Haya ni mambo ambayo unapaswa kuyaepuka sana hasa ukiwa kijana unayetegemewa na familia na taifa pia

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
1. Kutoatoa sababu au kuwapa lawama wengine mambo yako yanapokwenda kombo. Utasikia mtu oh magufuri amebana, mimi nina mkosi. Hizi ni sababu za kitoto sana. Napenda tabia ya simba. Kuna wakati huwa anapoteza maisha katika kutafuta chakula. Mara nyingine simba huugua baada ya kupigwa lakini hakati tamaa kuwinda. Ukiona mambo yako hayaendi jipange tena wala usilaumu wengine. Hata mkuu vipi lazima wanetu washibe na waende shule

2. Usisahau kuwa Sababu nyingi huwa hazileti uaminifu. Tumekubaliana kufanya jambo. Inafika wakati unaanza kutoa sababu nyingiii. Hizi mara nyingi huwa hazisaidii zaidi ya kukuonyesha kuwa hutunzi ahadi. Mmepanga dili inafika siku ya mwisho mtu anaanza kuleta sababu. Mimi hapo nitakwambia sawa ila huji kupata dili kwangu. Ugumu upo na dharura zipo ilq lazima mambo yote yaende.hata mwalimu akifundisha vibaya kafaulu na kufeli kupo pale pale
3. Usisahau mwisho wa siku watoto wanatakiwa kushiba na sio baba hajapandishwa cheo au hajapata safari ya kikazi. Kanuni iko hivi kazi hutangazwa kwa mwenye elimu na sio ambaye hakusoma sababu baba yake alikuwa mlevi au hakuwa na hela. Watu hawaangalii sababu zako. Watoto wakiwa na njaa hawatashiba sababu zako. Ishu ni moja. Pambana, pambama na timiza ahadi na malengo. Bora ufe unapambana kwa uadilifu na haki ukiwa umeshiba na watato wameshiba kuliko kufa njaa. Mwisho wa siku sababu hazishibishi mtu wala hazimpeleki mtu hospitali

4. Kutegemea kuhurumiwa ili usaidiwe. Duniani hapa hakunaga cha bure. Nimejifunza hilo sana. Jitetee sana lakini hakuna kinachokuja bure. Biblia haikukosea iliposema sisi wanaume tutakula kwa jasho. Tafuta huruma hizo na mwisho wa siki utaishia huzunii

5.usiache kuweka moyoni hili kuwa kuishi kwa kutegemea ndugu ni sawa na kuchimba kaburi na kujizika mwenyewe na familia yako kabisa. Kumbuka hakuna mtu anayeweza kumpenda mwenzake zaidi ya nafsi yake. Ndugu atakusaidia lakini sio zaidi ya uwezo wake au kuliko familia yake. Pia jua hakuna aliyezaliwa kwa ajili ya mtu mwingine. Lazima kila mtu ahibidishe na ndio msaada uje.

6. Kusubiri muujiza bila kujibidiisha ni sawa na kusubiri mvua ya mawe jangwani, au kusubiri meli jangwani. Musa hakuyaangalia maji ya bahari ya shamu. Aliyachapa kwa fimbo. Wewe imba sana huku.hufanyi kazi uone muujizi wa ndoto za mchana unavyokuja. Utaishia kusimulia wakina dangote ba mengi huku njaa inakuumiza kweli.
 
Nzuri sana, ujumbe umefika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom