Uchaguzi 2020 Haya ni mambo 10 niliyoona kwa CCM Vs CHADEMA mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,640
33,421
Wakuu,

1) What a match !, Mpaka sasa CCM inabebwa na watu wenye experience ambao kipindi kama hiki ndio unajua uwezo wao. Wao kelele nyingi ziko kwenye mipango (strategies) kuliko kelele na matamko ya majukwaani.

2) Tundu Lissu is impressive as usual lakini seems Chadema hawakumuandaa, experience yake ya uanaharakati ndio unaofanya aonekane active uwanjani lakini bado hajawa na madhara kihoja ingawa bado mapema. Mambo ya kusema atamshtaki JPM kwa rushwa ya kununua jogoo laki moja ni uanaharakati si level zake tena kama mgombea Urais.

3) John Pombe Magufuli yuko composed sababu ya records zake awamu hii ya kwanza. Lakini pia kwasasa nguvu kubwa ipo kwenye kupanga vyema mabeki Majimboni na Udiwani. Hapo ndio unapoona timu kubwa na yenye watu wazoefu inavyohandle mchezo. Ni kama wameamua kuacha wapinzani wacheze huku wao wakikamilisha ramani ya ushindi.

4) Kimbinu Chadema wanahitaji timu bora kumzunguka Lissu wakiwemo waandamizi wa serikali zilizopita akiwemo Nyalandu ili kumshape Lissu kama Mgombea Urais lakini pia mipango ya kusaidia kampeni Majimboni ambako hali si nzuri

5) Kimbinu CCM wana kazi kubwa ya kumaliza mchakato wa wagombea Ubunge na Udiwani bila mpasuko lakini maeneo mengi kimbinu wamejipanga kushinda.

6) John Pombe Magufuli takwimu zinambeba na wananchi wanajua matokeo yake wakimchagua tofauti na Lissu ambaye anapaswa kujikita kwenye hoja zenye matarajio ya wananchi hasa wanyonge walio wengi. Je ataweza kuaminisha wananchi ili wamchague?

7) Financially CCM wako stable kuhandle kampeni kuliko CHADEMA ambayo imepanga pia kusimamisha wagombea majimbo yote.

8) John Pombe Magufuli amefanikiwa kuhakikisha watendaji wake wote wanajua takwimu za mambo yaliyofanyika awamu hii hivyo itabidi kila hoja za Lissu zinazogusa takwimu ajipange otherwise akikosea atapingwa hata na Makatibu Tarafa. Hizo takwimu zimeimbwa muda mrefu na hata wananchi wengi wamezikariri.

9) Angalizo, Lissu usihangaike na wimbo wa katiba mpya hauna mashiko kwa wananchi wanyonge na hautampa kura. John Pombe Magufuli pia awekeze hoja kwenye mipango mipya hasa mapinduzi kwenye kilimo na uwekezaji.

10) Wapinzani bila kusimamisha mgombea mmoja huu utakuwa uchaguzi mgumu hadi majimboni kuliko wakati wowote.

Mizania pima mwenyewe, hayo ni maoni yangu binafsi
 
Tunashukuru na tunaheshimu maoni yako, ni kweli cdm wanaweza kuwa hawajajipanga vizuri, ila hukuhitaji kuweka sababu zote hizo, maana uchaguzi wa sasa hivi utafanyika kwa utashi na maamuzi ya madaraka ya Magufuli.

Subiri kadiri joto la uchaguzi linavyopanda, kama hujaona yale aliyoagiza kufanyika kwenye chaguzi zote za marudio na uchaguzi wa SM kujirudia. Naona unataka kutuaminisha huko ccm kuwa kuna mbinu sana, wakati maamuzi yote ya uchaguzi huu anayo Magufuli.
 
Tunashukuru na tunaheshimu maoni yako, ni kweli cdm wanaweza kuwa hawajajipanga vizuri, ila hukuhitaji kuweka sababu zote hizo, maana uchaguzi wa sasa hivi utafanyika kwa utashi na maamuzi ya madaraka ya Magufuli. Subiri kadiri joto la uchaguzi linavyopanda, kama hujaona yale aliyoagiza kufanyika kwenye chaguzi zote za marudio na uchaguzi wa SM kujirudia. Naona unataka kutuaminisha huko ccm kuwa kuna mbinu sana, wakati maamuzi yote ya uchaguzi huu anayo Magufuli.
Noted well mkuu
 
Hivi huyo magufuli takwimu gani zinambeba?

