayari kumuonyeshea Babake kidole cha kati.

Source: Woman who gave Donald Trump the middle finger fired from her job
 
Ilikuja habari hapa na watu kuanzia kusifia mwanamama aliyekuwa kwenye baiskeli na kuuonyeshea msafara wa Raisi wa USA kidole cha kati, sasa huyu mama Juli Briskman amefukuzwa kazi kwa kitendo hicho, Waafrika hatuwaelewi Wazungu ingawaje tunafikiri tunawaelewa!

Huyo mama alipata mashabiki hapa kwamba ni demokrasia na sisi tuige, ...
Akina Salary Slip na Allen Kilewella wamejificha. Wanaogopa kutokea hapa.
 
Ilikuja habari hapa na watu kuanzia kusifia mwanamama aliyekuwa kwenye baiskeli na kuuonyeshea msafara wa Raisi wa USA kidole cha kati, sasa huyu mama Juli Briskman amefukuzwa kazi kwa kitendo hicho, Waafrika hatuwaelewi Wazungu ingawaje tunafikiri tunawaelewa!

Huyo mama alipata mashabiki hapa kwamba ni demokrasia na sisi tuige, lkn wakati huwo huwo hao wanaosifia kwamba ni demokrasia hakuna alitetayari kumuonyeshea Babake kidole cha kati, ...
Ningeshangaa km asingechukuliwa hatua.

Democracy gan iyo yakumtusi kwa matendo Rais???

Mchezaji tuuu akionyesha dole anafungiwa ..sembuse Rais!!!
 
Ni vizuri tuwe tunajiridhisha kwenye mambo huyo Mama amefukuzwa na kampuni yake bila shinikizo la serikali ila ni kwamba kampuni uliona ameweka ile Picha ya kutukana kwenye Facebook page yake na taratibu za kampuni ni kutoweka Picha za namna hiyo.
Hivyo wameamua kumfukuza kazi ingawa inawezakana pia anaweza kuwafungulia mashtaka kwa double standard kutokana kuna mfanyakazi wa kiume amewahi kutukana mfanyakazi mwenzie kwenye Facebook page yake na akapewa warning tu.
 
Fukuzo halikuwa government action.

Sidhani kama unaweza kunielewa.

Rekebisho la Kwanza la Katiba ya Marekani linasema:

Bunge halitatunga sheria inayohusu kuanzisha dini, au kuzuia kuiabudu; au kukinza uhuru wa kusema, au wa tasnia ya habari; au haki ya watu kukusanyika kwa amani, na kudai Serikali itatue kero.
 
Watu walisifia kwasababu hakuchukuliwa hatua yoyote na serekali au polisi. Kufukuzwa kazi ni maamuzi ya kampuni.
Freedom of Speech...not freedom from consequences. Huyo mama ana uhuru wa kijieleza na hiyo kampuni ina uhuru wa kumtimua kazi.
 
Ni vizuri tuwe tunajiridhisha kwenye mambo huyo Mama amefukuzwa na kampuni yake bila shinikizo la serikali ila ni kwamba kampuni uliona ameweka ile Picha ya kutukana kwenye Facebook page yake na taratibu za kampuni ni kutoweka Picha za namna hiyo.
Hivyo wameamua kumfukuza kazi ingawa inawezakana pia anaweza kuwafungulia mashtaka kwa double standard kutokana kuna mfanyakazi wa kiume amewahi kutukana mfanyakazi mwenzie kwenye Facebook page yake na akapewa warning tu.

Hata akiwafungulia mashitaka hatafika mbali.

Mambo ya at-will employment hayo. Mwajiri anaweza kukuachisha kazi muda wowote, kwa sababu yoyote [ukiondoa labda ubaguzi wa rangi, dini, jinsia, au asili ya utokako], au hata bila sababu yoyote ile.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom