Haya ni maoni yangu tume ya katiba,je wewe mtumiaji wa jf umeshatuma maoni yako?

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,151
2,000
Wadau nimetuma maoni haya ktk tume ya katiba,nanyi ni ruksa kutuma yenu usikopi yangu,nimeweka hapa kuwapa hamasa tu kuwa kumbe inawezekana.


1.KUSIWE NA VYEO VYA WAKUU WA WILAYA
2.MAWAZIRI WASITOKANE NA WABUNGE WATEULIWE NJE YA WABUNGE
3.WAZIRI ATEULIWE KUTOKANA NA ELIMU YAKE MFANO,WIZARA YA SHERIA WAZIRI AWE AMESOMA SHERIA,AMA WIZARA YA ELIMU WAZIRI AWE MWALIMU
4.RAIS APUNGUZIWE MAMLAKA,MFANO RAIS AMEPEWA MAMLAKA MAKUBWA SANA KTK TUME ANAZOZIUNDA NA ANAWEZA KUKUBARI AMA KUKATAA USHAURI AMA UCHUNGUZI ULIOLETWA NA TUME ALIYOIUNDA,HAPO KUNA ONDOA UMUHIMU AMA MALENGO YA KUUNDA TUME ZA KICHUNGUZI KAMA RAIS ATAKUWA NA CHAGUO LA KUKUBARI AMA KUKAA UCHUNGUZI HUO
5.MUUNGANO UWE WA SERIKALI MOJA NA KUWE NA RAIS MMOJA TU WA MUUNGANO/KUWE NA SERIKALI TATU YAANI YA ZANZIBAR,TANGANYIKA NA MUUNGANO ILI KILA NCHI IWE NA MAMLAKA NA MAAMUZI KTK MAMBO YAKE
5.ARDHI IMILIKIWE NA SERIKALI NA IWE NA MAMLAKA YA KUPANGA MATUMIZI YA ARDHI HIYO NA HII ITAKUWA NI RAHISI KWA SERIKALI KUTUMIA ARDHI WAKATI WOWOTE ULE WATAKAO,TOFAUTI NA SASA MTINDO HUU UNATUMIWA NA UCHINA NA MIPANGO MIJI INAONEKANA VYEMA KWANI SERIKALI NDIO YENYE MAAMUZI YA MWISHO
6.MADARAKA YA KUTANGAZA HALI YA HATARI YASIPITIE KWA WABUNGE NA HATA KAMA YATAPITIA WAPEWE SIKU MOJA TU KUFANYA MAAMUZI KWANI TUNAVYO ONGELEA HALI YA HATARI INAMAANISHA NI HATARI YEYOTE ILE,INAWEZEKANA KUKAWA NA VITA JE HAO WABUNGE WATAPATA WAPI MUDA WA KUKAA NA KUPITISHA OMBI HILO? RAIS AMBAYE NDIO AMILIJESHI MKUU APEWE MAMLAKA YA MOJA KWA MOJA KUTANGAZA HALI YA HATARI PASI YA KUPITIA MILOLONGO MIREFU HADI BUNGENI
7.UMRI WA MTU KUGOMBEA URAIS USIWE MIAKA 40 UWE KUANZIA MIAKA 35 NA KUENDELEA LAKINI NI LAZIMA MGOMBEA URAIS AWE NA ELIMU ANGALAU YA CHUO KIKUU
8.UKOMO WA RAIS NA WABUNGE UWE NI WA MIAKA MINNE TU NA SI MITANO
9.HIKI PENGELE "(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidikuliko mgombea mwingine yeyote."KIONDOLEWE NA MSHINDI WA URAIS NI LAZIMA AFIKISHE ASILIMIA 50 YA KURA ZOTE ZILIZOPIGWA NA IKISHINDIKANA BASI KURA ZIRUDIWE KWA WALE TU WAGOMBEA WALIOKARIBIANA.
9.HIKI KIPENGELE PIA KIONDOLEWE"(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzikwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basihakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake" NA PINDI ITAKAPO ONEKANA KUNA TATIZO KTK KURA ALIZOZIPATA RAIS NI VYEMA KUWE NA UHURU WA KUPINGA AMA KUCHUNGUZA MATOKEO HAYO MAHAKAMANI AMA KUWE NA TUME YA KUFANYA UCHUNGUZI HUO.