Hali ya kiuchumi Kwa wananchi ikoje? Kwa wakulima wa mbaaazi, korosho, tumbaku takwimu zikoje?

Suala la ajira kwa vijana kafanya nini? Ameua uwekezaji na sekta binafsi kaishia kufanya maelfu ya vijana kuwa jobless na watu kupoteza ajira

Ameua watu, kubambikia watu makesi, kuonea watu mpaka hata watoto wadigo wanajua

Ameharibu biashara kupelekea watu kufunga biashara zao na wengine kufirisiwa na mabenki?

Huyo magufuli kafanya ya nini zaidi ya haya? Njia ni nyeupe sana kwa Tundu Lissu mwaka huu.
 
Ahsante sana Mkuu. Uko vizuri sana. 👊🏽👍🏽
Hivi huyo magufuli takwimu gani zinambeba???!

Hali ya kiuchumi Kwa wananchi ikoje? Kwa wakulima wa mbaaazi, korosho, tumbaku takwimu zikoje?

Suala la ajira kwa vijana kafanya nini??? Ameua uwekezaji na sekta binafsi kaishia kufanya maelfu ya vijana kuwa jobless na watu kupoteza ajira

Ameua watu, kubambikia watu makesi, kuonea watu mpaka hata watoto wadigo wanajua

Ameharibu biashara kupelekea watu kufunga biashara zao na wengine kufirisiwa na mabenki?

Huyo magufuli kafanya ya nini zaidi ya haya? Njia ni nyeupe sana kwa Tundu Lissu mwaka huu
 
Wakuu,

6) JPM takwimu zinambeba na wananchi wanajua matokeo yake wakimchagua tofauti na Lissu ambaye anapaswa kujikita kwenye hoja zenye matarajio ya wananchi hasa wanyonge walio wengi. Je ataweza kuaminisha wananchi ili wamchague?..

Mawazo ya Lissu ni ku-confiscate mali za CCM!
 
Hayo mambo yako yote uliyoisifia CCM hakuna hata moja la ukweli, jambo moja la msingi ni kwamba CCM inabebwa na Tume ya uchaguzi na jeshi la polisi.

Hata huyo Magufuli unayemsifia anaonekana yupo composed ni kwasababu anajua kuna kura za wizi atazipata yeye na wagombea wa chama chake majimboni. Wastaafu wanakaa miaka zaidi ya miwili bila mafao yao halafu unasema Magufuli yuko composed!.

Kuhusu Katiba Mpya unasema hilo halina maana, hapo ndipo nimekuona ulivyo myopic kwenye mambo muhimu, kwa taarifa yako Katiba Mpya ni muhimu kama au zaidi ya uchaguzi wenyewe, kwangu hakuna maana ya kufanya uchaguzi wakati playing field haiko level, ila kwako unaona sawa tu!.
 
Wakuu,

Haya ni mambo 10 niliyoona mpaka sasa kuelekea kipute cha kampeni rasmi.

1)What a match!, Mpaka sasa CCM inabebwa na watu wenye experience ambao kipindi kama hiki ndio unajua uwezo wao. Wao kelele nyingi ziko kwenye mipango (strategies) kuliko kelele na matamko ya majukwaani.

2)Tundu Lissu is impressive as usual lakini seems Chadema hawakumuandaa, experience yake ya uanaharakati ndio unaofanya aonekane active uwanjani lakini bado hajawa na madhara kihoja ingawa bado mapema. Mambo ya kusema atamshtaki JPM kwa rushwa ya kununua jogoo laki moja ni uanaharakati si level zake tena kama mgombea Urais.

3)John Pombe Magufuli yuko composed sababu ya records zake awamu hii ya kwanza.Lakini pia kwasasa nguvu kubwa ipo kwenye kupanga vyema mabeki majimboni na udiwani.Hapo ndio unapoona timu kubwa na yenye watu wazoefu inavyohandle mchezo. Ni kama wameamua kuacha wapinzani wacheze huku wao wakikamilisha ramani ya ushindi.

4) Kimbinu Chadema wanahitaji timu bora kumzunguka Lissu wakiwemo waandamizi wa serikali zilizopita akiwemo Nyarandu ili kumshape Lissu kama mgombea Urais lakini pia mipango ya kusaidia kampeni majimboni ambako hali si nzuri

5) Kimbinu CCM wana kazi kubwa ya kumaliza mchakato wa wagombea ubunge na udiwani bila mpasuko lakini maeneo mengi kimbinu wamejipanga kushinda.

