Haya ni mazungumzo ya watanzania ndani ya daladala leo asubuhi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya ni mazungumzo ya watanzania ndani ya daladala leo asubuhi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mama D, Aug 16, 2011.

 1. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145


  Nimepanda daladala saa moja kamili asubuhi hadi nafika saa mbili na robo mazungumzo yalkua yanahusu


  1.Kutumika helkopta katika kukarabati njia za umeme.

  2.Raisi wa mambo ya nje

  KuhusuKutumika helkopta katika kukarabati njia za umeme. wananchi walichangia kama ifuatavyo......

  • Kwanini vijana wa kitanzania wenye ujuzi wakisaidiana na wasio na ujuzi (vibarua) wasitumike kufanya hiyo kazi.
  • Mafisadi wameamua kutumia njia ya helikopta ili waweze kujilipa mamilioni.
  • Serikali imekufa hakuna serikali wala viongozi wa serikali tanzania
  • Hiyo ni janja ya nyani sawa na walivyoamua kuibana ewura kwa maslahi ya biashara zao za mafuta maana hamna hohehahe mwenye biashara kubwa kama ya mafuta
  • Mwingine akasema inawezekana kuna mtu mkubwa serikalini anatakuuza mafuta ya ndege kwa wingi ndio katengeneza huo mchakato
  • Na mwingine akasema hata umeme kukosekana ni deal maana wameingiza makontena ya majenereta ya uwezo tofauti yako bandarini sasa wanakata umeme ili waweze kuuza jenereta zao.

  Kuhusu Rais wa Tanzania......Hoja ilkua kubwa na watu walkua na hasira katika kuliongelea hili wakitumia lugha kali zilizoashiria hasira zao
  • mchangiaji aliekua na hasira sana alisema kwa sauti kubwaaa..... HAKUNA RAISI WA TANZANIA ILA YUPO RAIS WA MAMBO YA NJE YA TANZANIA.............
  ****NIKAWA NIMEFIKA NILIKOKUA NAENDA NA KUACHA MJADALA UKIENDELEA.****

  Sijui kama serikali inatambua kuwa imekalia kuti kavu......tena linalowaka moto jangwani.

  Ila nimegundua elimu ya uraia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.......inapendeza kuona watanzania wanajadili mambo ya msingi yanayohusu nchi na maisha yao kila wanapokutana na kuwa na muda ..... hata ndani ya vyombo vya usafiri.
   
 2. C

  Chumvi1 Senior Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 137
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  popote pale kunapokuwa na group kubwa ya watu sasa hivi Tanzania ukianzishwa mjadala kuhusu serikali ya kikwete watu huwa wanaropoka, watu wameelewa maana hata hao ccm wenyewe wanaona wameingia chaka.
   
 3. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwani Kikwete amebakisha muda gani kuachia Urais?
   
 4. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kazi ipo
   
 5. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Babu yangu mwenyewe ni mwana ccm dam,anawalaani viongozi wote wa ccm kwamba wako humo kwa maslahi ya matumbo yao,na ameapa kwamba kama atakuwa hai hatathubu kumpigia kura mgombea yeyote wa ccm,kura yake itaenda upinzani ila ahami chama na mikutano yao atahudhuria kama kawaida ila KURA HAWAPATI TENA.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wengine sasa wanamwombea kifo
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mi mwnyw leo nimepanda hiace toka sakina mpaka ngaramtoni hakika hakuna kinachojadiliwa zaidi ya hali mbaya serikali na ukizingatia kipindi kilichokuwa hewani kwenye redio iliyokuwa inasikika ni ISEMAVYO MAGAZETI kila m2 aliongea kwa jazba ya namna yake na nikamsikia mama mmoja wa makamo tu akisema kwanini Mwalimu Nyerere asifufuke? Akasema kwa hasira na akaanza kumwomba MUNGU na wa2 wote wakaiponda chama cha mapinduzi na wakisema mwenye chama wamemuua waweze kufaidi na ndiyo nikateremka sehemu wanapaita Kibaoni nikiacha mjadala ukiendelea. Ila hakika Watanzania wamechoka na serikali iliyoko madarakani kabisa.
   
 8. b

  boybsema Senior Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mafisadi wakubwa...akina SSM ni akina nani tena hao??????????
   
 9. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nina shaka. Umewezaje kuweka mazungumzo yote hapa?
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Watu wana machungu sana na nchi yao.<br>Tatizo akina mama ndo wanatuangusha ukifika uchaguzi ndo wa kwanza kupokea ugua pole kama khanga, t shirt, kofia na zile buku 2000-5000 alafu utasikia huyo huyo apite mwisho wa siku wao ndo wanateseka kwa kurubuniwa na wanasihasa.
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  `nimegundua kumbe wanaotakiwa kujivua gamba la uzoba ni wananchi`by KP
   
 12. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,716
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  mashaka yako nini ni kuwa haiwezekani kuweka haya mazungumzo hapa? kwa teknolojia yote hii m2 ashindwe kuweka mazungumzo ajabu unaweza rekodi ukifika ofisini unasikiliza anaandika just like mwandishi wa habari, pia kama kichwa kiko powa nadhani kama cha mtoa mada kilivyo unaandika mawazo yote kwa maneno yako c lazima uandike exactly walichokuwa wanazungumza. kifupi wananchi uelewa umekuwa sana wanahoji kila tendo na pongezi kwa vyombo vya habari vinafanyna kazi yake vizuri (baadhi!), mwananchi hatanunua gazeti ila anaweza akasikia yakisomwa kwenye redio!
   
 13. gwino

  gwino JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tupo kwenye mapito y kujifunza na kujutia makosa tulofanya kuwaweka madarakani hawa wanyonyaji
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  wewe mama d vipi?

  mimi hapo nidsingeshuka mpaka mwisho wa basi..
  halafu ningapanda la kurudi..
   
 15. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hao wanaolalamika ndiyo haohao waliomchagua mkuu. Ni wanafiki wasiojielewa wanachokinena na wamepumbazwa na upepo wa kisiasa kiasi cha kuvimbiwa ulimbukeni wa utopia. Wao wanafikiri kwamba maisha bora huja kwa kupiga umbeya na uzushi.
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Naungana na walalamikaji.
   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nimependa huyo aliyesema hatuna rais wa Tz bali tuna rais wa mambo ya nje ya Tz... Amepatia mpaka raha... Tz kweli hakuna rais kuna Vasco Dagama!
   
 18. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Walichagua wenyeweeee na wanaumizwa wenyeweee kwa ukilaza wao asilimia kubwa ya wapiga kura ni watu wa kawaida sana wasiokuwa na akili ya kufanya maamuzi sahihi wenye uwezo huo ni wachache na hawana muda wa kupiga kura juzi nlikuwa naongea na jamaa yangu nikamuuliza ulipiga kura mwaka jana akanijibu kuwa hana muda mchafu wa kupoteza ye alikuwa bize kutengeneza hela tu siku hiyo sasa watu kama hawa ndo waelewa halafu kura hawapigi halali yao kuumizwa!!!!!
   
 19. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Mazungumzo haya ya kuonyeshwa kukatishwa tamaa na Serikali iliyoko madarakani hayakuanza leo,
  Toka kabla hata ua uchaguzi na bado matokeo ya uchaguzi tumeyaona,
  Sijui tunakosea wapi Tanzania, something went wrong but hatujui ni nini hiyo?
   
 20. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  natamani siku moja hilo lindege limmalizie huko angani

  kazi kuzurura hovyo nchi za watu huku nchi yake ikiteketea
   
Loading...