10.KTK MADARAKA YA KUTANGAZA VITA,TANGAZO HILO HALINA HAJA YA KUUNGWA MKONO NA WABUNGE NA TENA KUSIWE NA SIKU 14 ZA KUPIGA KURA ZA KUUNGA MKONO TANGAZO HILO KWANI MAADUI HAWATAKUWA NA MUDA WA KULISUBIRI BUNGE LIFANYE MAAMUZI,NI VYEMA PINDI RAIS AKISHA TOA TANGAZO HILO KTK MAMLAKA HUSIKA HATUA YA HARAKA ICHUKULIWE ILI KUWEZA KULINDA USALAMA WA NCHI,WATU NA MALI ZAO MAPEMA IWEZEKANAVYO
11.KUHUSU "Kinga dhidi ya mashataka ya madai,"ILI KUONDOA ILE TABIA YA MARAIS KUFANYA MAKOSA HUKU WAKIJUWA KUWA WANALINDWA NA KINGA,NI VYEMA KUWE NA SHERIA YA KUMSHITAKI RAIS PINDI TU ATAKAPOFANYA KOSA AKIWA KAMA RAIS NA KOSA HILO LIKAISABABISHIA NCHI KUINGIA KTK MATATIZO MAKUBWA ASHITAKIWE KWA MAHAKAMANI NA WAKATI AKIWA ANASUBIRI HUKUMU NAFASI YAKE ISHIKWE NA MAKAMU WA RAIS,MAANA RAIS ANAWEZA UZA AMA KUINGIA MIKATABA MIBOVU AMBAYO ITAIGHARIMU NCHI,HATUNA HAJA YA KUSUBIRI HADI ATOKE MADARAKANI,NI VYEMA SHERIA IKAFANYA KAZI YAKE HATA KAMA BADO YUPO KTK UONGOZI,HII ITALETA NIDHAMU KTK NAFASI HIYO NA KUWAFANYA MARAIS WAWE MAKINI NA MAAMUZI YAO.
12."(5) Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika mahakama yoyote."KAMA MAWAZIRI WAMEMSHAURI VIBAYA RAIS NI VYEMA SWALA HILO LIKAPEWA NAFASI YA KUHOJIWA AMA KUCHUNGUZWA ILI KUBAINI KAMA HAKUKUWA NA USHAURI WENYE KULENGA UPENDELEO WA WAZIRI AMBAE LABDA ANA MASLAHI BINAFSI,KUWEPO KWA KIPENGELE HICHO KUNALENGA KUWAPA NAFASI MAWAZIRI KUMSHAURI RAIS HATA SWALA AMBALO LINAMASLAHI KWAKE YEYE KAMA WAZIRI AMA KIKUNDI CHA WATU WACHACHE WALIOMTUMA
13.ILI KUWEZA KUWA NA MGAWANYO SAWA WA KAZI ZA SERIKALI KWA WATANZANIA ZAIDI YA MILIONI 45,NI VYEMA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WASITOKANE NA WABUNGE ILI TUWEZE KUWAACHA WABUNGE WASHUGHURIKIE MATATIZO YA WANANCHI WALIOWACHAGUA NA KUACHA KAZI ZA UWAZIRI NA UNAIBU KUSHIKWA NA WATU BAKI KWANI INAONEKANA MBUNGE AMBAYE NI WAZIRI ANAPATA MISHAHARA MIWILI KWA WAKATI MMOJA NA KUMBE INAWEZEKANA BASI KAZI HIYO YA UWAZIRI NA UNAIBU WAKAPEWA WATU WENGINE WENYE UWEZO NA WEREDI TENA WENYE FANI HUSIKA ILI KUONGOZA WIZARA HUSIKA.
13.SI LAZIMA MGOMBEA URAIS,UBUNGE,UDIWANI,AWE NA CHAMA,NI VYEMA TUKAWA NA MGOMBEA BINAFSI HII ITASAIDIA KUONDOA ILE MIGONGANO NA NJIA NGUMU ZA KUWAPATA WAGOMBEA KUPITIA VYAMA VYA SIASA,NA MUDA MWENGINE UTAKUTA MGOMBEA MWENYE SIFA HUACHWA LABDA KUTOKANA NA UKILITIMBA ULIOPO KTK VYAMA.
14.MUDA WA MBUNGE KUSHIKA MADARAKA UWE NI MIAKA MINNE TU KAMA YA RAIS NILIVYOPENDEKEZA HAPO JUU.