6) JPM takwimu zinambeba na wananchi wanajua matokeo yake wakimchagua tofauti na Lissu ambaye anapaswa kujikita kwenye hoja zenye matarajio ya wananchi hasa wanyonge walio wengi. Je ataweza kuaminisha wananchi ili wamchague?

7) Financially CCM wako stable kuhandle kampeni kuliko Chadema ambayo imepanga pia kusimamisha wagombea majimbo yote.

8) JPM amefanikiwa kuhakikisha watendaji wake wote wanajua takwimu za mambo yaliyofanyika awamu hii hivyo itabidi kila hoja za Lissu zinazogusa takwimu ajipange otherwise akikosea atapingwa hata na makatibu tarafa. Hizo takwimu zimeimbwa muda mrefu na hata wananchi wengi wamezikariri.

9) Angalizo, Lissu usihangaike na wimbo wa katiba mpya hauna mashiko kwa wananchi wanyonge na hautampa kura. JPM pia awekeze hoja kwenye mipango mipya hasa mapinduzi kwenye kilimo na uwekezaji.

10) Wapinzani bila kusimamisha mgombea mmoja huu utakuwa uchaguzi mgumu hadi majimboni kuliko wakati wowote.

Mizania pima mwenyewe, hayo ni maoni yangu binafsi
emoji41.png
Takwimu gani za maana zinambeba Magufuli??

Za kuteka, kutesa wapinzani??

Magufuli for 5yrs consecutively hajapandisha mishahara ya watumishi wala madaraja vitu ambavyo vipo kisheria..je hizo ni takwimu za kumbeba hizo??

Amekamata na kubambikia kesi watu wangapi huyu mtu?? Wangapi wanasota mahabusu na magerezani sababu ya mkono wa chuma wa Magufuli??

Utawala ambao haueshimu Katiba na Haki za Binadamu hata kama umefanya mazuri gani ni bure..yupo wapi Ben Saanane, Azory, Kanguye na wengine?? Si ni Utawala huu ndio umewapoteza..?? Unafikiri watu hawayajui haya??

Hata ukija kwenye infrastructure, Rais gani hakujenga miundombinu kwenye Utawala wake katika Awamu zilizopita??

Eti Magufuli yupo composed...yupo composed kwenye nini?? Huyu mtu anaongea ovyo na kukashifu watu hasa wanawake kila siku halafu unasema yupo composed?? Acha mzaha wewe.. Unakumbuka alivyowakashifu watu Bukoba baada ya lile tetemeko..so he was very composed that day..mtu anaongea ovyo utafikiri sio Mkuu wa Nchi..unasema yupo composed..kila mahali akiongea ni kubaribu..

Analojivunia ni moja, anao uwezo wa kuuvuruga uchaguzi na akatangazwa ameshinda kama alivyofanya kwenye ule wa Serikali za Mitaa sababu NEC sio huru kabisa, lakini kwamba atashinda kwasababu ya takwimu ulizoziweka..hakuna kabisa.
 
Wakuu,

10) Wapinzani bila kusimamisha mgombea mmoja huu utakuwa uchaguzi mgumu hadi majimboni kuliko wakati wowote.
Huu ni ugomvi mkubwa, ni kitu ambacho hakiwezekani kabisaaa, adui mkubwa hapa ni "RUZUKU"
 
"joto la uchaguzi" litakuunguza wewe peke yako mkuu,wananchi walio wengi hawafatilii vijembe na kebehi.Kura zitakustaajabisha sana na huenda ukaachana na siasa
Tunashukuru na tunaheshimu maoni yako, ni kweli cdm wanaweza kuwa hawajajipanga vizuri, ila hukuhitaji kuweka sababu zote hizo, maana uchaguzi wa sasa hivi utafanyika kwa utashi na maamuzi ya madaraka ya Magufuli.

Subiri kadiri joto la uchaguzi linavyopanda, kama hujaona yale aliyoagiza kufanyika kwenye chaguzi zote za marudio na uchaguzi wa SM kujirudia. Naona unataka kutuaminisha huko ccm kuwa kuna mbinu sana, wakati maamuzi yote ya uchaguzi huu anayo Magufuli.
 
Back
Top Bottom