15.Tume ya Uchaguzi IWE HURU,VIONGOZI WAKE WASICHAGULIWE AMA KUTEULIWA NA RAIS HII INASABABISHA WALIOTEULIWA NA RAIS KUSHINDWA KUFANYA AMA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO VYEMA KWA KUHOFIA KIBARUA CHAO KUTOKA KWA MTU ALIYEWATEUWA,NI VYEMA VYAMA VYOTE VYA SIASA ,MAKUNDI YA JAMII MBALIMBALI WASHIRIKI KUUNDA TUME HURU YA UCHAGUZI,HII ITAPUNGUZA MANUNG'UNIKO KWA JAMII NA KUIFANYA TUME KUFANYA KAZI YAKE PASI YA KUPENDELEA KUNDI AMA CHAMA CHOCHOTE KILE
16.SPIKA ASIWE MBUNGE,KWA KUWA BUNGE NI MUHILI MMOJA WAPO UNAOJITEGEMEA BASI NI VYEMA KUKAWA NA WAFANYAKAZI WA MUHIMILI HUO KAMA ILIVYO KWA MAHAKAMA,SPIKA AWE NI MMOJA WA WAFANYAKAZI WA MUHILI WA BUNGE KAMA VILE KATIBU WA BUNGE SI MBUNGE,WAFAGIAJI SI WABUNGE,MASAJENTI WA BUNGE SI WABUNGE,NA SPIKA PIA ASITOKANE NA WABUNGE IWE NI KAZI KAMA KAZI NYINGINE NA YENYE KIKOMO CHAUSTAHAFU,LAKINI PIA SPIKA AWE MTU MWENYE ELIMU ANGALU YA CHUO KIKUU KTK MASWALA YA SHERIA,NA HII NI KWA WOTE,IWE NAIBU SPIKA N.K.LENGO NI KUWAACHA WABUNGE WAFANYE KAZI WALIZOTUMWA NA WALIOWAPA KURA NA NAFASI YA USPIKA IWE NI YA KUDUMU KAMA NILIVYO ELEZA HAPO JUU
17.DPP AMEPEWA MADARAKA MAKUBWA SANA JUU YA HAKI ZA WASHITAKIWA KUPEWA DHAMANA,KWANI ANAWEZA KUZUIA DHAMANA HIYO PASI YA KUTOA SABABU YEYOTE ILE,WAKATI KISHERIA DHAMANA NI HAKI YA MSHITAKIWA NA KIKAWAIDA HUKUNA JAMBO LISILOKUWA NA SABABU,NI VYEMA IKAWA WAZI NA DPP ATOE SABABU MAALUMU ZA KUZUI DHAMANA KWA MSHITAKIWA YOYOTE YULE,TOFAUTI NA SASA KUWA HATAKIWI KUTOA SABABU KWA NINI KAZUIA DHAMANA.
18.RAIS,WABUNGE NA BAADHI YA WAKURUGENZI WAPUNGUZIWE KIINUWA MGONGO,KWA MFANO MBUNGE ANAFANYA KAZI KWA MIAKA MITANO TU NA BAADA YA UKOMO WA UBUNGE ANAPATA ZAIDI YA MILIONI 40 KAMA KIINUWA MGONGO HII SI SAHIHI NA NDIO INASABABUSHA WASOMI WETU KUACHA KAZI ZAO NA KUKIMBILIA MASLAHI MAKUBWA KTK NAFASI YA UBUNGE,KUWE NA SHERIA MAALUMU ITAKAYOWEKA WAZI NA KUWABANA WABUNGE,RAIS NA BADHI YA WAKURUGENZI KUTOPATA KIWANGO KIKUBWA CHA PESA KAMA KIINUWA MGONGO
19.MIKATABA YOTE IWE YA MADINI,UMEME AMA MANUNUZI YA KISERIKALI IWE WAZI KWA WANANCHI ILI KUWEZA KUWASHIRIKISHA WANANCHI KUELEWA NINI KIMETENDEKA KTK MKATABA HUSIKA,NI VYEMA KTK KATIBA HII KUWE NA KIPENGERE KITAKACHO ELEZEA KUWEPO KWA UWAZI WA MIKATABA YOTE,MAANA USIRI WA MIKATABA UNASABABISHA WATENDAJI WA SERIKALI NA SERIKALI KUINGIA MIKATABA HATA ISIYOKUWA NA MANUFAA KWA UMMA.
20.KATIBA IELEZE BAYANA JUU YA WALA RUSHWA NA TUWE NA SHERIA YA KUWAPA ADHABU KARI MFANO MLA RUSHWA ATAHUKUMIWA KUNYONGWA LAKINI PIA ADHABU ZIFUATAZO ZITAENDELEA WAKATI AKISUBIRI KUNYONGWA KUFIRISIWA MALI ZAO NA KUTOPATA TENDA NDANI YA TANZANIA NA HATA KULIPA FIDIA KWA KOSA HILOHILO LA ULAJI RUSHWA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom